Zanzibar yakabiliwa na ukiukwaji wa haki za binadamu

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
597
1,000
Zanzibar imetajwa kukabiliwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu, katika ripoti iliyotolewa na shirika la haki za binaadamu, ikiungana na nchi nyingine duniani kukabiliana na madhila kama hayo.

Wakati wanaharakati wa haki za binaadamu wakiwemo wa Shirika la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch wakiendelea kulalamika kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadam katika nchi mbali mbali duniani, Zanzibar pia imetajwa leo katika ripoti kuwa inakabiliwa na hali kama hiyo.

Katika ripoti inayoangazia haki za binaadamu Zanzibar, watayarishaji wa ripoti hiyo kutoka "kituo cha huduma za sheria" wasema bado utekelezaji wa haki ni tatizo ambapo udhalilishaji, mauaji, watu kupigwa, na matumizi mabaya ya madaraka bado vinaongoza katika ukiukwaji wa haki.

Akizindua ripoti hiyo mjini Zanzibar kwa watu kutoka sekta ya umma na binafsi, Mwanasheria maarufu Jaji Mshibe Ali Bakar alisema kila kukicha haki za binadamu zinaendelea kukiukwa katika ngazi zote na kuathiri zaidi watu maskini.

Alisema mara nyingi wakati wa uchaguzi kinachoangaliwa ni ule uchaguzi wenyewe lakini ili ujue uchaguzi mzuri ni kuangalia utaratibu mzima wa uchaguzi kuanzia uandikishaji, kampeni za uchaguzi na kutangazwa matokeo yenyewe.

Ripoti hiyo pia imeelezea haki za mtoto zinavyokanyagwa na masuala ya ubakaji yalivyokithiri katika visiwa vya Unguja na Pemba huku mahakama zikilaumiwa kwa kuzifuta kesi nyingi kwa kukosekana ushahidi na katika hilo.

Katika ripoti hiyo imetajwa kuwa idadi ya watu waliouliwa imeongezeko kutoka wanne Mwaka 2015 hadi mauaji 34 Mwaka jana, Pamoja na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya haki zao kubinywa.

Akitoa maoni yake mbele ya hadhara hiyo Rais wa chama cha wanasheria Zanzibar Omar Said Shaaban aliipongeza ripoti hiyo lakini akashauri wadau wapewe muda wa siku nzima wa kuipokea na siku ya pili kuijadili.

Katika ripoti hiyo pia limetajwa suala la uhuru wa mahakama katika kufanya kazi zake na kutaja haki ya washitakiwa kupewa dhamana katika kesi za jinai.

Mwandishi: Salma Said.

Mhariri: Josephat Charo DW.
 
Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
9,582
2,000
Pia uminywaji wa haki za Wengine kwa kisingizio cha dini.

Wengine kupigwa mijeledi kwa kula Chakula katika mwezi fulani. Huku serikali ikiwa na Baraka zake juu ya hilo.

Punguani Waheed.
Hawa wanaopigwa kwa kula ovyo ovyo,huwa wanafanya kusudi,kama unataka kula,kaa kwako ndani kula,na ndio kawaida,hata siku zisizo za mfungo,mtu unakula nyumbani kwako.Na hao wanaopigwa ni waislamu,asiye muislamu haguswi.
Utakuta mtu,ameingia ndani ya uislamu,lakini hafungi.Kama hufungi ukila kwako,nani atakuletea tabu.Lakini unakula barabarani,kwa makusudi.
 
hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,318
2,000
Kuna utofauti mkubwa kati ya police service na police force.
Kwa tanzania wanatumia mfumo wa police force.

Kwahiyo hilo swala kupigwa wananchi labda waje wabahatike waje waitoe ccm madarakani
Na wabadilishe jeshi la polisi kutoka police force kuja kuwa police service.

Kwasababu serikali iliyopo madarakani kwasasa haiwezi kufanya hivyo kwasababu nguvu yake kubwa inategemea jeshi la police na mfumo wake wa police force.
 
Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,767
2,000
aleesha
lengo la wewe kuleta habari ni kuonesha ukiukwaji wa haki za binadamu kwa misingi ya kisiasa
lakini nakuambia siasa katika jimbo la zanzibar ina nafasi ndogo sana juu ukiukwaji huo
haki za binadamu zanzibar kwa kiwango kikubwa hutekelezwa kwa misingi ya dini hasa kiislamu ilhali zanzibar ni huru juu ya masuala ya kiimani
 
Mtu anapojaribu kuelimisha ili afahamike zaidi hutoa na mifano, hem naomba unipe mfano au mifano nikubaliane na weye. Samahan lakin
 
kaburungu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,321
2,000
Hawa wanaopigwa kwa kula ovyo ovyo,huwa wanafanya kusudi,kama unataka kula,kaa kwako ndani kula,na ndio kawaida,hata siku zisizo za mfungo,mtu unakula nyumbani kwako.Na hao wanaopigwa ni waislamu,asiye muislamu haguswi.
Utakuta mtu,ameingia ndani ya uislamu,lakini hafungi.Kama hufungi ukila kwako,nani atakuletea tabu.Lakini unakula barabarani,kwa makusudi.
Kula hovyo hovyo ndio kukoje, halafu unaposema wanafanya kusudi unamaanisha nini? Na kama haitoshi unampangia mtu sehemu ya kula eti kama unataka kula kaa kwako. Na unaposema siku zisizo za mfungo mtu unakula nyumbani, mantiki yako ni ipi hasa! Acheni kuwa manual ya maisha ya wengine mkuu.
 
aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
597
1,000
Kuna utofauti mkubwa kati ya police service na police force.
Kwa tanzania wanatumia mfumo wa police force.

Kwahiyo hilo swala kupigwa wananchi labda waje wabahatike waje waitoe ccm madarakani
Na wabadilishe jeshi la polisi kutoka police force kuja kuwa police service.

Kwasababu serikali iliyopo madarakani kwasasa haiwezi kufanya hivyo kwasababu nguvu yake kubwa inategemea jeshi la police na mfumo wake wa police force.
Najaribu kulinganisha nchi nlizotembea na nchi ninayoishi nakubaliana na ww 100%. Na pia najaribu kuuangalia uchaguzi wa majuzi wa Uiengereza ulivyoendesha na uchaguzi wa nchi yangu kweli kuna tofauti sana kwa upande wa Polisi
 
aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
597
1,000
Pia uminywaji wa haki za Wengine kwa kisingizio cha dini.

Wengine kupigwa mijeledi kwa kula Chakula katika mwezi fulani. Huku serikali ikiwa na Baraka zake juu ya hilo.

Punguani Waheed.
Naona hili suala la kula limekuumizeni sana ila kiufupi tu halikuanza jana na leo na pia miaka yote ya nyuma kila aliekuja Zanzibar alikua akiuheshimu huu mfungo ila hao wanaokula na kuvaa hovyo wanafanya makusudi kujaribu nini kitatokea. Unaenda ugenini watu na mila zao unataka kutumia nguvu kuwabadilisha i think its not fair.
 
Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,767
2,000
Mtu anapojaribu kuelimisha ili afahamike zaidi hutoa na mifano, hem naomba unipe mfano au mifano nikubaliane na weye. Samahan lakin
hebu soma hoja namba 5 halafu uniambie unaakisi nini mtu unapokutana na suala kama hilo ikiwa unaamini mwenye wazo hilo mzanzibari
 
Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,380
2,000
Hawa wanaopigwa kwa kula ovyo ovyo,huwa wanafanya kusudi,kama unataka kula,kaa kwako ndani kula,na ndio kawaida,hata siku zisizo za mfungo,mtu unakula nyumbani kwako.Na hao wanaopigwa ni waislamu,asiye muislamu haguswi.
Utakuta mtu,ameingia ndani ya uislamu,lakini hafungi.Kama hufungi ukila kwako,nani atakuletea tabu.Lakini unakula barabarani,kwa makusudi.
Wale Wazungu waliokatwa visu hotelini walkuwa waislam?

Unamfahamuje mtu kuwa ni muislama ama siyo musilam kwa kula? Kwamba namna hii ya kula ni ya muisilam na hii ni ya asiyekuwa musilam?

Sheria gani imelaimisha watu kulia nyumbani tu wakiwa Zanzibar?

Kinachowafanya wafungaji washindwe kufunga kwa kuwa kuna mtu anakula ni kwamba mungu wao mrafi sana anatamani kula akiona watu wanakula na kusahau kuwahudumia hao wanaoshinda na njaa mchana AU ni hulka ya kawaida waliyonayo waislam ya wivu wa kutaka watu wote wawe kama wao?

Mbona dini zingine huwa wanafunga na hata huwez ikujua kuna watu wanafunga tena kwa muda mrefu mara nyingine zaidi ya mwezi na wala hakuna anayezuiwa kula h ata majumbani kwao? Huku kufunga kwa hawa watu kunakuwaje kwa shari namna hiyo? wanafunga ili kukoleza hasira au wanafunga kama show?
 
chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,714
2,000
Kula hovyo hovyo ndio kukoje, halafu unaposema wanafanya kusudi unamaanisha nini? Na kama haitoshi unampangia mtu sehemu ya kula eti kama unataka kula kaa kwako. Na unaposema siku zisizo za mfungo mtu unakula nyumbani, mantiki yako ni ipi hasa! Acheni kuwa manual ya maisha ya wengine mkuu.
Kuheshimu mila na tamaduni za watu ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu,miaka ya nyuma kuna kijana alihukumiwa mahakamani kwa kusema Jesu sio Mungu,sioni kama itakuwa busara kuadhini "allahu Akar" kanisani....

Makusudio yangu lazima Wazanzibari waheshimiwe mila na tamaduni zao,asilimia 95 ya wenyeji wa Zanzibar ni waislam,huu mungano hauna maana dini na tamaduni za Zanzibar zifutike
 
kaburungu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,321
2,000
Kuheshimu mila na tamaduni za watu ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu,miaka ya nyuma kuna kijana alihukumiwa mahakamani kwa kusema Jesu sio Mungu,sioni kama itakuwa busara kuadhini "allahu Akar" kanisani....

Makusudio yangu lazima Wazanzibari waheshimiwe mila na tamaduni zao,asilimia 95 ya wenyeji wa Zanzibar ni waislam,huu mungano hauna maana dini na tamaduni za Zanzibar zifutike
Ni kwa sababu hujui maana ya Allah Akbar ndio maana unasema sio busara kusema hivyo kanisani. Kuna shida gani mtu akisema Mungu mkubwa kanisani?

Heshima hailazimishwi wala haiombwi ipo tu na wala heshima haina muda, kipindi, au msimu wa utekelezaji wake ipo na itaendelea kuwepo.
 
Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
9,535
2,000
Zanzibar imetajwa kukabiliwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu, katika ripoti iliyotolewa na shirika la haki za binaadamu, ikiungana na nchi nyingine duniani kukabiliana na madhila kama hayo.

Wakati wanaharakati wa haki za binaadamu wakiwemo wa Shirika la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch wakiendelea kulalamika kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadam katika nchi mbali mbali duniani, Zanzibar pia imetajwa leo katika ripoti kuwa inakabiliwa na hali kama hiyo.

Katika ripoti inayoangazia haki za binaadamu Zanzibar, watayarishaji wa ripoti hiyo kutoka "kituo cha huduma za sheria" wasema bado utekelezaji wa haki ni tatizo ambapo udhalilishaji, mauaji, watu kupigwa, na matumizi mabaya ya madaraka bado vinaongoza katika ukiukwaji wa haki.

Akizindua ripoti hiyo mjini Zanzibar kwa watu kutoka sekta ya umma na binafsi, Mwanasheria maarufu Jaji Mshibe Ali Bakar alisema kila kukicha haki za binadamu zinaendelea kukiukwa katika ngazi zote na kuathiri zaidi watu maskini.

Alisema mara nyingi wakati wa uchaguzi kinachoangaliwa ni ule uchaguzi wenyewe lakini ili ujue uchaguzi mzuri ni kuangalia utaratibu mzima wa uchaguzi kuanzia uandikishaji, kampeni za uchaguzi na kutangazwa matokeo yenyewe.

Ripoti hiyo pia imeelezea haki za mtoto zinavyokanyagwa na masuala ya ubakaji yalivyokithiri katika visiwa vya Unguja na Pemba huku mahakama zikilaumiwa kwa kuzifuta kesi nyingi kwa kukosekana ushahidi na katika hilo.

Katika ripoti hiyo imetajwa kuwa idadi ya watu waliouliwa imeongezeko kutoka wanne Mwaka 2015 hadi mauaji 34 Mwaka jana, Pamoja na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya haki zao kubinywa.

Akitoa maoni yake mbele ya hadhara hiyo Rais wa chama cha wanasheria Zanzibar Omar Said Shaaban aliipongeza ripoti hiyo lakini akashauri wadau wapewe muda wa siku nzima wa kuipokea na siku ya pili kuijadili.

Katika ripoti hiyo pia limetajwa suala la uhuru wa mahakama katika kufanya kazi zake na kutaja haki ya washitakiwa kupewa dhamana katika kesi za jinai.

Mwandishi: Salma Said.

Mhariri: Josephat Charo DW.
Mwandishi mpuuzi huyu, watu 35 wamekufa tangia 2015 anashangaa Wakati watu 35 wamekufa kibiti Mwaka huu huu haoni ajabu, analalamikia Zanzibar! Ovyo kabisa huyu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom