kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,418
- 7,201
Binafsi nilishangaa kujua mfumo wa zanzibar ni kumaliza shule ya msingi darasa la sita kisha mtu anaenda form 1. Sijui wanakimbilia wapi? Au kwa vile shule zao kuna kina mama na kina baba wanalea japo wao ni watoto?
Mfumo huo pia umekua na matokeo duni ya kidato cha nne. Kila mwaka shule za Zanzibar zinashika mkia matokeo ya NECTA form IV na form VI.
Ningewashauri vigogo wa elimu Zanzibar kwa kushirikiana na bara ili kuwa na mfumo mmoja wa Jamhuri. Kwanza waondoe mfumo wa miaka 6 kwa elimu ya msingi ili mfumo uwe miaka 7 sawa na bara.
Na hili suala la watoto wazazi kuchanganyika kwenye shule japo Rais Samia kalitolea mfano liigwe huku bara ukweli linapingwa vikali na wengi. Kwa maoni yangu binafsi linachangia kukwamisha maadili na kushusha umakini wa mwanafunzi kutokana na kutangulizwa fikra zake kwenye mambo ya mapenzi na ndoa kabla ya muda muafaka.