Zanzibar: Wanaokula hadharani, kuvaa nguo fupi kukiona | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar: Wanaokula hadharani, kuvaa nguo fupi kukiona

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pepombili, Aug 17, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imelitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaokula hadharani na kuvaa nguofupi wakati huu wa mfungo mtukufu wa Ramadhani.

  Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alipozungumza na waandishi wa habari jana.

  Alisema serikali imeamua kutoa agizo hilo baada ya kujitokeza baadhi ya watu kuonekana wakila mchana hadharani na baadhi ya vijana kuonekana wakiwa wamelewa na kuranda mitaani kinyume na misingi ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

  Aidha, alisema baadhi ya wanawake wamekuwa wakionekana mitaani wakiwa wamevaa nguo zisizokuwa na heshima.

  Waziri Aboud amesema kwamba baadhi ya migahawa na nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitoa huduma mchana katika kipindi cha Mwezi Mtukufu. Waziri Aboud alisema kimsingi wananchi hawazuiwi kula mchana kulingana na imani zao, lakini wanatakiwa kufanya hivyo wakiwa katika maeneo ya faragha kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

  "Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawataka wale wote wanaojishirikisha na vitendo hivyo waache mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria pamoja na kwenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na mafundisho yake Mtume Mohammad," alisema.

  Aidha, alisema serikali inatarajia wananchi wote Unguja na Pemba watashirikiana kurudisha heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

  Waziri Aboud amesema serikali imeamua kutoa tamko hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka Jumuiya moja ya kidini Zanzibar juu ya kuwepo watu wanaokula mchana na kuvaa nguo fupi bila kuzingatia misingi ya mfungo wa Mwezi wa Ramadhani.

  Kweli muheshimiwa umesema kweli na mimi nakuunga mkono kwa asilimia 100% lakini mbona mpaka leo tunawaona watalii hasa wazungu wakitembea uchi mitaani bila hata ya kubugudhiwa je hili tangazo linawahusu na wazungu wanaotembea na vichupi barabarani na kuwa vichwa wazi au sisi wenyeji tu ?
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Duh! Kaazi sana.
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Safi sana
   
 4. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Labda kwa kipindi hiki cha mfungo biashara ya utalii imesimama.... tusiwalaumu zanzbar ni nchi waache waweke sheria zao wanavyojisikia wenyewe kulingana na utamaduni wao...
   
 5. bht

  bht JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  nilidhani kufunga ni symbolic tu....
   
 6. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Natamani sana kuona watu wakichapwa bakora wakitembea uchi na hasa tukianza na watalii wanaovaa vichupi na kutembea vichwa wazi ndani ya mwezi huu mtukufu na wale wote wanaofungua vilabu vya pombe wachomewe moto big up Zanzibar Go AHEAD
   
 7. p

  pori Member

  #7
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani naomba kuuliza? Hivi kwa nini waislamu wanapofunga wanakuwa na masharti mengi sana? je wakristu wanapofunga kwaresima, waislamu huwa wanalazimishwa kula mafichoni? kama ni maadili basi yawepo wakati wote na siyo kipindi cha mfungo tu!
   
 8. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kaaazi kweli kweli
   
 9. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Haina maana yeyote . . . mtu aliyefunga kweli hata mwanamke akatize uchi hawezi hisi/ona kitu maana yeye yupo kwenye ibada, hii hawatakuwa wamefunga ibada ila wamefunga kujitesa tu..
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wafunge hotel zote basi tuone kama watapata maendeleo maana mtu anayekula hotelini hajifichi yupo hadharani au wanataka wakalie cho.oni
   
 11. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwezi wa Ramadhani una heshima maalumu ambayo ni lazima kila mtu auheshimu.
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Napita waungwana.
   
 13. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Watiizedi bana. Kaaazi kweli kweli. Hata wasiouabudu huo mwezi? Mbona bongo tuna tafuna tu any time na anywhere? Au ile ni Islamic Republic of Zanzibar? Kwahiyo miezi mingine tutembee uchi?
   
 14. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  nilie4nda Tanga ... wakati wa kufuturu ukifika biashara zimesimama.. jamaa petrol station waligoma kunijazia mafuta eti hadi wamalize kufuturu... hehehehe
   
 15. doup

  doup JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  kwa waislamu tu, na si kwa wengineo. Sisi wengine tunauona kama kaida tu, Na tunajitaidi tuwakwaze wenzetu, Au Znz ni kama Iran (Inchi ya Dini ya Kiislamu?).
   
 16. m

  mkipunguni Member

  #16
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 1, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweni hii ni nchi tofauti???? Mh huu muungano mbona una mambo mengi hovyo yaani ikitokea nimesafiri kikazi znz basi ndio nilazimishwe kufunga lol!!!!
   
 17. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Hivi ukiwa umefunga ukaona mwenzako atapiga supu kuku asubuhi asubuhi roho inakutoka na saumu inaisha? Nauliza maana i nilidhani muumini wa kweli aliyefungwa hawezi ingiwa na tamaa hata iweje. Au mnalazimishwa kufunga
   
 18. bht

  bht JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kufunga ni alama tu kwamba kadiri mtu atakavyojinyima chakula (fikiria kushinda njaa ilivo ngumu) basi aweze pia kuyashinda majaribu na tamaa zinazomwangusha dhambini.

  lazima upigane vita ndipo uvikwe taji, sasa kama unakimbia vita hautakuwa mshindi.
   
 19. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Si jaipenda kabisa hii na ikiendekezwa inaweza kuleta matatizo. Kwani Zanzibar ni waislam tu?
  Sisi ofisini kwetu mabinti wote wanatakiwa kuvaa skirt fupi juu ya paja wote ili wawe wepesi kumove.

  Hii ndio mizee mimalaya, wanaogopa totos zao zitabebwa na wenzao kipindi hiki...
  Wanafunga nini wafungue tu waendelee kufurahia uumbaji wa mungu...!
   
 20. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wasianze kupangia watu sehemu za kulia kisa wao hawali..
  Huko ni kuingilia uhuru wa mtu wa kuabudu. mie dini yangu mwezi huu hainiruhusu kabisa kula kwakifichoni maana ni uchoyo.
  Mwezi huu natakiwa kulia hadharani ili wale walioshinda njaaa wapate kula.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...