Zanzibar: Waziri Jafo aridhishwa miradi ya Muungano

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
ZANZIBAR :- WAZIRI JAFO ARIDHISHWA MIRADI YA MUUNGANO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amefanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi inayotekelezwa pande mbili za Muungano visiwani Zanzibar na kuonesha kuridhishwa na utekelezaji wake.

Akiwa ameambatana na Naibu Waziri wake Mhe. Hamad Hassan Chande alikagua miradi mitano katika mikoa mbalimbali ya Unguja Zanzibar ambapo alisema utekelezaji wa miradi hiyo ni matunda ya Muungano ambao sote tunajivunia.

Alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo huku akisisitiza kuwa imejipanga kuondoa changamoto 10 za Muungano zilizosalia.

Aidha, aliwataka wasimamizi wa miradi kusimamia kwa umakini fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Muungano ili zilete matokeo mazuri.

“Binafsi nimefarijika sana kutembelea miradi hii na kukuta inatekelezwa kwa ufanisi lakini niwasihi muhakikishe gharama zinazotumika zinawiana na ubora wa miradi hii. Naagiza Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) msimamie majengo haya kwa ukaribu mkizangatie thamani ya fedha,” alisema.

Hata hivyo Waziri Jafo alielekeza uongozi kukamilisha jengo la huduma ya mama na mtoto lililoanza kujengwa na kuachwa kwa kipindi kirefu bila kumalizika pembeni ya kituo cha afya cha Kianga katika Wilaya ya Magharbi Mkoa wa Mjini Magharibi kujengwa upya kwa kutumia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na kukamilika kufikia Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali anayeshughulia Muungano Zanzibar Khalid Bakar Hamran aliwataka wananchi waibue miradi ambayo wana changamoto ili waweze kutatuliwa.

Alisema fedha za TASAF zimeongezeaka kutoka sh. bilioni 12 za awali hadi 21.2 ambazo zitawawezesha kuendelea kutekeleza miradi ya TASAF katika sekta za afya, elimu na maji.

Hamran aliahidi kuwa mradi huo utaendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na kumbi za kufanyia mitihani katika skuli za sekondari na ofisi za walimu.

Aliahidi kutekeleza agizo la Waziri Jafo la kuchukua hatua ya kutekeleza maelekezo ya Waziri Jafo.
 
Back
Top Bottom