Zanzibar wana vitu gani vya kujivunia ukiachana na fukwe na utamaduni wao?

Tanganyika kuna mengi ya kujivunia ukiachana na viongozi butu wasio na maono wala hekima.

Lakini, swali langu kama linavyojieleza hapo juu, wenzetu wazanzibari wana kipi cha kujivunia tofauti na fukwe nzuri ya bahari, utamaduni wa kuvutia, labda, na muungano na Tanganyika?
Kabla ya kuandika ungeisoma historia na jografia ya Zanzibar , naamini usingeandika hii.
Ukiacha fukwe ambazo wewe unaona ni kitu kidogo sana, Zanzibar ina magofu na majengo ya kale, mimea ya viungo vya chakula na vyakula ambavyo kwa wenzetu wanaopenda mapishi ni maarufu sana, aina tofauti ya nyani na misitu na mwani.
Utalii wa pwani ni maarufu sana na duniani na vipo visiwa vinaingiza mapato makubwa sana na ni maarufu sana kuliko huku bara. Tatizo la utalii wa mbuga za wanyama si shirikishi sana kama utalii wa pwani ambao watu huogelea na kucheza kwenye maji, wanyama unawaangalia tu kwa mbali kisha unaondoka, hauwagusi wala kucheza nao.
 
Back
Top Bottom