Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
Date::2/18/2010
Mseto Zanzibar baada ya miezi 3
MUUNDO wa Serikali ya Mseto visiwani Zanzibar utajulikana katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Idd Hassan Pandu, amesema.
Alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalumu na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC1.
"Ofisi yangu imekwisha pokea rasimu ya muundo wa Serikali ya Mseto, lakini pamoja na majukumu iliyonayo Zec, itabidi ifanye kazi ya kupokea kura za maoni ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa na kisha itoe majibu ya kura hizo za maoni,"alisema Pandu.
Alisema baada ya kupokea muswada huo anaufanyia kazi kabla ya kuuwasilisha Nec kwa ajili ya utekelezaji.
Kwa mujibu wa Pandu, kazi ya Zec itakuwa ni kusimamia mchakato wa kura za maoni kuhusu uanzishwaji wa serikali hiyo.
Hata hivyo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema hakuna umuhimu wa kupiga kura za maoni kuhusu suala hilo kwa kuwa Wanzazibar wamekwisharidhia mfumo huo mpya wa serikali.
Alisema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo hicho jana kama ilivyokuwa kwa mwanasheria mkuu huyo wa serikali.
"Kwa kawaida majibu katika kura zozote za maoni ni ndio au hapana. Sasa kwa Zanzibar hili halina umuhimu wowote kwa kuwa tayari wamekwishakubali suala hili,"alisema Dk Bana.
Dk Bana ambaye ni mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa chuoni hapo pia alieleza sababu za kupinga kura za maoni kuwa ni kuondoa gharama zisizokuwa za lazima katika mchakato huo.
Katika mkutano wa siku mbili wa Nec uliofanyika Jumapili na Jumatatu iliyopita mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, pamoja na mambo mengine Nec iliridhia rasmi kuwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi visiwani Zanzibar iundwe Serikali ya Mseto.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM John Chiligati alisema NEC imefanya hivyo kwa maslahi ya Zanzibar na Wazanzibar ili kuondoa malumbano na chuki iliyodumu kwa muda mrefu visiwani humo. Alisema tangu NEC iliyokutana Butiama walikubaliana Zanzibar kuwe na Serikali ya Mseto, lakini CUF walisusia mazungumzo hivyo jambo hilo likakosa msukumo.