figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,888
Watoto wanne wenye Umri wa Miaka kati ya Miwili na Mitatu wa Familia tofauti Mjini Unguja, wamefariki dunia baada ya kushindwa kutoka nje ya gari walilokuwemo kutokana na milango ya gari hiyo kujifunga hali iliyosababisha kukosa hewa.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Ali Nasser amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika eneo la Kidongo Chekundu.
======
Watoto wanne wamefariki dunia baada ya kujifungia kwenye gari kwa muda mrefu huko katika maeneo ya kidongo Chekundu Mjini Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir amesema tukio hilo lilitokea hapo jana katika maeneo ya kidongo Chekundu ambapo watoto hao wamekutwa wakiwa katika Gari aina ya VITZ yenye namba za usajili Z 986 DW inayomilikiwa na Ndugu Omar ambayo ilikuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabra katika maeneo ya kidongo chekundu mjini Zanzibar.
Akiwataja watoto hao waliofariki ni Haitham Mustafa Abuubakar miaka 2 mkaazi wa Kidongo Chekundu, Muslihi Hamza Bakari Miaka 2 Jang’ombe, Dodo Muhammed miaka miwili na miezi saba mkaazi wa Jang’ombe na Munawar Ahmed khamis Jang’ombe.
Amesema vifo vya watoto hao kinasababishwa na kukaa muda mrefu katika gari hiyo na kukosa hewa na kupelekea kushindwa kupumua katika kipindi chote ambacho wanatafutwa na familia zao.
Akizungumza juu ya Maiti hizo Mtaalamu wa Uchunguzi wa Hospital Mnazi mmoja Zanzibar Dk.Marijani Msafiri alifahamisha kuwa watoto hao walifariki dunia kutokana na kuwa na mazingira ya joto kali na ukosefu wa hewa aina ya oxgen wakiwa ndani ya gari hiyo.
Kwa mujibu wa Dk. Marijani tayari watoto hao wamechukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa taratibu za Mazishi.
Chanzo: Zanzibar 24