Zanzibar 2020 Zanzibar: Wananchi Walalamikia Majina yanayoenda kupiga kura ya mapema, wawakana

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Salaam Wakuu,

Huku Zanzibar mambo si Mambo. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC, ilipanga kupiga kura siku mbili yaani kundi Maalum litapiga kura tarehe 27, na Wengine tarehe 28.

Wananchi wa Zanzibar hasa Pemba, wameanza kulalamikia Majina yatakayo piga kura ya Mapema wakidai si wenyeji wa huko.

Mmoja ya Wazanzibari amenukuliwa akisema "Tukitaka kuwa wakweli wa nafsi zetu tunaoijua Zanzibar na watu wake ni wazi wasiokuwa waislamu tena kutoka Bara ni kundi maalum la kupiga kura mapema. Nasema sio kwa ubaguzi Bali kwa wanaoijua Zanzibar na watu wake wamenielewa. Tulipokuwa tunakataa hii kura sababu tunayajua haya".

Wananchi wanahofia hii kura ya tarehe 27 Oktoba, inaweza kuvuruga Uchaguzi wa Zanzibar.
20201023_124243.jpg
 
Kuna 'mapepo' huvuka bahari kutoka Bara kwenda kupiga kura Zanzibar kwenye kila auchaguzi kwa miaka mingi.

Vv
 
CCM huwa hawaeleweki wanatumia nguvu nyingi sana kupindisha haki gharama ambayo wangeitumia kufanya mambo mazuri kwa wananchi na wakawakubali
 
22 October 2020

WATAZAMAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA UCHAGUZI NA MWONGOZO WA WATAZAMAJI

Balozi Omar Ramadhani Mapuri mwakilishi wa NEC, IGP Simon Sirro, mwakilishi wa usawa wa kijinsia wazungumza

Source : NEC ONLINE TV - Tanzania
 
Hayo majina ngoja tuingie intaneti na ku google kuwajua vizuri wapiga kura hawa wametokea wapi kina Tunduu, Shika, Tarimo n.k wasipokuwepo hao watakuwa ama ni maruhani au wakulima, wavuvi n.k wasiokuwepo ktk intaneti

Pia kuhakiki taarifa za mpiga kura bofya: https://vis.nec.go.tz
Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA​

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI​

MFUMO WA KUHAKIKI TAARIFA ZA MPIGA KURA

nec-logo.png
Kuhakiki taarifa, Mpiga Kura anatakiwa kuwa na Namba ya Mpiga Kura ambayo ipo kwenye Kadi ya Mpiga Kura.
Kuhakiki taarifa weka namba ya mpiga kura (kama ilivyoandikwa kwenye kadi yako ya Mpiga Kura, Mfano : T-XXXX-XXXX-XXX-X) kwenye kisanduku hapo chini kisha bonyesha kitufe cha Tafuta

Namba ya Mpiga Kura*
Source : https://vis.nec.go.tz
 
Tizama mtu wa Tanganyika au TZ bara ukiwa Znz umejiandikisha kupiga kura unaruhusiwa kupiga kura kumchagua rais wa jamhuri ya muungano tu, hawa wenye majina ya kafiri kama mnavyowaita ni askari kwa hiyo watapiga kura moja tu ya kumchagua rais wa Jamhuri ya Tanzania, sasa tatizo lipo wapi?
 
Kama wana kazi maalum si waainishe na shughuli zao au wanapofanyia kazi? Kuweka Tu majina hivyo si ndo ubabaishaji huo??
 
Yani hapa ni kuwa wameandaa watu kama 50,000 wanatoka bara wanaebda kupiga kura zanzibar. Baada ya hapo wanarudishwa ili kesho yake wapige kura bara.
 
Wazanzibar msikubali wanataka kuiba kura yaani wapiga kura wasiozidi laki sita kura zipigwe siku mbili? Wakati bara wapiga kura milioni ishirini na nane kura zinapigwa siku moja ? Inaingia akilini ?
IMG_20201022_105629.jpg
IMG_20201023_124941.jpg
IMG_20201023_124952.jpg
IMG_20201023_124957.jpg
IMG_20201010_141201.jpg
IMG_20201010_141146.jpg
Screenshot_20201010-141123.png
 
Salaam Wakuu,

Huku Zanzibar mambo si Mambo. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC, ilipanga kupiga kura siku mbili yaani kundi Maalum litapiga kura tarehe 27, na Wengine tarehe 28.

Wananchi wa Zanzibar hasa Pemba, wameanza kulalamikia Majina yatakayo piga kura ya Mapema wakidai si wenyeji wa huko.

Mmoja ya Wazanzibari amenukuliwa akisema "Tukitaka kuwa wakweli wa nafsi zetu tunaoijua Zanzibar na watu wake ni wazi wasiokuwa waislamu tena kutoka Bara ni kundi maalum la kupiga kura mapema. Nasema sio kwa ubaguzi Bali kwa wanaoijua Zanzibar na watu wake wamenielewa. Tulipokuwa tunakataa hii kura sababu tunayajua haya".

Wananchi wanahofia hii kura ya tarehe 27 Oktoba, inaweza kuvuruga Uchaguzi wa Zanzibar.
View attachment 1609453
Hili bango linaonyesha ubaguzi wa aina fulani. Mleta bango unachosema ni nini - eti Zanzibar na Pemba - hakuna wasiokuwa Waislamu!? Ni kweli hicho unachosema au unadhani Unguja na Pemba hakufikiwi na watu wengine kiasi cha kuchangamana? Wale wanaolima kwa mikataba na tayari ni wakazi wa huko hawawezi kuwa hivyo na kuwa na haki ya kupiga kura za mapema? Tuache kutafuta vijisababu vya kushindwa mapema!
 
Back
Top Bottom