Zanzibar wanapunguza gharama za kuunganisha umeme, Tanzania bara tunaongeza

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Jana rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza mapinduzi akihutubia mwananchi wa Zanzibar katika kuhitimisha maadhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar alitoha hotuba nzuri sana. Aligusia mambo mengi sana yaliyofanyika na wanayo tarajia kufanya siku za usoni.

Wameweka kipaumbele kwenye kuzalisha umeme wa Megawatts 18 kwa nguvu za jua. Lakini amesema watapunguza gharama za kuunganisha umeme kutoka laki sita(600,000) mpaka laki mbili(200,000) ili kuwapa uwezo mwananchi wake waweze kuunga umeme ambao ni muhimu sana kwa mwananchi wa Zanzibar.

Lakini cha kushangaza bara wameongeza gharama za kuunganisha umeme wakati wote ni Watanzania. Kuna haja CCM bara na CCM Zanzibar kuwa na malengo ya kufanana kwa baadhi ya mambo hususani huduma za kijamii.

Zanzibar umeme wao wanachukua Tanzania bara japokuwa wana shirika lao la umeme la ZECO lakini cha kushangaza wao wanapunguza gharama sisi tunaongeza gharama
 
Laki mbili si elfu ishirini na saba. Hivyo wewe unaamini Tsh 27000 zinatosha kukuletea umeme ndani bila Tanesco kufidia gharama zinazozidi. Tanesco imefilisiwa kwa wizi na maamuzi mabovu ya kisiasa. Tanesco lazima iendeshwe kibiashara - angalau wasipate hasara za kujipangia.
Wabinafsishe shirika uone mwananchi atakavyo bembelezwa kuwekewa umeme! Na gharama yake itakuwa kulipia umeme alio utumia tu!
 
Laki mbili si elfu ishirini na saba. Hivyo wewe unaamini Tsh 27000 zinatosha kukuletea umeme ndani bila Tanesco kufidia gharama zinazozidi. Tanesco imefilisiwa kwa wizi na maamuzi mabovu ya kisiasa. Tanesco lazima iendeshwe kibiashara - angalau wasipate hasara za kujipangia.
Yaani Mita ile, waya mkubwa wa 10mm umbali wa mita labda 20, ndo iwe 27000/= ni ajabu!

Waya wa 4mm huku mtaani ilikuwa 4500 bei ya 2018 sasa hivi nasikia vitu vya umeme vimepanda, kwa umbali huo wa 20 meter, maana yake ni 4500 ×20=90,000 sasa sijui waya wa 10mm unauzwa shilingi ngapi, bado nguzo yaani ulitoe gogo la nguzo kule Mafinga, tena iwe treated, mfano hiyo nguzo uisafirishe hadi Mwanza, then gharama ya mafundi, maana yote hiyo inaingizwa kwenye total cost...utakuja kuona hata hiyo 321,000/= wanayo charge sasa ni sawa na bei chee ya promotion....wenye akili mpo?

Mnaopenda mteremko mpo?
 
Wametoa wapi umeme mkubwa hivyo? yaani megawat 18 kwa jua? TANESCO shitukeni.
Safari ya singapori imeanza kwa guu la kulia. 18 mw ni zaidi ya nusu ya hitaji la umeme Zanzibar. Yajayo yana furahisha.
 
Laki mbili si elfu ishirini na saba. Hivyo wewe unaamini Tsh 27000 zinatosha kukuletea umeme ndani bila Tanesco kufidia gharama zinazozidi. Tanesco imefilisiwa kwa wizi na maamuzi mabovu ya kisiasa. Tanesco lazima iendeshwe kibiashara - angalau wasipate hasara za kujipangia.
Wanafidia au wanakata kwenye REA na EWURA.
 
Tunaanza kulialia kwamba Wakoloni wa Kizanzibari wanatutesa😁
 
Yaani Mita ile, waya mkubwa wa 10mm umbali wa mita labda 20, ndo iwe 27000/= ni ajabu!!!!!
Waya wa 4mm huku mtaani ilikuwa 4500 bei ya 2018 sasa hivi nasikia vitu vya umeme vimepanda, kwa umbali huo wa 20 meter, maana yake ni 4500 ×20=90,000 sasa sijui waya wa 10mm unauzwa shilingi ngapi, bado nguzo yaani ulitoe gogo la nguzo kule Mafinga, tena iwe treated, mfano hiyo nguzo uisafirishe hadi Mwanza, then gharama ya mafundi, maana yote hiyo inaingizwa kwenye total cost...utakuja kuona hata hiyo 321,000/= wanayo charge sasa ni sawa na bei chee ya promotion....wenue akili mpo?
Manaopenda mteremko mpo?
Huwa waya na vifaa ni mali ya nani?
Acha uzwazwa REA na EWURA wanakata pesa kupeleka wapi?
Huo sio mteremko ni kodi zetu.
 
