Zanzibar: Waziri wa Mawasiliano aapishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar: Waziri wa Mawasiliano aapishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 25, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][/h]Posted on July 24, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,katika hafla iliyofanyika Ikulu leo

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuwaapisha Mhe.Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Hamad Masoud Hamad.

  Wakati huo huo, Dk. Shein amemuapisha Sheikh Daud Khamis Salim kuwa Kadhi wa Rufaa Pemba. Sheikh Daud aliteuliwa Mei 26 mwaka huu.

  Hafla hiyo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud.

  Wengine ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib, Washauri wa Rais, Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Issa Haji, Naibu Mufti Sheikh Mahmoud Wadi, Naibu Kadhi Sheikh Hassan Othman Ngwali pamoja na viongozi wengine.

  Dk. Shein jana tarehe 23 Julai 2012, alikubali ombi la Mhe. Hamad Masoud Hamad la kutaka kujiuzulu ili awajibike kisiasa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit iliotokea tarehe 18 Julai, 2012 ambayo ilisababisha vifo na majeruhi kadhaa.

  Kutokana nakujiuzulu huko kwa Mhe. Hamad, Dk. Shein alimteua Mhe. Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hongera zenu am sure kwa zanzibar its such a big news
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,792
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  Maalim mbona hakuwepo au alikuwa anapalilia maua ya ikulu na kutengeneza chai??
   
 4. saidyakub

  saidyakub Senior Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hongera kwa kutimiza dhana ya Uwajibikaji...Naanza kuamini kwamba ni kweli sisi tunawacheleweshea maendeleo kwa ukiritimba wetu na dhana ya kulindana tuliyokua nayo wabara
   
Loading...