Zanzibar waipiga tena kumbo Tume ya Katiba

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
0
uamsho5-564x423.jpg

WAZANZIBARI wamezidikudhihirisha kuwa muhimukwao kwa sasa ni juu yamadai yao ya kutambuliwakama nchi na dola kamilikwanza na wala sio la ainaya katiba.
Hayo yameendeleakujitokea mbele ya TUMEya Mabadiliko ya Katibaambapo Tume hiyo imejikutaikipokea maoni ya uwapoau kutokuwapo Muungano badala ya Katiba.Katika vikao katiya wajumbe wa tume nawananchi katika Shehiyatofauti Unguja, tume hiyoimeshuhudia wananchi
Na Mwandishi Wetu
walio wengi katika walewaliofika mbele ya tumewakitoa maoni yanayohusuaina ya Muungano kati yaTanganyika na Zanzibar.Akizungumza hivikaribuni juu ya hali hiyo,mwenyekiti wa timu yaTume ya Mabadiliko yaKatiba inayokusanya maonihayo Zanzibar, ProfesaMwesiga Baregu alikiri kuwawanachopata Zanzibar nikama kura za maoni kuhusukuwapo, kutokuwapo au ainaya mfumo wa Muunganowanaoutaka Wazanzibari.Taarifa zinaonyesha kuwakati ya watu 123 waliotoamaoni kwenye Shehiyaya Mombasa, kwa njia yakuzungumza ni mtu mmoja peke yake aliyetoa maoni yaKatiba Mpya. Na wakati akitoa maonihayo, ilikuwa wazi kuwaalikuwa akiwakera wengikwani wakati akijielezambele ya wajumbe wa tume,wananchi waliibua migunona zomeazomea ikiashiriakutofurahishwa na hatuayake hiyo; ingawa wajumbewa tume waliasa wananchikuvumiliana.Kwa upande mwingine,limetolewa somo juu yamuungano wa mkataba,msamiati na dhana ambayoumekuwa maarufu nakusemwa na wengi.Akitoa darsa hiyo kupitiamtandao, Ismail Jussaamesema kuwa Muungano waMkataba ni MASHIRIKIANOkati ya nchi mbili au zaidiambazo kila moja huwainabaki na mamlaka yakekamili ya KIDOLA kitaifana kimataifa lakini badozikawa zina mashirikianokatika maeneo maalumzitakazoamua kushirikiana,mahusiano ambayo huwayanaongozwa na Mkataba.Akifafanua zaidi akasemakuwa, Muungano waMkataba ni tofauti kabisana Muungano wa Kikatibaambao huwa unamaanishakuwepo kwa Serikali yaMuungano inayosimamiamambo ya Muungano.Katika Muungano waMkataba, Jussa anasema,kila nchi hubaki na Serikaliyake kamili yenye kusimamiamambo yote. Na kwamba, yalemaeneo ya USHIRIKIANOhusimamiwa kupitia amaKAMISHENI YA PAMOJAau KAMATI YA PAMOJAkwa kadiri makubalianoyatakavyokuwa yamewekwakwenye Mkataba.Akielezea faida zaMuungano wa Mkataba, Jussaamesema kuwa ni pamoja nakuwa inaondoa khofu ya nchimoja kuimeza au kuitawalianchi nyengine.Kwamba kila nchi inabakina uhuru na mamlaka yakekamili kitaifa na kimataifakuamua mambo yake.Kwa utaratibu huo, kilanchi mwanachama ina uhuruwa kujitoa katika jambololote ililoamua mwanzokushirikiana pale inapoonahakuna maslahi au faidakuendelea nalo.Kwa upande mwingineakasema kuwa, muungano wamkataba huvutia nchi nyingikuingia katika Muungano waaina hiyo kwa sababu hakunakhofu ya kupoteza mamlakaau kupunguziwa madarakaau mambo yake kuamuliwana nchi nyengine. Na hiyo ni kwa vile,mahusiano huwa ni yakirafiki na ya ujirani mwemayanayopelekea kuaminianana kuondoa kutiliana shakakusikokwisha.
 

Penguine

JF-Expert Member
Nov 29, 2009
1,306
2,000
Wazanzibar hawautaki Muungano. Tunawalazimisha tu. Kwa mtu ambae hajawahi kukutana na Waznzbr akawa anawasikiliza wanasiasa majukwaani, ataambiwa Muungano uko imara. Lkn kwa mtu aliyepata kuketi pamoja na waznzbr, akawatazama na kuwaskiliza, HAWAUTAKI Muungano.

Lkn kweli, kwa katiba yao ilivyo bado mtu husomi maandishi na picha huoni? Shein yupo vile alivyo kuhusu Muungano kwasababu ya viapo vya Dodoma. Lasivyo, yeye na watuwake hawautaki muungano.
 

Mjuni Lwambo

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
7,239
2,000
Kiukweli mimi naona wanachoenda kupresent wazanzibari kwenye maoni ya katiba mpya sio mawazo yao halisi, hawa watu ukichunguza utagundua kuwa wamekaririshwa hicho wanachokisema(probably kutoka misikitini au kwenye mikutano ya uamsho) na kwa maana hiyo basi kinachoprevail znzbar kuhusu maoni ya katiba mpya ni mawazo ya watu wachache wanayowakaririsha wananchi wa kawaida kwa sababu zilizojificha. Ukihudhuria utoaji wa maoni zanzibari kila mtoa maoni anatamka hichohicho bila kukosea hata nukta, Hata kwenye picha aliyoweka mtoa maada ambaye anaonekana kuamini ktk utengano utaona bango lilibebwa na kila mtoa maoni ni lile lile kuashiria kuwa it is from one source.
 

Mjuni Lwambo

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
7,239
2,000
Wazanzibar imefikia kipindi sasa wameaminishwa kuwa matatizo yao yote yamesababishwa na muungano, na ndio maana sasa hakuna wanachotoa maoni kwenye katiba ijayo bali wao wanaongelea muungano tu, INASIKITISHA.
 

Cynic

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
5,146
2,000
Kuna uwezekano mkubwa tu kwamba kwenye hatua ya kura ya maoni wazanzibari wataipiga chini katiba. Itakuwa vigumu mno kupata > 50% ya kura ZNZ
 

takashi

JF-Expert Member
Apr 1, 2009
905
195
Nyie mna chuki na Wakristo na si muungano. Be precise please.

Wakristo na Ukristo umekuwepo Zanzibar kabla ya Muungano...Wa Zanzibari wanadai mamlaka kamili juu ya mustakabali wa nchi yao na sio kingine. Zama za kuiburuza Zanzibar zimekwisha.
 

takashi

JF-Expert Member
Apr 1, 2009
905
195
Kiukweli mimi naona wanachoenda kupresent wazanzibari kwenye maoni ya katiba mpya sio mawazo yao halisi, hawa watu ukichunguza utagundua kuwa wamekaririshwa hicho wanachokisema(probably kutoka misikitini au kwenye mikutano ya uamsho) na kwa maana hiyo basi kinachoprevail znzbar kuhusu maoni ya katiba mpya ni mawazo ya watu wachache wanayowakaririsha wananchi wa kawaida kwa sababu zilizojificha. Ukihudhuria utoaji wa maoni zanzibari kila mtoa maoni anatamka hichohicho bila kukosea hata nukta, Hata kwenye picha aliyoweka mtoa maada ambaye anaonekana kuamini ktk utengano utaona bango lilibebwa na kila mtoa maoni ni lile lile kuashiria kuwa it is from one source.

Kinacho endelea Zanzibar kuhusu maoni ya katiba mpya ni matokeo kawaida tu. Zanzibar (waznz) wamekuwa wakilalamika kwa miaka mingi kuhusu mfumo wa Muungano jinsi unavyokandamiza haki za Zanzibar katika Muungano. Walichokipata ni dharau,kejeli, na vitisho. Sasa sio ajabu kuona wengi wao kuwa wanataka Zanzibar yenye malaka kamili. Dharau ina kikomo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom