Zanzibar: Waziri wa Elimu atangaza Elimu Msingi kuwa na darasa la saba kama Tanzania Bara

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Elimu ya Msingi Tanzania Zanzibar ilikuwa na utofauti na Tanzania Bara kwa kuwa walikuwa wanaishia darasa la sita kuhitimu Elimu ya Msingi

Waziri wa Elimu wa Zanzibar, Simai Mohammed Said ametangaza kuanzia 2022 Elimu ya Msingi itakuwa na darasa la Saba
===

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imefanya mabadiliko katika ngazi ya elimu ya msingi kwa kurejesha darasa la saba kuanzia mwaka 2022 kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Simai Mohammed Said amesema mabadiliko hayo ni kwa ajili ya kuimarisha elimu ya msingi kuwa ya miaka saba badala ya sita kama ilivyo sasa.

Waziri Simai amesema kufuatia tathmini zilizofanywa na Wizara pamoja na ushauri wa wadau na wazazi wa Wanafunzi kupitia mijadala mbali mbali wameona kuna haja ya kulifanyia kazi suala hilo kwani Wanafunzi wanaanza elimu ya Sekondari wakiwa na umri mdogo hali inayopelekea matokeo mabaya katika mitihani ya Kitaifa.

Akizungumzia kuhusiana na mabadiliko ya mitaala amesema Wizara ipo katika hatua za kukamilisha mtaala huo kwa ngazi ya maandalizi na msingi ambapo umezingatia mabadiliko mbali mbali ikiwemo kupunguza idadi ya masomo ambavyo yameonekana ni mengi ukilinganisha na uwezo wa watoto katika kujifunza.

Nae Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar bw Ali Khamis Juma amesema Wizara itatoa muongozo kwa Baraza la Mitihani kupinga matokeo ya Wanafunzi waliofanya mitihani ya darasa la sita kwa mwaka huu ambapo kwa waliofikiwa ufauli wa asilimia 60 ndio watakaoendelea na masomo ya kidato cha kwanza na waliopata asilimia 40 ndio watakaondelea na masomo ya darasa la saba.

Nao baadhi ya Wanafunzi wamepongeza hatua hiyo ya Serikali kwani imeonekana Wanafunzi na wazazi walio wengi walikuwa wakitoa malalamiko yao juu ya watoto wao kupeleka Sekondari wakiwa na umri mdogo ambao bado hawajatambua thamani ya elimu yao

IMG_20211224_153948_162.jpg
 
hawa watu hawajui hata wanachokifanya, maamuzi waliyoyachukua mwanzo yalikua ni sahihi kabisa. ILa baada ya mambo kutokwenda walivyopanga na yoyte ni kwa sababu waliokosa muongozo mzuri wameamua kabadili gia angani.

CCM ni laana kwenye hili taifa.
 
Mmh ndio maan hawa watu Ni wepes sana. Kwenye maswla ya kitaluma wengi wanapenda kufany biashara haswa wapemba wako wengi kariakoo kuuza maspare na vikorokoro vingi ...
 
Kama zamani mtoto anakwenda kujifunza kusoma na kuandika darasa la kwanza na la pili ambapo kwa sasa shule nyingi zinachukua mwanafunzi wa darasa la kwanza ambae anajua kusoma na kuandika kutoka chekechea kuna haja gani ya kuwa na Madarasa Saba yangebaki sita tu ila wangeboresha mfumo wa elimu
 
Kwa nini wasipunguze hayo masomo mengi ila miaka 6 ya shule ya msingi ibaki pale.
Mbona mimi nina mtoto ana miaka 12 na yupo form three na bado anakiwasha vizuri kabisa.
 
Waafrika tunadhidi kuthibitisha low IQ. Wakati mjapani anaitafuta master akiwa na miaka 19 sisi ndio kwanza tunarudusha idadi ya madarasa ili wanafunzi wahenyeke mashuleni mpaka wakome.
Cha msingi tusiopenda huu mfumo wa madarasa mengi tuwaanzishe watoto wetu shule wakiwa na miaka 4, it works! i have tested it japo walimu wakuu wanakuwa wabishi kupokea watoto wa miaka 4 utafikiri mtoto ni wake.
Mtaala wa Tanzania ni Spiral mambo yanajirudia rudia yale yale.
Sekondari unarudia yale ya msingi.
Chuo kikuu mwaka wa1 Kuna mada za sekondari 6o%.
Pamoja na kuwa na mtaala huu unaodhaniwa ni bora na walioutunga hakuna uvumbuzi, innovation, au uanzishaji wa kampuni kutoka kwa wahitimu wa huu mtaala.
Tumebaki kupaka rangi mtaala na kuzalisha watu wa kawaida ambao hata kulikuwa hakuna haja ya kukaa many years at school.
Nadhani mtaska wetu ni kwa ajili ya watoto wakaongezeje umri shuleni ili waende kuwa bodaboda na vibarua wazuri.
 
Kwa nini wasipunguze hayo masomo mengi ila miaka 6 ya shule ya msingi ibaki pale.
Mbona mimi nina mtoto ana miaka 12 na yupo form three na bado anakiwasha vizuri kabisa.
Mi nimemuanzisha mtoto drs 1 akiwa na miaka 4 na anaendelea vizuri tu, ansutsmbuzi,anajya kusoma,anaweza kujihudumia, kujieleza nk.
Mwafrika kakariri mfumo alioupokea kwa mzungu hivyo kuubadirisha anaona kama anakosea.
 
Mmh ndio maan hawa watu Ni wepes sana. Kwenye maswla ya kitaluma wengi wanapenda kufany biashara haswa wapemba wako wengi kariakoo kuuza maspare na vikorokoro vingi ...
Kwenye biashara wanafanikiwa?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom