Zanzibar Vs. Nyololo - Kuuliwa kwa Mwandishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar Vs. Nyololo - Kuuliwa kwa Mwandishi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bhikola, Sep 4, 2012.

 1. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu wana jamii, kwanza heshima mbele
  Kwanza niseme kuwa nimepokea taarifa za kifo cha mwenzetu kule nyololo kwa masikitiko makubwa sana, na mpaka sasa ninapoangalia picha zile, nashindwa kuelewa kabisa kuwa hiyo ni tanzania yangu ile ile ambayo viongozi wake wanatoka mapovu mdomoni kila siku kuinadi huku ulaya kwa hao majambazi wanaowaita wawekezaji kuwa ni kisiwa cha amani
  Katika kutafakari, kuna swali moja nimeloshindwa kujibu mpaka sasa, Kama waliweza kutuliza fujo za zanzibar zilizohusisha ghasia na vurugu kubwa pasipo kuua hata panzi, ikiwa bahati mbaya tu kwa panya wa kanisani walioungua wakati makanisa yanachomwa, lakini wanashindwa kuzuia au kutuliza watu ambao hata hawaandamani bali wamekusanyika mpaka waue watu?
  anyway - RIP Mwandosi, damu yako haitapotea bure, na kila ukombozi wa watanzania utakapo ongelewa, jina lako halitarukwa katika orodha ya waliomwaga damu

  PoliCCM wajue siku zote kuwa, hauwezi kunyamanzisha watu kwa kuwaua, unaweza kuwanyamanzisha kwa kusikiliza kelele zao
   
Loading...