Zanzibar: Wawakilishi nao posho, mishahara juu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar: Wawakilishi nao posho, mishahara juu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by 2mbaku, Dec 25, 2011.

 1. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakati sakata la kuongezwa posho za wabunge likiwa bado linafukuta Tanzania bara, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) wameongezewa posho na mshahara na kuanza kupokea kwa mwezi Sh. Milioni 4.3 kuanzia Oktoba mwaka huu. imefahamika.

  Kabla ya marekebisho yalioanza kutekelezwa mwezi Oktoba Wawakilishi walikuwa wakipata mashahara na posho mbali mbali jumla ya Sh Milioni 3.3 kwa mwezi. Kiwango cha chini cha mshahara Zanzibar kwa mfanyakazi wa Serikali ni 125,000 kwa mwezi.

  Ongezeko hilo la Shilingi Milioni moja la mshahara na posho mbalimbali limekuja siku chache baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongeza posho za wabunge kutoka Sh. 70,000 kwa siku hadi 200,000 na kusababisha manungÂ’uniko makali kutoka kwa jamii.

  Julai mwaka huu wajumbe hao wa Baraza la Wawakilkishi walitishia kugoma kuchangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi wakitaka serikali kuzingatia marekebisho ya maslahi yao. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed, alithibbitisha ongezeko la mishahara ya Wawakilishi kwa asilimia 200.

  Alisema ongezeko hilo litasaidia Wawakilishi kumudu gharama za maisha zilizoogezeka na kuwatia motisha kufanyakazi kwa bidii chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

  Alisema marekebisho hayo yamekwenda sambamba na marekebisho ya wafanyakazi wote katika sekta ya umma Zanzibar kwa madhumuni ya kusadia kumudu maisha yao.

  Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC), Mohammed Mwinyi Khamis alisema kiwango hicho cha nyongeza ni kikubwa ikilinganishwa na kima cha chini cha mfanyakzi wa kawaida.

  Mwinyi alisema kwamba katika tathmini yao walipendekeza watumishi wa umma walipwe mshahara wa kima cha chini Sh 234,000 na wafanyakzi katika sekta binafsi walipendekeza Sh 174,000 kwa mwezi.

  Hata hivyo, alisema wafanyakazi katika sekta binafsi wameendelea kulipwa kima cha chini Sh 70,000 na watumishi wa umma 125,000 licha ya kupanda kwa gharama za maisha kuazia Januari mwaka huu.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Bora hawa wana akili kidogo!
   
 3. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yaheeee,bora yenu nyie ati mwapandisha kwa wafanyakazi wote huku bara yaheeee ugumu wa maisha uko kwa wabunge tu.
   
 4. j

  janejean Member

  #4
  Dec 25, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  muungano huu ni sawa na "ndoa ya utotoni" mie hata sielewi!
   
 5. c

  chama JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Posho ni wimbo unaokubalika na CCM nafsi za wabunge wetu zimeshatekwa na pesa; hoja zinazokubalika ni za kutetea maslahi yao

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
Loading...