Zanzibar: Watendaji wa Serikali watakiwa kuweka pembeni ushabiki vyama vya kisiasa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,757
2,000
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui amewataka watendaji wa serikali katika sekta ya afya, kuweka pembeni itikadi za vyama na ushabiki wa kisiasa na malengo yawe kuwatumikia wananchi.

Mazrui alisema hayo wakati akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa kaimu wa wizara hiyo, Simai Mohamed Said, makao makuu ya wizara Mnazi Mmoja mjini hapa.

Alisema ushabiki wa vyama vya siasa, hauna nafasi katika ofisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa wizara hiyo, ambayo ni miongoni mwa taasisi zinazowagusa wananchi moja kwa moja.

''Sitaki ushabiki wa vyama vya siasa katika sehemu za kazi…mapenzi yenu yaacheni Kisiwandui na Vuga katika ofisi za chama cha ACT-Wazalendo, hapa tunataka kazi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi''alisema.

Alisema katika kipindi kifupi, anatarajia kukutana na watendaji wa sekta mbalimbali za afya kwa ajili ya kufahamu changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuleta ufanisi.

''Nimeteuliwa juzi lakini katika kipindi kifupi nitaonana na watendaji mbalimbali kujua changamoto za kazi kwa lengo la kuleta ufanisi''alisema.

Mapema, aliyekuwa Kaimu wa wizara hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu, Simai Mohamed Said aliwataka watendaji wa wizara hiyo na vitengo mbalimbali, kufanya kazi na Mazrui ili kukidhi malengo na matarajio ya Rais Dk. Mwinyi kutoa huduma kwa wananchi.

''Sekta ya afya ndiyo tegemeo na kimbilio la wanyonge, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejizatiti kutoa huduma za afya bure kwa wananchi wake....nawaomba watendaji wote muelekeze nguvu zenu kwa waziri Mazrui na mmpe ushirikiano wa dhati''alisema.

Chanzo: Habari Leo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom