Zao la mchikichi, dhahabu mpya shambani, mbegu ya kisasa na mazao mengi zaidi

Mr Finest

Member
Aug 24, 2019
95
103
Zao la mchikichi, dhahabu mpya shambani

Note ; uzi developed
Kihiga uwanja mpya wa maboresho, mbegu za kisasa hadi magerezani TANZANIA inatumia mabilioni ya fedha kila mwaka takribani bilioni 600 kuagiza mafuta ya kula kutoka nje kwa vile kiwango cha bidhaa hiyo kinachozalishwa nchini hakikidhi mahitaji ya walaji.

Kwa kiasi kikubwa mafuta yanayozalishwa yanatokana na michikichi ambayo pamoja na kuchakatwa mafuta ya kula kama mawese kuna mengine yanayotumiwa viwandani au mafuta ya mise ambayo hupatikana hapa nchini japo kwa kiwango kidogo.

Chikichiki ndilo zao linalotoa mafuta mengi kwenye yale yanapandwa ukilinganisha na mazao mengine kama alizeti, ufuta, pamba, karanga na soya, wanasema watalaama wa kilimo.

Hata hivyo, mchikichi pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha mafuta kwa wingi lakini unalimwa kienyeji kwa miaka mingi hasa katika Mkoa wa Kigoma na kusababisha wananchi kutoona umuhimu na faida zake, anasema mtalamu wa kilimo Dk. Filson Kajimbo.

Kutokana na upungufu wa uzalishaji wa mafuta hapa nchini serikali imeziagiza Taasisi ya Kilimo (TARI) kuanza kufufua michikichi inayolimwa kwa wingi mkoani Kigoma kwa kuanza utafiti wa mbegu bora ili zizalishe mafuta, hilo linatokea baada ya kulipa kipaumbele zao hilo na sasa TARI imeanzisha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo cha Michikichi-Kihinga.

Kwa hiyo TARI Kihinga iliyoko Kigoma ndiyo inayobeba jukumu la uzalishaji wa mbegu bora za michikichi, anasema Dk Filson Kagimbo.

KUFUFUA MICHIKICHI
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili kuhusu utekelezaji wa mkakati huo ,Kaimu Mkurugenzi wa TARI Kihinga, Kagimbo, anasema uzalishaji umeanza kwa mikungu 1,290 inayochavushwa ili kuanza kutoa mbegu za michikichi iliyoboreshwa.

Dokta Kajimbo anasema takribani mbegu 2,000,000 zimeanza kuzalishwa ili kupanda miti hiyo na kupata mafuta baada ya kuchavushwa.

Hatua itakayopunguza matumizi ya fedha za kigeni kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi, kwa mujibu wa maoni yake. Anasema mbegu hiyo iliyochavushwa itatosha kupanda eneo la hekari 38,000 na kwamba kwa sasa mbegu 63,000 zimeshavunwa na zinazoweza kupandwa kwenye heka 1,260 zilizoko mkoa wa Kigoma maeneo na mingine inayolimwa michikichi.

UMUHIMU KIPEKEE
Aidha, Kagimbo anasema michikichi ni maarufu kwa mafuta ya kula na yale yanayotumika viwandani na ndilo zao pekee linalotoa mafuta mengi kwa mimea inayopandwa ardhini ukilinganisha na mazao mengine ya mafuta kama karanga, ufuta, pamba na alizeti. Anasema ukiweka mazao yote yanayotoa mafuta kila zao likawekwa kwenye eneo la heka moja, ni mchikichi pekee inayotoa mafuta mengi kuliko mengine anasema Dk. Kagimbo.

Mtaalamu huyu ambaye pia ni Mratibu wa Kitaifa wa Michikichi anasema mkakati huo utazalisha na kuongeza mafuta huku ukipunguza uagizaji wa mafuta kutoka nje . “Mafuta ya mawese yanayozalishwa na kuliwa nchini ni asilimia 0.7 hivyo kunahitajika nguvu ya ziada kwajili ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo”,anasema mtaalamu huyo wa kilimo. Anaongeza kuwa uzalishaji wa zao lamchikichi upo chini na kufikia wastaniwa tani 1.6 kwa hekta wakati nchi kama Malaysia wanapata tani nane kwa hekta kiwango ambacho kinapaswa kufikiwa na Tanzania pia.

MBEGU MPYA
Dokta Kagimba, anataja sababu kubwa ya uzalishaji mdogo kuwa ni pamoja na kutumia mbegu za kienyeji ambazo zimekuwa zikitoa mafuta kidogo kwa kuwa asilimia 90 ya michikichi yote inayolimwa nchini ni ya kienyeji.Anasema kuwa mbegu za kisasa zilizoanza kuzalishwa za michikichi aina ‘Tenera’ kwa sasa matumizi yake ni wastani wa asilimia 10 pekee ambazo zimeonyesha uwezo wa kutoa mafuta mengi Anasema asilimia 90 ya michikichi yote inayolimwa Tanzania ni aina ya Dura ambayo ni ya kienyeji.

Asilimia 10 ni aina ya Tenera ambayo ni ya kisasa. “Mbegu ya Tenera ambayo ni ya kisasa inaweza ikatoa mafuta mara tano mpaka 10 zaidi ya ile ya Dura na hivyo tukiongeza uzalishaji wake tutapata mafuta ya kutosha na ziada kupitia michikichi yetu.” Anasema mtaalamu huyo.

ARDHI DUNI
Dokta Kagimbo anatoa sababu ya uzalishaji wa michikichi kuwa chini nchini kuwa ni pamoja na udogo wa eneo linalotumika kwa uzalishaji wa zao hilo, kuwa ni udogo wa ardhi inayotumiwa kulima. Anatoa mfano Kigoma ambako michikichi inalimwa kwa wingi zaidi ya asilimia 80, eneo linalofaa ni hekta 114,000 wakati eneo lililolimwa ni hekta 23,000 kiwango ambacho ni kidogo na hivyo uzalishaji wake kuwa wa chini.

Anaeleza sababu ya tatu inayosababisha uzalishaji wa michikichi kuwa chini kuwa ni umri mkubwa wa miti iliyo mashambani hapo na kwamba kuna zaidi ya asilimia 95 ya michikichi iliyolimwa ina zaidi ya miaka 60. Anasema wakati mmea huo unatakiwa kuishi si zaidi ya miaka 30 kwa uzalishaji wenye tija , huko Kigoma imekuwa na umri wa karibu mara mbili wa ule unaotakiwa. “Mti wa mchikichi unao uwezo wa kuishi hata zaidi ya miaka 150 lakini katika umri huo, uzalishaji wakehauna tija hata kidogo na hivyo kutokuwa na faida,”anasema Dk Kagimbo.

Alisema serikali imeamua kufufua kilimo cha michikichi na imeshaanza kuchukua hatua ambayo ni kuongeza zao hilo kwenye orodha ya mazao ya kimkakati ikiwa ni pamoja na serikali kuanzisha Kituo cha Utafiti ch Kihinga TARI ambacho kinaratibu utafiti katika nyanja zote za mnyororo wa thamani wa zao hili.

TARI ILIVYOJIPANGA
Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk Geoffrey Mkamilo, anasema kuwa mpango huo wa uzalishaji wa mbegu hizo umelenga kuisaidia kuokoa zaidi ya Sh. bilioni 600 zinazotumika kwa mwaka kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nje. “Hilo linatokea wakati uwezo wa kuzalisha mafuta upo. TARI Kihinga itaongeza idadi ya watalaam wazao hilo na kuwapatia vitendea kazi kama magari na pikipiki kama alivyoagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa kikao cha wadau wa zao hilo.”anasema Dk.Mkamilo. Anaongeza kuwa serikali imetenga fedha za kutosha kwa ajili ya kufanya mageuzi makubwa kwa ajili ya kuanza kuzalisha kwa wingi miche ya chikichi bora ili kumaliza tatizo la mafuta nchini.

