zanzibar wanaume!!!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
nnaomba hii ibakie ili tuweze kuchangia.

hawa wanaume wa shoka chini ya kocha wao mzalendo abdul gahni msoma wanaozikosha nyoyo za watanzania na kufanya kweli. nnasikia wametandaza ball la kutisha huko arusha.

hata hivyo kwa nn timu yetu ya taifa inajaa wachezaji upand mmoja wakati tukija kwenye mashindano ya kitaifa yanayotushirikisha sote hawa wenzetu tunawatoa mafua.

pili kwa nn hapa habari za klimanjaro ziapokelewa bomba na hizi za zanzibar mnaziwekea mguu na hali zote zinawakilisha zanzibar?

na kama huamini mamod si muda wataiondosha hali ingekuwa kili ingekaa sana hapa

Zanzibar yatinga robo fainali kwa kishindo

* Jibuti kama 'Call Box', yapigwa 9-0 Dar

Na Glory Mhiliwa, Arusha

TIMU ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' jana ilitinga robo fainali ya michuano ya Chalenji kituo cha Arusha baada ya kuifunga Ethiopia mabao 3-1, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Zanzibar ikicheza soka la uhakika iliwadhibiti vilivyo mabingwa watetezi kivuli hao wa michuano ya Chalenji.

Tofauti na mchezo wa kwanza ambao ilitoka sare ya mabao 2-2 na Sudani, jana Zanzibar iliwachukua dakika tatu kupata bao lililofungwa na Abdallah Juma kwa shuti.

Waethiopia walisawazisha dakika ya 32 mfungaji akiwa Behaile Demeke kwa kona iliyomshinda kipa Farouk Ramadhan.

Zanzibar ilipata bao la pili dakika ya 64 mfungaji akiwa Abdi Kassim, baada ya kupata pasi ya Hamis Mcha, kabla ya kupachika la tatu dakika ya 75 mfungaji akiwa Ali Mkweche.

Kutokana na ushindi huo Zanzibar Heroes imetinga robo fainali ikiwa na pointi nne na mabao matano ya kufunga, ambapo kwa sasa inaongoza Kundi C, ikiwa imemaliza michezo yake miwili.

Ethiopia na Sudani zinaumana kesho katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo, ambapo Sudani itakuwa ikihitaji sare ili iungane na Zanzibar, kwani timu hiyo ina pointi moja baada ya kutoka 2-2 na Zanzibar katika mchezo wa kwanza, wakati Ethiopia italazimika kushinda, matokeo ambayo hayawezi kuiathiri Zanzibar Heroes.

Naye Erasto Stanslaus anaripoti kuwa timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' jana iliifunga Jibuti mabao 9-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Jibuti ambayo mechi ya kwanza ilifungwa na Uganda mabao 7-0, jana hadi mapumziko ilikuwa tayari imebugizwa mabao 4.

Mabao ya Rwanda yalifungwa na Oliver Karekezi dakika ya 18, ambapo bao la pili beki wa Jibuti Faysal Abdi alijifunga dakika ya 22 katika harakati za kuokoa. Bao la tatu lilifungwa dakika ya 38 na la nne dakika ya 43 yote mfungaji akiwa Kamana Bogota.

Bao la tano liliwekwa kimiani na Roger Tuyisenge dakika ya 47, wakati la sita lilifungwa na Elius Uzamukunda dakika ya 54 na la saba lilipachikwa na Ngoma Herman dakika ya 62.

Katika mchezo huo Jibuti walizidiwa kwa kiasi kikubwa, ambapo hawakufanya mashambulizi ya nguvu na kujikuta wakichezewa nusu uwanja katika kipindi cha pili.

Mabao mengine ya Rwanda yalifungwa na Ndoli Jean dakika ya 77, wakati la tisa lilifungwa dakika ya 84 na Karekezi.

Kwa matokeo hayo Rwanda imetinga robo fainali ikiwa na pointi sita kama Uganda ambayo pia imeshafuzu, lakini timu hizo zinatofauatiana mabao ya kufunga na kufungwa. Rwanda imeshamaliza michezo yake, wakati Uganda leo inacheza na Eritrea kukamilisha ratiba.

Tayari Kundi hilo B timu zake zilizofuzu zimejulikana ambazo ni Rwanda, Uganda na Eritrea. Timu tatu kutoka Kundi A na tatu kutoka Kundi B zinafuzu robo fainali pamoja na mbili kutoka Kundi C.

souce majira
 
mtu wa pwani........

maximo alipotembelea zenji last time,alisema hajaona vipaji vyovyote huko znz ameona vijana wengi kazi yao kula MBATATA ZA UROJO na KUCHEZA ZENJI FLAVOUR.

HONGERA SANA TIMU YETU YA MAPINDUZI STARS.
 
basi atajua kama tunakula mbatata za rojo au boko boko.

ajue ss si mbatata tu hata shurba twala.

na hao wenzetu tunawangoja tuwafundishe mpira kule mpira ni vipaji sio kulazimisha.

mnazi mmoja ndio mazalio yetu tukea miaka mitano hadi hivyo mwamme
 
Mtu wa pwani hawa jamaa wanatubinyia kimataifa na sisi ikija CHALLENGE tunamkoma nyani kweupeee.
 
tunataka kutoa ujumbe mzito mwaka huu.

halafu waendelee kun'ga'ngana population density ooh nyny kidogo kwa hio ratio yenu mchezaji mmoja.

hawa walalamishi lkn hiki kigezo tosha kuwa tukiachwa peke yetu hawa wenzetu tutawafunika kwenye anga nyingi tu
 
Back
Top Bottom