Zanzibar 2020 Zanzibar ya sasa inahitaji Viongozi nje ya hawa Watoto wa waliowahi kuwa Marais; akina Mwinyi, Jumbe na Karume

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,401
2,631
CCM Watu wanaowaheshimu japo kuna muda wanawakosoa wameshayachoka sasa haya Majina ya sijui akina Mwinyi, Jumbe na Karume na badala yake wanataka Kuziona Sura mpya kama si ngeni ambazo nazo zitaiongoza Zanzibar kwa Mafanikio makubwa mno na yenye Tija.

Ninawaombeni CCM Mrithi wa Dkt. Ali Mohammed Shein anayemaliza muda wake atoke kwa Mmoja wa hawa niwatajao na ninaowakubali zaidi

1. Mbarawa 51%
2. Nahodha 39%
3. Masauni 10%

Tafadhali CCM wala msipoteze muda wenu kuwajadili sijui watoto wa akina Mzee Mwinyi, Jumbe na Karume kwani hawana tena jipya Kiuongozi.
 
Kwanini hoja iangaliwe KINASABA na SI sifa zinazostahili?! Komredi wangu nadhani nayo Ina ukakasi hivi kwani tutakuhoji kwann uko EMOTIONAL SENSITIVE AND DESPERATE na watia nia ambao wana UHUSIANO na majina hayo uliyoyataja.

Ni kwanini UMMINYE MTU kwa kosa la yeye Kuwa na unasaba na viongozi waliopita?

Km mwanachama kijana nadhani tutakapoliruhusu hili basi tujue LITASHUKA chini kwa MAWAZIRI WABUNGE MADIWANI MAKATIBU,teuzi za serikali,MPAKA watendaji vijijini.

HILI NALIPINGA huku kichwani nikiwa sober kwa kutokunywa KILE KITU kiitwacho FARU JOHN "hatimiliki" ya Yule mh.mwenyekiti wa chama Cha UTOPORO!!

Assalaam alaykum,
Alamsik binnour.
 
Naona Watu mnaotoka katika hizi Familia Tatu za akina Mwinyi, Jumbe na Karume sasa mnajitokeza na huu Uzi unawachoma kweli kweli. Poleni!
 
Naona Watu mnaotoka katika hizi Familia Tatu za akina Mwinyi, Jumbe na Karume sasa mnajitokeza na huu Uzi unawachoma kweli kweli. Poleni!!!!
Kuhusiana na watu kinasaba SI dhambi...HAKUNA aombae kuwa na udugu na fulani.

DHAMBI YA UBAGUZI.
 
Zanzibar inahitaji kupata "UHURU" kutoka kwa "MKOLONI" Chama Cha Mapinduzi, bado wapo kwenye utawala wa kikoloni, kujikwamua kutoka katika mikono hatari ya CCM ndio nusura yao pekee.

Hakuna cha "Masauni" wala "Nahodha" wala Kapteni wala Substitute, au lasivyo maisha yao yatabakia kua vile vile.
Nadhani huu mtego alotegewa Jumbe, akaja Maalimu Seif na wale Magaidi basi na wewe umo. Ajenda ya kusema Bara sijui nini ni ya wazungu wanaotaka Mpemba aliyepo Mwanza afukuzwe kurudi kwao Zanzibar, Msukuma aliyepo chake chake afukuzwe arejee kwao Kishapu, Mzanzibar aliyemuoa Mnyamwezi na wanaishi Isevya Tabora basi watenganishwe na ndoa ife maana hao ni raia wa nchi mbili tofauti wanahitaji kukatiana VIZA ili kuishi Tanzania.

Kwa ufupi wazungu/waarabu wamekua wakitamani sana kuivuruga Zanzibar, na kama walitaka kufanikiwa maana watu kama wewe bado wapo. Hivyo Zanzibar inahitaji mtu anayetambua utu wetu na udugu wetu ktk Muungano (ndiyo maana Seif will never ever ever kuja kuwa rais wa Zanzibar).

Zanzibar inahitaji mtu mwenye maono ya Zanzibar ambayo mtoto wa kiume halindwi zaidi kuliko mtoto wa kike, Zanzibar ambayo dawa za kulevya ni adimu na au hazipatikani kabisa (funga drug dealers wote), Zanzibar ambayo hapa kazi tu, etc
 
Zanzibar inahitaji kupata "UHURU" kutoka kwa "MKOLONI" Chama Cha Mapinduzi, bado wapo kwenye utawala wa kikoloni, kujikwamua kutoka katika mikono hatari ya CCM ndio nusura yao pekee.

Hakuna cha "Masauni" wala "Nahodha" wala Kapteni wala Substitute, au lasivyo maisha yao yatabakia kua vile vile.
Tongotongo za Uhuru zinaathali kubwa . Hata ukipewa Zanzibar yote utaona bado hauko huru. Utaanza kutafuta uhuru wingine.

Fikra za kijima ni kuona hauko huru ndani ya nchi yako. Watu kwenye akili wanaona fulsa ndani ya muungano. Jamii inaboreka na kukua, watu sasa wanaoana , dini zinasambaa na uchumi unakua.
 
Utoto wa Rais sio sifa ya kuwa Rais lakin pia sio kigezo cha kuwanyima U Rais, zijadiliwe sifa na vigezo husika.
 
Nadhani huu mtego alotegewa Jumbe, akaja Maalimu Seif na wale Magaidi basi na wewe umo. Ajenda ya kusema Bara sijui nini ni ya wazungu wanaotaka Mpemba aliyepo Mwanza afukuzwe kurudi kwao Zanzibar, Msukuma aliyepo chake chake afukuzwe arejee kwao Kishapu, Mzanzibar aliyemuo Mnyamwezi na wanaishi Isevya Tabora basi watenganishwe na ndoa ife maana hao ni raia wa nchi mbili tofauti wanahitaji kukatiana VIZA ili kuishi Tanzania...
Nakubaliana na wewe Slave Master Sultan Seif Sharif Hamad kamwe hatakuwa raisi wa Zanzibar
 
CCM Watu wanaowaheshimu japo kuna muda wanawakosoa wameshayachoka sasa haya Majina ya sijui akina Mwinyi, Jumbe na Karume na badala yake wanataka Kuziona Sura mpya kama si ngeni ambazo nazo zitaiongoza Zanzibar kwa Mafanikio makubwa mno na yenye Tija.

Ninawaombeni CCM Mrithi wa Dkt. Ali Mohammed Shein anayemaliza muda wake atoke kwa Mmoja wa hawa niwatajao na ninaowakubali zaidi...
Zanzibar inahitaji Rais mlokole
 
Huyo wa kwanza ana nafasi kubwa hasa ukizingatia Rais wao anateuliwa na wabara. Mbarawa kama aliukwaa uongozi yaani uwaziri wa jamhuri basi huyu ndiye rais wa Zanzibar ajaye. Kama unabisha muulize Magufuri atampendekeza nani kati ya hilo lundo
 
Back
Top Bottom