Yaani Mita ile, waya mkubwa wa 10mm umbali wa mita labda 20, ndo iwe 27000/= ni ajabu!!!!!
Waya wa 4mm huku mtaani ilikuwa 4500 bei ya 2018 sasa hivi nasikia vitu vya umeme vimepanda, kwa umbali huo wa 20 meter, maana yake ni 4500 ×20=90,000 sasa sijui waya wa 10mm unauzwa shilingi ngapi, bado nguzo yaani ulitoe gogo la nguzo kule Mafinga, tena iwe treated, mfano hiyo nguzo uisafirishe hadi Mwanza, then gharama ya mafundi, maana yote hiyo inaingizwa kwenye total cost...utakuja kuona hata hiyo 321,000/= wanayo charge sasa ni sawa na bei chee ya promotion....wenue akili mpo?
Manaopenda mteremko mpo?
Sijui kama huyu raia anajua kama huwa anakatwa pesa ya REA kila anunuapo umeme?
Na kama anajua huwa anakatwa, nadhani huwa anafikiri inakwenda kununulia vitumbua watumishi wa Tanesco.
 
Huwa waya na vifaa ni mali ya nan?
Acha uzwazwa REA na EWURA wanakata pesa kupeleka wap?
Huo sio mteremko ni kodi zetu.
Nani amekuambia ni kodi zetu? Rea ni udhamini wa nje na hii toka enzi za Kikwete, kodi yako ifanye mambo mangapi, kulipa walimu, wabunge, madaktari, polisi, wanajeshi, iendeshe miundombinu ya nchi, watu walilishwa matangopoli sana, kipindi cha utawala uliopita na nakuambia sio kwamba walikua hawakopi iaipokuwa waropokaji walitulia maana ukiropoka tu imekula kwako
 
Mpango ule na bei zile ulikuwa na kurahisisha umeme vijijini. Sasa wamerudisha bei na kuturudisha nyuma.
 
Yaani Mita ile, waya mkubwa wa 10mm umbali wa mita labda 20, ndo iwe 27000/= ni ajabu!!!!!
Waya wa 4mm huku mtaani ilikuwa 4500 bei ya 2018 sasa hivi nasikia vitu vya umeme vimepanda, kwa umbali huo wa 20 meter, maana yake ni 4500 ×20=90,000 sasa sijui waya wa 10mm unauzwa shilingi ngapi, bado nguzo yaani ulitoe gogo la nguzo kule Mafinga, tena iwe treated, mfano hiyo nguzo uisafirishe hadi Mwanza, then gharama ya mafundi, maana yote hiyo inaingizwa kwenye total cost...utakuja kuona hata hiyo 321,000/= wanayo charge sasa ni sawa na bei chee ya promotion....wenue akili mpo?
Manaopenda mteremko mpo?
Mkuu, baada ya hapo umeme unatumia bure?
 
Baada ya kulipia yote hayo katika hiyo 391,000 hizo nguzo na waya zinakuwa mali ya nani? Inakuwa mali ya aliyetoa hela kuunganisha au ya Tanesco
 
Nani amekuambia ni kodi zetu? Rea ni udhamini wa nje na hii toka enzi za kikwete,kodi yako ifanye mambo mangapi, kulipa walimu ,wabunge,madaktari, polic,wanajeshi , iyendeshe miuondo mbinu ya nchi, watu walilishwa matngo poli sana, kipindi cha utawala uliopita na nakuambia sio kwamba walikua hawakopi iaipokuwa waropokaji walitulia maana ukiropoka tu imekula kwako
Kwaiyo kila unaponunua umeme na mafuta makato ya REA ndio ufadhili?
Huyo aliyekopa alillipa til. 50 na hakukopa akalipe deni.
Tuambie makato ya REA yanafanya kazi gani.
Akili ndogo ni mtaji wa CCM.
 
total cost...utakuja kuona hata hiyo 321,000/= wanayo charge sasa ni sawa na bei chee ya promotion....wenue akili mpo?
Ni non profit cooperation! Hatuangalii faida. Ndiyo maana kuna tozo, kodi na vingine kama hivyo kukidhi hitaji hili.
 
Jana rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza mapinduzi akihutubia mwananchi wa Zanzibar katika kuhitimisha maidhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar alitoha hotuba nzuri sana.
Aligusia mambo mengi sana yaliyofanyika na wanayo tarajia kufanya siku za usoni.

Wameweka kipaumbele kwenye kuzalisha umeme wa Megawatts 18 kwa nguvu za jua.
Lakini amesema watapunguza gharama za kuunganisha umeme kutoka laki sita 600000 mpaka laki mbili 200000 ili kuwapa uwezo mwananchi wake waweze kuunga umeme ambao ni muhimu sana kwa mwananchi wa Zanzibar.

Lakini cha kushangaza bara wameongeza gharama za kuunganisha umeme wakati wote ni Watanzania.
Kuna haja CCM bara na CCM Zanzibar kuwa na malengo ya kufanana kwa baadhi ya mambo hususani huduma za kijamii.
Zanzibar umeme wao wanachukua Tanzania bara japokuwa wana shirika lao la umeme la ZECO lakini cha kushangaza wao wanapunguza gharama sisi tunaongeza gharama
Labda TANESCO ya bara na Zanzibar wamekubaliana hivyo.
 
Back
Top Bottom