Mkamilo anataja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni pamoja na uzalishaji wa mbegu unaotumia teknolojia ya kisasa ya kuchavusha maua ya mchikichi aina ya Duraili iweze kuongeza uzalishaji wa mafuta kutoka tani 1.6 kwa hekta ya sasa na kufikia tani nne hadi tano kwa hekta. Mkakati mwingine ni kuongeza michikichi kwenye orodha ya mazao ya kimkakati, kama ambavyo serikali imetangaza na kwamba TARI Kihinga inafanya na kuratibu utafiti katika nyanja zote za mnyororo wa thamani wa zao hilo.

Mkamilo anasema tayari mbeguhizo zimeanza kusambazwa katika taasisi zilizochaguliwa rasmi kwa uzalishaji wa michikichi mkoani Kigoma.Anazitaja kuwa ni pamoja naGereza la Kwitanga ambalo limepewa mbegu 30,000 zinazotosha eneo la ekari 600, kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa *JKT) Bulombora, iliyopewa mbegu 19,000 ambazo zinapandwa kwenye ekari 393, na Gereza la Ilagala mbegu 10,000 zinazoweza kupanda kwenye ekari 200.Mkurugenzi huyo anasema TARI kwakushirikiana na wazalishaji wa kampuni binafsi wa mbegu wana mkakati wa kuzalisha mbegu milioni 5.0 kwa mwaka.

Aidha, ndani ya miaka mitatu zitakuwa zimezalishwa mbegu milioni 15 za kutosha eneo linalofaa kulima michikichi mkoa wa Kigoma kabla ya kuhamia mikoa mingine inayolima zao hilo ya Mbeya, Morogoro, Tanga, Pwani, Dar es Salaam na Kagera.Dokta Mkamilo anasema baada kuwapawakulima mbegu bora katika eneo lote linalofaa kwa michikichi, likapandwa na yote iliyozeeka ikatolewa na kupandwa ya kisasa, uzalishaji wa mafuta utaongezeka na hivyo uangizaji wa mafuta ya kula kutoka njeutakwisha.

WADAU UZALISHAJI
Mkuu wa Gereza la Kwitanga lililopo Kigoma, Dominic Kristian, ambaye ametoa shamba kwa ajili ya uchavushaji wa michikichi anasema kuwa tayariwameshaanza kupanda mbegu hizo baada ya kuchavushwa na hekta nyingine zinaendelea lengo ni kupata miche yenye mikungu inayotoa mawese mengi.Mkuu huyo wa gereza anasema kuwa kwa kushirikiana na wadau watahakikisha wanafikisha malengo waliyopewa na serikali ifikapo mwakani kwa kuwa utayarishaji wa mashamba hayo umekamilika.

Nawakumbusha kwa wale wawekezaji huu ndio muda muhafaka wa kufanya uwekezaji .
Maeneo ya kufanya uwekezaji
-Ukulima wa Miche ya mchikichi
-Kuanzisha viwanda vya kuchakata mafuta ya mawese
-kuanzisha viwanda vya kuchakata mise
-Utenengenezaji wa sabuni

Uwekezaji huu ,baada ya miaka kadhaa at least miaka 3-4 ijayo , hawa ndio watakuwa matajiri wapya mjini kwa maana watakuwa tayari kwenye solo na uzoefu wakutoka kwenye hii sekta.

Nakaribisha maoni
 
Tunaomba ufafanuzi zaidi kuhusu kupatikana kwa mbegu nje ya Kigoma au lazima iwe Kigoma? Je kwa ekari moja ni miche mingapi ya inapandwa? Uzaaji wake ni baada ya muda gani?
 
Nashukuru kwa habari hii. Ingependeza zaidi tungejua kuhusu upatikanaji wa miche(mbegu), ardhi gani inakubali zao hili(mikoa na wilaya gani) na masoko- mnunuzi mkubwa kwa sasa ni nani?
 
Mwaka jana ilikuwa korosho kila mkoa, wewe unaleta chikichi. Munaamini wakulima hatujui lolote, eti? Tatizo la kilimo chetu siyo mbegu, ardhi, au uelewa. Tatizo ni soko la mazao yetu. Lete masoko mengine yote yatajirekebisha yenyewe; mbegu tutatafuta wenyewe, mbolea tutaitafuta. Mbinu za uzalishaji hazihitaji longolongo ya utafiti.
 
Mbegu za michikichi hii ya kisasa kwa kiasi kikubwa inazalishws na TARI
Maeneo mengi KILIMO hiki kina kubali vizuri , mikoa ya pwani yote , kigoma , morogoro , Dodoma , singida.

Kwa Sasa kwa Tanzania soko la mchikichi bado sio kubwa kwa Sababu ya utegemezi mkubwa wa zao ili kutoka nje ya nchi . Kuna uwezekana mkubwa baada ya hii miaka isiyopungua 2-3 , utegemezi huo ukaondoka kabisa kwa maana Kama taifa litajotolesheza na mafuta

Nashukuru kwa habari hii. Ingependeza zaidi tungejua kuhusu upatikanaji wa miche(mbegu), ardhi gani inakubali zao hili(mikoa na wilaya gani) na masoko- mnunuzi mkubwa kwa sasa ni nani?
 
Zao hili mbegu za kisasa kabisa zinapatikana maeneo mengi na sio kigoma tu . Kwenye ofisi za TARI za kila mkoa zinapatikana , mikoa Kama Tanga , morogoro , pwani
Lakini pia unaweza kuzipata kwa watenezaji wa binafsi

Pia kila eka moja inapaswa kuchukua Miche isiyopungua 50-55
Mche mmoja unawezo wa kuanza kuvunwa baada ya miaka mitatu tu na inauwezo zaidi ya Mara 5-10 ya uzalishaji ukilinganosha na Miche ya kienyeji , unawezo wa kutoa Lita 20-22 ya mafuta kwa mwaka
Tunaomba ufafanuzi zaidi kuhusu kupatikana kwa mbegu nje ya Kigoma au lazima iwe Kigoma? Je kwa ekari moja ni miche mingapi ya inapandwa? Uzaaji wake ni baada ya muda gani?
 
Kwa kiasi kikubwa soko letu la ndani limeadhiliwa na masoko ya nje , ambapo wa Tz wengi wametengeneza mazoea ya kuazigiza na kuzidhamini bidhaa za nje not only kwa mchikichi , ni hata kwa mazao mengine pia
Nini kifanyike

[ To stabilize internal market ]
Kwanza Kama waTz tudhamini na kutumia bidhaa zetu
Pili serikali ilinde na kutoa ruzuku kwa bidhaa zetu na kuweka vikwazo kwa biddhaa ambazo tunazalishi , zisiagizwe kutoka njee
Tuongeoze dhamani ya bidhaa zetu

Tuanze kusaka masoko ya nje kwa bidhaa zetu wenyewe [ tukisha jitosheleza ]
Na pia kwa kuwa uhitaji wa mafuta Ni mkubwa nchini , nadhani mchikichi unaenda kuondoa tatzo la mafuta Tz

[ Tutegemee uzalishaji utakao pita kiasi kwa miaka 5 ijayo , na tujiandae kwa masoko ya nje , EAC , SADC , uerope na America ]
Nadhani kwa hapo taratibu taratibu tutatatua tatizo la masoko
Nadhani korosho kwa sasa[ mwaka huu ] hakujatokea tatzo bado , serikali ilijifunza vyema
Mwaka jana ilikuwa korosho kila mkoa, wewe unaleta chikichi. Munaamini wakulima hatujui lolote, eti? Tatizo la kilimo chetu siyo mbegu, ardhi, au uelewa. Tatizo ni soko la mazao yetu. Lete masoko mengine yote yatajirekebisha yenyewe; mbegu tutatafuta wenyewe, mbolea tutaitafuta. Mbinu za uzalishaji hazihitaji longolongo ya utafiti.
 
Kuna baadhi ya maeneo kigoma unayapata kwa 100k au chini ya hapo [ Mashamba Poli ]
Ardhi ya kigoma ni ardhi nzuri na yenye rutuba zakutosha.

Pia utaweza ardhi Hiyo ya kigomainakubali mazao mengi ikiwemo kwa kutaja machache Mahindi, maharagwe, viazi na mengine mengi.
 
Kuna baadhi ya maeneo kigoma unayapata kwa 100k au chini ya hapo [ Mashamba Poli ]
Ardhi ya kigoma ni ardhi nzuri na yenye rutuba zakutosha
Pia utaweza ardhi Hiyo ya kigomainakubali mazao mengi ikiwemo kwa kutaja machache Mahindi , maharagwe , viazi na mengine mengi
Naomna connection mkuu
 
Mkuu Naomba Connection ya kununua kwa hizo bei
 
Kwa kiasi kikubwa soko letu la ndani limeadhiliwa na masoko ya nje , ambapo wa Tz wengi wametengeneza mazoea ya kuazigiza na kuzidhamini bidhaa za nje not only kwa mchikichi , ni hata kwa mazao mengine pia
Nini kifanyike

[ To stabilize internal market ]
Kwanza Kama waTz tudhamini na kutumia bidhaa zetu
Pili serikali ilinde na kutoa ruzuku kwa bidhaa zetu na kuweka vikwazo kwa biddhaa ambazo tunazalishi , zisiagizwe kutoka njee
Tuongeoze dhamani ya bidhaa zetu

Tuanze kusaka masoko ya nje kwa bidhaa zetu wenyewe [ tukisha jitosheleza ]
Na pia kwa kuwa uhitaji wa mafuta Ni mkubwa nchini , nadhani mchikichi unaenda kuondoa tatzo la mafuta Tz

[ Tutegemee uzalishaji utakao pita kiasi kwa miaka 5 ijayo , na tujiandae kwa masoko ya nje , EAC , SADC , uerope na America ]
Nadhani kwa hapo taratibu taratibu tutatatua tatizo la masoko
Nadhani korosho kwa sasa[ mwaka huu ] hakujatokea tatzo bado , serikali ilijifunza vyema
Usiseme wa-Tanzania sema viongozi. Unajua mfuta ya michikichi yanavyoagizwa nje ya nchi na jinsi Mukulo alivyoondoa ushuru. Uchumi wa wahindi haufiki kokote! Wahindi walihonga Kenya, wakaenda Uganda na kumalizia Tz. Nchi zote hizi zikaondoa kodi kwa kisingizio cha mafuta ghafi.

Hali hii haihitaji kubadiri tabia, ni kusimamia na kuondoa sheria mbovu za kibiashara. Alizeti itapata soko, michikichi itazalisha mafuta na TZ tutakula mafuta yetu.
 
Mwaka jana ilikuwa korosho kila mkoa, wewe unaleta chikichi. Munaamini wakulima hatujui lolote, eti? Tatizo la kilimo chetu siyo mbegu, ardhi, au uelewa. Tatizo ni soko la mazao yetu. Lete masoko mengine yote yatajirekebisha yenyewe; mbegu tutatafuta wenyewe, mbolea tutaitafuta. Mbinu za uzalishaji hazihitaji longolongo ya utafiti.
Bibi zetu walipanda chikichi hazikuwatoe je sisi zitatutoa kama mifumo ni ileile ya mabibi.Hata processing ni vivilevile.

Binafsi nilitaka kupanda chikichi kwetu kigoma,nikazama kusoma articles zinazohusu chikichi, nyumbani Tz hakuna tafiti zozote, nyingi nilizipata kutoka Asia, Singapore, Thailand, Vietnam nk.

Mambo makubwa niliyoyapata ni kwamba chikichi ni zao ka kiviwanda hata biofuel ni zao mojawapo, wenzetu kunaviwanda vinatumia mawese kuendesha mitambi yao.

Vyakula vingi ulaya wanavitengeneza na mawese. Nk, nk
Nilipochunguza hapa home nikagundua mawese yanatumika zaidi kwa sabuni na mafuta ya kula kidogo.Products nyingi za mawese zinatupwa kuanzia makanfi(lugha ya kigoma kambakamba baada ya kuchuja), maganda ya mise, chelewa,majani.

Bei ya mawese lita haizidi sh1500 kulinganisha na mafuta mengine.
Binafsi nilitupiliambali wazo la mawese nikaamua kununua mashamba ya kupanda Parachichi.

Parachichi unauza ghafi shambani chikichi una hudumia shamba, una vuna ngazi, unapeleka nyumbani,unavundika,unakamua unapeleka sokoni nk. Mkulima wa parachichi Alishasahau anasubiri mavuno ya pili were unahangaika .Chikichi kila siku upo shamba kuhudumia shamba.

Mambo ni mengi sana, mkigoma bora aanze kupanda korosho,ndizi,kahawa, parachichi,maharage,afuge samaki chikichi ziwe za mwisho.

Wanakigoma tusipochekecha akili tutaendelea kuwa masikini, wanasiasa wana ajenda zao nawe mkulima weka ajenda zako za kuutokomeza

umasikini.Kigoma ni mkoa wenye fursa nyingi Ila umedumaa hata wakazi wake hawana siha wala furaha ya maisha.Binafsi huwa naumia sana kuuona mkowa wetu ukiwa wa mwisho kimaendeleo.

Kupanga ni kuchagua, chxgua kuendelea kuwa masikini au kuutokomeza umasikini.Kamwe mwanasiasa hawezi kuutokomeza umasikini Bali ni were mwenyewe.Chagua zao la kukutoa ktk umasikini na so zao la kuwasaidia wanasiasa kudhibi mfumuko wa bei za mafuta.Kigoma muwe na akili za demand and supply,sio mtu anawaambia tu pandeni nanyi mnakulupuka bila kutafiti.

Siku mkiuza Lita sh 500 msije kumlaumu mtu, kigoma itainuliwa na watu wenye akili timamu.
 
Mkuu umeongea kwa hisia sana, mkoa wa kigoma fursa zipo ila watu wamelala sijui kuna nini hapo kati. Wageni naona wanazifakamia hizo fursa vilivyo, labda wazawa nao watastuka.
 
Unajua wageni ndio wanachangamsha mji.Binafsi nipo nje ya kigoma,napoenda nyumbani barabara imejaa mapori ya miti lakini mikoa mingine barabara yote imejaa mazao mfano mkoa wa Moro, toka mikumi mpaka ifakara utaona ndizi, miwa mpunga nk Mapori sio mengi ila Tabora kwenda kigoma kumejaa mapori tu, hivi ina maana hakuna uzalishaji.
Kigoma inafaa sana kwa ufugaji samaki lakini huwezi ona miradi mikubwa ya ufugaji.Watu wa kigoma tumelala sana.
 
Danganyweni hivyo hivyo,huko kanda ya ziwa wakulima hua wanadanganywa eti Pamba ni dhahabu nyeupe,nenda kaangalie sasa maisha ya hao wakulima wa Pamba.Unaweza kulia.
 
Mkuu biashara ambayo hujui utamuuzia nani sifanyi.Watanzania wengi gawapendi kula mafuta ya mawese, wamelogwa na alizeti.
Serikali ikete wawekezaji sio kushawishi tu wakulima.
Wakulima wajifunze Ku process mawese kuwa bidhaa mbalimbali hapo haita wakata ila kama watasubiri wahindi waje wanunue itakula kwao.
Mawese yanagoa bidhaa nyingi sana, ika wakulima hawajui chochote.
 
Unajua wageni ndio wanachangamsha mji.Binafsi nipo nje ya kigoma,napoenda nyumbani barabara imejaa mapori ya miti lakini mikoa mingine barabara yote imejaa mazao mfano mkoa wa Moro, toka mikumi mpaka ifakara utaona ndizi, miwa mpunga nk Mapori sio mengi ila Tabora kwenda kigoma kumejaa mapori tu, hivi ina maana hakuna uzalishaji.
Kigoma inafaa sana kwa ufugaji samaki lakini huwezi ona miradi mikubwa ya ufugaji.Watu wa kigoma tumelala sana.
Ardhi ipo ya kutosha ila sasa sijui ni hakuna exposure ya kinachoendelea huko duniani au la! Kingine hawa watu wa huku wanawaza masoko ya humuhumu ndani ya mkoa au wilaya zao, hawajiongezi ili hata kidogo kutafta masoko yatakayowalipa ili kutoendelea kulima kwa ajili ya matumbo tu.

Ila pia mkuu unaonaje uwekeze pia huko hata kidogo kama namna ya kuwapa mwanga watu wa jamii yako?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom