Zanzibar: Watu Watano wafariki, 12 wamelazwa baada ya kula Samaki aina ya Kasa

Watu wawili wamefariki na wengine 11 kujeruhiwa Kisiwani Pemba baada ya kula samaki anaesemekana kuwa na sumu Katika Shehia ya Msuka Mgharibi Kijiji cha Taponi, Mkuu wa Wilaya anaeleza kila kitu
View attachment 2024740

====

UPDATES: 28 NOV 2021

====

Tarehe 25 Novemba 2021 huko Pemba, Watu 25 wa familia tano walikula samaki aina ya Kasa ambaye kasababisha Vifo na Majeruhi.

Kamanda wa Polisi Kaskazini Pemba, ACP Juma Khamis ameiambia JamiiForums kwamba Watu Watano Wamefariki baada ya kula samaki aina ya Kasa. Kati ya Waliokufa ni Watoto wanne wa kuanzia Mwaka mmoja hadi 11 na Mtu mzima mmoja wa miaka 70 mwanamke.

ACP Juma kasema Watu 12 bado Wamelazwa na Watatu kati yao hali zao sio nzuri.

Kamanda amesema Serikali ya Zanzibar ilishapiga Marufuku ulaji wa Samaki aina ya Kasa na Bunju, kutokana na kuwa na Sumu, lakini bado watu wanawavua na kuwatoa baadhi ya viungo vyenye sumu kisha wanakula. Katoa wito watu kuepuka ulaji wa samaki aina ya Kasa na Bunju.
Kasa siyo samaki,ni Kobe wa baharini
 
Naombeni maana ya neno kujeruhiwa
Nahis limetumika ndivyo sivyo hapo juu

Yan ule kitu upate jeraha??🤔
Uko sahihi neno hilo halikupaswa kutumika hapo. Nadhani editing haikuzingatia usahihi wa matumizi ya maneno kwa kuyalinganisha ili kuleta maana sahihi
 
Back
Top Bottom