Zawadi anastahili Kaseja tyuu?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,293
12,593
Mabeki, Viungo, wawinga, na mafowadi kwenye mechi na Burundi hawakustahili pongezi pia kama za kipa wetu Juma Kaseja?
 
Mabeki, Viungo, wawinga, na mafowadi kwenye mechi na Burundi hawakustahili pongezi pia kama za kipa wetu Juma Kaseja?
Mtoto pendwa kaamua, utamfanyaje? Kwanza Ile ahadi ya awali ya kila mmoja kupewa m10 haijatekeleza.
 
Wote wanastahili...! Ila aliyejitolea kwa Kaseja yawezekana ndo uwezo wake. Sasa sisi tumpongeze kwa moyo wa kutoa halafu kuhamasisha wengine wajitoe...badala kusubiri tufungwe tuanze tulaumu
 
Wanastahili wote.
Yy kaanza na kaseja we fuata na Gadiel.
Mm nije na Nyoni na mwingine achague mtu wake hivi kwanini sisi maskini ni walalamishi sana?
 
Mpira wa miguu sio kama draft au table tennis. Zawadi isiporatibiwa Kwa ustadi inaweza kugeuka sumu kali (detromental) kwenye jambo linalokisudiwa
Mkuu hajasema kwa ajili ya kufuzu kasema nyota wake wa mmchezo.
Asa kuna man of the match wawili
 
Mkuu hajasema kwa ajili ya kufuzu kasema nyota wake wa mmchezo.
Asa kuna man of the match wawili
Kama wale wapigaji wetu wa penalties wangekosa wote kufunga bado man of the match angepewa hizo 10,000,000? Je, kama Samata asingefunga lile bao na Burundi wakapata bao 1 je, man of the match angekuwa Kaseja?
 
Zawadi ya Timu nzima,imepitia kwa nahodha.(Sina uhakika though)
zawadi, kanuni na vigezo lazima vifahamike kwa wote kabla ya game kuanza ili kuwe na equal chance kwa kila mmoja kuipigania na kuipata. Aina ya zawadi na vigezo haviwezi kuwa mfukoni kwa mtu.
 
zawadi, kanuni na vigezo lazima vifahamike kwa wote kabla ya game kuanza ili kuwe na equal chance kwa kila mmoja kuipigania na kuipata. Aina ya zawadi na vigezo haviwezi kuwa mfukoni kwa mtu.

Una hoja ya msingi Kavulata
 
Mabeki, Viungo, wawinga, na mafowadi kwenye mechi na Burundi hawakustahili pongezi pia kama za kipa wetu Juma Kaseja?
Wewe umewapa wachezaji gani zawadi mbali ya kaseja ?
au zawadi yako ni kujaribu kutafuta mapungufu ya zawadi aliyoitoa Makonda ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom