Zanzibar yafanikiwa vita dhidi ya malaria kabla ya 2023, huku China ikitoa mchango katika uvumbuzi wa Artemisinin

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111221346851.jpg

Pili Mwinyi

Malaria ni ugonjwa hatari sana unaotokana na mbu jike ambaye anaambikiza binadamu na baadaye akuwa na homa kali, baridi, na mafua. Ugonjwa huu unaweza kusababisha kifo au hata matatizo ya akili pale malaria inapopanda kichwani. Mafanikio makubwa yamepatikana duniani katika kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa malaria, lakini gonjwa hili bado linaendelea kuwa tatizo kubwa la afya ya umma, huku takriban watu bilioni 3.2 duniani kote wakiwa katika hatari ya kuambukizwa.

Kwa visiwa vya Zanzibar, Tanzania hivi sasa ugonjwa huu umebaki simulizi tu midomoni mwa watu wengi. Kwani wengi wao ni ama hawajawahi kuambukizwa hapo awali, au kwa muda mrefu sana. Yote haya ni kwasababu Kisiwa hiki kimefanikiwa kupunguza maambukizi ya malaria hadi chini ya asilimia moja, na kwa sasa kuna watu wachache mno wenye ugonjwa huu, wengi wao wakiwa wasafiri na wafanyakazi wahamiaji.

Zanzibar ni miongoni mwa maeneo ya Afrika yaliyoweza kupunguza kwa kiasi kikubwa mzigo wa malaria kutoka asilimia 40 mwaka 2005 hadi chini ya asilimia 1.5 mwaka 2011–2012. Kulingana na utafiti wa hivi karibuni wa viashiria vya malaria, maambukizi ya malaria visiwani Zanzibar sasa ni chini ya 0.07%. Kuongezeka kwa hatua za kudhibiti malaria kumesababisha kupungua kwa kasi kwa matukio ya malaria Zanzibar.

Mafanikio haya ya kupunguza maambukizi ya malaria katika jamii yamechangiwa na utekelezaji wa hatua zilizoidhinishwa na zinazofaa, zikiwemo matibabu muafaka kwa kutumia tiba mchanganyiko ya artemisinin, kuongeza matumizi ya vyandarua vyenye dawa za kuua wadudu na vinavyodumu kwa muda mrefu, kampeni zilizofanikiwa za kunyunyiza dawa majumbani, na kufanyika kwa vipimo vya haraka vya malaria katika vituo vya afya.

Ni kweli, kwa juhudi hizi zilizochukuliwa na serikali ya Zanzibar, zinastahili pongezi kubwa na pia iwe mfano wa kuigwa na maeneo mengine ya Tanzania kwa ujumla na Afrika, ili tuweze kufikia lengo la kutokuwa na mgonjwa wa malaria hata mmoja ifikapo 2023.

Tunapotaja mbinu za kupambana na malaria hatusahau mchango mkubwa unaotokana na dawa mchanganyiko ya artemisinin ambayo ilianza kutumika Zanzibar mwaka 2005. Artemisinin ni dawa ambayo imevumbuliwa na mwanasayansi wa kike wa China aliyepata tuzo ya Nobel, Profesa Tu Youyou, ambaye aliangalia zaidi upande wa tiba za jadi ili kutibu malaria. Kwa ushujaa wake Profesa Tu Youyou alijitolea kuwa binadamu wa kwanza kufanyiwa majaribio ya dawa hizo. Hatimaye alifanikiwa kuokoa maisha ya mamilioni ya watu na sasa dawa hizi zimekuwa mchango mkubwa sana visiwani Zanzibar na barani Afrika kwa ujumla.

Wakati dunia ikiwa na lengo la kutokomeza malaria kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2030, visiwa hivyo tayari vimeshapiga hatua kubwa ya kutokomeza malaria kabla ya kufikia mwaka 2023. Haya yote yanatokana na ushirikiano mkubwa na wa karibu unaooneshwa kati ya wananchi na serikali yao.

Ingawa Zanzibar imedumisha kupunguza maambukizi ya malaria chini ya asilimia moja kwa muongo mzima uliopita, lakini kuutokomeza moja kwa moja ugonjwa huu bado ni changamoto kubwa. Utafiti wa mwaka 2019 ulioongozwa na Kituo cha Mpango wa Mawasiliano cha Johns Hopkins, Taasisi ya Afya ya Ifakara na Mpango wa Kutokomeza Malaria Zanzibar unashauri kuwa ili kukabiliana na changmaoto hizo, ni vyema kuelewa tabia ya binadamu wakati wa usiku, wakati mbu wa malaria wanapouma.

Pia utafiti huo umeshauri kuwa, kuwalenga watu wanaofanya kazi na kujumuika nje ya nyumba nyakati za jioni pamoja na wasafiri na wafanyakazi kutoka nje ya visiwa ambao wanaweza kupeleka malaria visiwani, kunaweza kuongeza kasi ya kutokomeza ugonjwa huo.

Kwa kuwa hatua nyingi zinazochukuliwa na mamlaka ya Zanzibar zinalenga majumbani tu, basi sio mbaya kufuata ushauri ulitolewa na taasisi hizo zilizofanya utafiti kwa kuanza kuangalia maambuklizi ya nje ya nyumba ili kumaliza kabisa hiyo asilimia ndogo ya maambukizi ya malaria.
 
Nimeishi huko kama miezi sita hivi,maralia ipo ila dawa za maralia ndio hazipatikani utazunguka pharmacy zote,hata hospital hakuna dawa za maralia ilibidi niagize kwa mtu anayetoka bara kuja Zanzibar.
 
Umeongea pointi ,wanachokifanya wazanzibar ni kupambana na uhalisia!!

Kuna jamaa yangu Yuko huko yeye mwenyewe amewahi niambia maneno Kama haya yako,na hii ilikuwa mwaka 2018,na nasikia hata kuriport tu kuwa una malaria ni balaa huko Zanzibar

Sasa sijui wanafanya haya ili kumfurahisha nani?
 
Hivi ninavyoandika bado nipo huku Zanzibar kikazi na huo ndio uhalisia ulivyo,hupati dawa za maralia wao wanasema walishaipiga vita ila kiuhalisia bado ipo,japo sio kali kiivyo.Niliagiza dawa bara tena zilikua za aina zote za maralia maana hali ilikua mbaya kwangu,then nilitumia kwa maelekezo tu kutoka kwa ndugu yangu mmoja daktari huko, imagine unatumia dawa bila kupima lakini dalili zote unaona ni maralia.
 
Hatua nzuri...umasikini + magonjww ni kifo..

Shida wanasiasa na watunga sera hanaangalia bajeti ya madawa na vifaa tiba na kujenga vituo vya afya..

Hawataki kabisa kuwekeza kwenye udhibiti wa magonjwa ambayo ndio njia rahisi ya kupambana na kutokomeza magonjwa mengi katika jamii ikiwemo malaria.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hivi ninavyoandika bado nipo huku Zanzibar kikazi na huo ndio uhalisia ulivyo,hupati dawa za maralia wao wanasema walishaipiga vita ila kiuhalisia bado ipo,japo sio kali kiivyo.Niliagiza dawa bara tena zilikua za aina zote za maralia maana hali ilikua mbaya kwangu,then nilitumia kwa maelekezo tu kutoka kwa ndugu yangu mmoja daktari huko, imagine unatumia dawa bila kupima lakini dalili zote unaona ni maralia.
Kwahiyo wameadopt akili ya mwendazake na korona,maana alisema tu hakuna korona na korona ikapotea na ole wake useme mtu amefariki kwa korona,ilikuwani changamoto za upumuaji,
 
Ugonjwa wa malaria ulikuzwa sana kuliko uhalisia wa uwepo wa malaria na vimelea vyake.

Watu wengi walikufa sio kutokana na malaria bali pia madhara makubwa yaliyotokana na dawa za malaria.

Asilimia kubwa zamani kabla ya kuwepo kwa vipimo vya uhakika, matibabu ya ugonjwa wa malaria yalitegemea dalili na historia jinsi mgonjwa anavyojisikia, eneo analotoka( maeneo yenye maambukuzi) pamoja na uelewa wa mtoa tiba au huduma.

Ukiumwa na kichwa, homa, kuchoka n.k utaambiwa una malaria wewe.

Ahsante kwa teknolojia na uvumbuzi wa vitendanishi vya kupimia MRDT( malaria rapid diagnostic test) vimesaidia sana kupunguza false negative test za malaria ukilinganisha na matumizi ya microscope.

Zanzibar wanajua na walishagundua kuwa malaria ilikuwa overated.
 
Nimeishi huko kama miezi sita hivi,maralia ipo ila dawa za maralia ndio hazipatikani utazunguka pharmacy zote,hata hospital hakuna dawa za maralia ilibidi niagize kwa mtu anayetoka bara kuja Zanzibar.
Acha uongo ww, useme dawa ulizikuwa unazitaka ww ila dawa zipo tele tu.
 
Umeongea pointi ,wanachokifanya wazanzibar ni kupambana na uhalisia!!

Kuna jamaa yangu Yuko huko yeye mwenyewe amewahi niambia maneno Kama haya yako,na hii ilikuwa mwaka 2018,na nasikia hata kuriport tu kuwa una malaria ni balaa huko Zanzibar

Sasa sijui wanafanya haya ili kumfurahisha nani?
Sio kweli tena kwa taarifa yako ilikuwa uki report kesi ya malaria kwenye kitengo Chao kuna pesa ulikuwa unapewa, na timu nzima ya kitengo cha malaria wanafika mpaka eneo analoishi mgonjwa dawa ya kuua vimelea vya mbu inapulizwa.

Zanzibar wamejitahidi sana kwenye issue ya kupambana na malaria wanastahili pongezi japo malaria bado ipo na huwez lingamisha na bara ambapo watu washaizoea.
 
Hivi ninavyoandika bado nipo huku Zanzibar kikazi na huo ndio uhalisia ulivyo,hupati dawa za maralia wao wanasema walishaipiga vita ila kiuhalisia bado ipo,japo sio kali kiivyo.Niliagiza dawa bara tena zilikua za aina zote za maralia maana hali ilikua mbaya kwangu,then nilitumia kwa maelekezo tu kutoka kwa ndugu yangu mmoja daktari huko, imagine unatumia dawa bila kupima lakini dalili zote unaona ni maralia.
"Unatumia dawa bila kupima" hili ni tatizo la wengi, hairuhusiw kutoa dawa bila cheti, hukupima malaria alafu unakula dawa za malaria huoni hayo ni matumizi mabaya ya ubongo?

Ni maeneo gan Zanzibar ambapo dawa za malaria hakuna? Acheni upozoshaji usiokuwa na maana yyte, jamaa wamepiga hatua kubwa sana kuthibiti malaria wapongezwe.
 
Umeongea pointi ,wanachokifanya wazanzibar ni kupambana na uhalisia!!

Kuna jamaa yangu Yuko huko yeye mwenyewe amewahi niambia maneno Kama haya yako,na hii ilikuwa mwaka 2018,na nasikia hata kuriport tu kuwa una malaria ni balaa huko Zanzibar

Sasa sijui wanafanya haya ili kumfurahisha nani?
Ni kama tulivyosema hatuna korona halafu ikatuzoa
 
Back
Top Bottom