Zanzibar 2020 Zanzibar wapiga kura ya mapema. Makundi yanayoshiriki ni Watumishi wa ZEC na Vyombo vya Ulinzi na Usalama (Oktoba 27, 2020)

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wazanzibari leo wanapiga kura ya mapema ambapo makundi maalum wakiwemo Watumishi wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) na Wasimamizi wa Uchaguzi watashiriki katika zoezi hilo.

Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Hamid Mahmoud Hamid amesema wanaopiga kura leo watatumia Vituo ambavyo wamejiandikisha, kura zao zitahifadhiwa na kulindwa ili kujumlishwa na kura zitakazopigwa kesho.

Aidha, amesema Vyombo vya Ulinzi pia vitapata nafasi ya kupiga kura leo huku akisisitiza sio Askari wote watakaoshiriki bali ni wale watakaohusika kusimamia shughuli za Uchaguzi.

======

UPDATES: 28-10-2020

DKT. HUSSEIN MWINYI APIGA KURA, AHIMIZA WAZANZIBARI KUENDELEA KUJITOKEZA


Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dkt. Hussein Mwinyi amepiga kura Mjini Unguja ambapo ametoa rai kwa Wazanzibari kuendelea kujitokeza Vituoni kwa ajili ya kupiga kura

Vilevile, Mgombea Mwenza wa Urais JMT, Samia Suluhu Hassan naye amepiga kura Zanzibar na kuwataka walio na wasiwasi kujitokeza kupiga kura akisema hali ipo vizuri
 
Kura ya mapema ukiitafakari vema ni Wizi mtupu. Eti makundi maalum yakapige kura ya wawakilishi na Raisi wa Zanzibar Leo, kisha kesho yarudi tena yakapige za nafasi za Muungano!

Kwani hiyo kesho kungekuwa na uzito kwa makundi hayo kupiga kura zotr mbili mapema?

Jiulize pia, udhibiti wa kura za Leo ikiwa ni pamoja na kuwatambua hao wanaoenda kupiga hiyo kura, ukoje?

Huu ni mchezo wa kwanza kwenda kuharibu huu Uchaguzi.
 
Hizo kura zinapotea wangepiga zingeongeza idadi ya kura
Hadi Sasa mnahaha hamjapata tallying center za upinzani pamoja na kutapatapa mara mumkamate Mazrui, Mdee, Heche, Esta Matiko, lema mmeambulia patupu, hakuna kura mtakayoiba this time hata msaidiwe na wachina, mkichezea tu mifumo kila kitu kitaonekana.

Kuulinda udhalimu udikteta ni gharama kubwa Sana
 
Thus wenzetu hutushangaa Sana hivi uchaguzi hauwezekani bila kumwagwa damu, kwanini vyombo vya ulinzi kuingilia ugomvi wa wanasiasa.

Vinazidiwa hata na vya Malawi kule vinalinda nchi na sio chama
 
Kuna mchezo mchafu unaendelea katika huu Uchaguzi, inakuaje Zanzibar ina watu kiduchu wapige kura siku mbili?
 
Wizi mtupu wa Kura! kweni Tanganyika hakuna Watumishi wa NEC mbona hatupigi mara mbili
ActWazalendo na Chadema Zanzibar kama kupiga wote tunapiga Leo Leo kama ni kesho wote kesho

Ukoloni sasa baasi!

Kura zinapigwa mara mbili kuwapa vyombo vya ulinzi na usalama nafasi ya kuhudumu vizuri siku ya kesho, sasa mnapo vuruga na siku ya leo mnaendelea kuthibitisha kuwa mnapenda vurugu na walioweka siku mbili tofauti walikuwa sahihi kabisa
 
Huo uchaguzi umeshavurugwa na ZEC yaani wapiga kura laki 5 wanapiga siku mbili halafu wapiga kura milion 29 wanapiga siku moja. Hata aibu ya binadamu hawana kabisa hao.

Yote ni kutaka kuingiza nchi kwenye machafuko bila sababu. Sasa wanachokitafuta hao ZEC watakipata
 
Usionje sumu kwa ulimi
Unajua Zanzibar kuna baadhi huwa hawasikii mpaka wapewe dawa

Atakaye vunja sheria na taratibu ashughulikiwe vilivyo na mamlaka zote zinazo husika

Mfano:
1. Vyombo vya ulinzi na usalama kutumia nguvu kwa wavunja amania na usalama.

2. Mahakama kuhukumu wavunja amani na usalama.

3. Tume ya Uchaguzi & Ofisi ya msajili kukiondoa kwenye uchaguzi ama kushiriki siasa chama, mgombea, mwanachama aliyeshiriki kwenye kuvunja amani, taratibu na sheria.

Bila hatua kali basi vituko, makusudi, uvunjifu wa sheria na taratibu unaofanywa na baadhi ya watu Zanzibar hautakoma ova!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom