Zanzibar: Viongozi wa UAMSHO wahojiwa na Polisi, kupandishwa kizimbani Jumatatu...

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Wakuu,

Kutakuwa na Joint Press Conference itakayofanywa na Jeshi la Polisi (Z'bar) wakiwa na Sheikh Fareed wa Uamsho. Najitahidi kuweza kuwarushia nini kimeongelewa kadiri nitakavyoweza.

Ni muda wowote kuanzia saa nne za asubuhi kwa mida ya Tanzania. Kwa sasa jamaa yupo Polisi. Huenda akahojiwa kwanza au wakaanza na Press Conference ili waachane na vyombo vya habari.

Tayari vyombo vya habari wapo hapa wakisubiri kujua nini kinaendelea.

>>~~~~~~<<
UPDATES:

Mpaka saa 4 usiku, walikuwa wanaendelea kuhojiwa na tayari imefahamika kuwa watafikishwa mahakamani Jumatatu.

Vyombo vya usalama vimejiandaa kukabiliana na purukushani za aina yoyote toka kwa wafuasi wa Uamsho.
Watu sita wamekamatwa kwa tuhuma za kumuua Afisa wa Polisi marehemu Said Abdulrahman.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa aliwaambia waandishi wa habari kwamba watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) walikamatwa sehemu tofauti, mmoja amekamatwa Kisiwa kidogo cha Tumbatu, wa pili maeneo ya Mjini Unguja, mtuhumiwa wa tatu alikamatwa ofisi za Idara ya Uhamiaji alikokwenda kushughulikia hati ya kusafiria ili aweze kutoroka hapa nchini.

Kamishna Mussa alisema watuhumiwa wengine watatu wamekamatwa Mkoani Tanga ambako walikimbilia kujificha baada ya kufanya mauaji ya Afisa Polisi Koplo Said Abdulrahman.

"Watu hao walitorokea huko na tunaendelea kuwahoji&#8230;tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao mkubwa uliotuwezesha kufanikisha ukamataji huo, tunavishukuru vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyo katika Shehia mbalimbali kwa kuimarisha ulinzi wa maeneo yao katika kipindi chote cha fujo na vurugu hizo" Alisema Kamishna Mussa.

Kamishna Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi la Polisi hivi sasa linawazuilia viongozi wakuu wa uamsho ili kuwahoji Sheikh Farid Hadi na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam ili kufahamu wapi alipokuwa na kuthibitisha kama kweli alitekwa ama la.

kufuatia kuzuiliwa kwa amiri mkuu wa jumuiya na taasisi za kiislam Zanzibar sheikh Msellem bin Ali, msemaji wa harakati hiyo sheikh Farid hadi na naibu amiri wa jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislam zanzibar jeshi la polisi limekuwa likizunguka katika maeneo mbali mbali kuweka ulinzi ili kuhofia kuvunjika tena kwa amani.

Vikosi vya SMZ vikiwa havina uniform maalum vimekuwa vikizunguka katika baadhi ya maeneo kupiga risasi juu huku kukiripotiwa baadhi ya nyumba kadhaa kuvamiwa na kufanywa vitendo vya wizi katika maeneo ya muembe makumbi.

Viongozi hao wamezuiliwa katika kituo cha polisi Madema baada ya kumsindikiza Sheikh Farid majira ya saa tatu za asubuhi leo kwenda kutoa maelezo.

Katika hatua nyengine Polisi imeonya kuchukua hatua kali dhidi ya wafuasi wa UAMSHO wanaodaiwa kutaka kuvamia kambi za Polisi, kambi za Majeshi na Ofisi za Serikali ya Mapinduzi.

"Natoa onyo kali kwa wananchi wote kuwa hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria, Jeshi la Polisi na Vikosi vyote vya ulinzi na usalama tumejipanga madhubuti kukabiliana na mtu yoyote ama kikundi chochote kitakachofanya vurugu" Alisema Kamishna Mussa.

Akizungumzia hali ya amani, Kamishna Polisi alisema kwamba Mji wa Zanzibar ni shwari kwa sasa na wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

"Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama vimeimarisha ulinzi, tunaomba wananchi wasiwe na hofu na waendelee kutii sheria za nchi bila kushurutishwa, waendelee kudumisha amani katika maeneo yao na pia waendelee kutupatia taarifa za mara kwa mara za hali ilivyo huko wanakoishi"
 
Apigane vita vya Mujahidina Afghanistan akiwa kati ya Makomandoo 300 wa Osama halafu leo atishwe na polisi wa Tanzania? nyinyi hamjui mambo yalivyo.
 
Huyu Shehe Fareed ametia doa uislamu, amewadhalilisha wafuasi wake, amesababisha mauaji, amesababisha uharibifu wa mali, ametowesha Amani, amedanganya. Hawa ndio mashehe wanaojitangaza wanataka kuleta maendeleo ya waislamu?
 
Huyu Shehe Fareed ametia doa uislamu, amewadhalilisha wafuasi wake, amesababisha mauaji, amesababisha uharibifu wa mali, ametowesha Amani, amedanganya. Hawa ndio mashehe wanaojitangaza wanataka kuleta maendeleo ya waislamu?

usanii wake umesababisha kifo cha mtu asiyekuwa na hatia,na mambo mengine mengh ya uvunjifu wa amani.
 
Natamani polisi waisome hii:
Nilimsikia kwa makini dereva wa sheikh Fareed wa UAMSHO akielezea jinsi walivyoachana na sheikh Faeed. Nimemsikia Fareed mwenyewe akieleza jinsi alivyoachana na dereva wake. Wote wanasema dereva alitumwa na Fareed akanunue umeme, hapo hawajatofautiana.

Tofauti inakuja pale ambapo dereva amesema alimuacha Fareed anaenda kwenye gari (la waliomteka) wakati Fareed anasema gari (la waliomteka) lilikuja wakati dereva ameenda kununua umeme.

Kwa lugha nyingine, dereva anasema aliliacha gari la watekaji likiwa limeshafika na Fareed alilifuata mwenyewe, lakini Fareed amesema wakati gari (la waliomteka) linafika, dereva hakuwepo!

Wachambuzi wa mambo hebu angalieni hapo, inavyoonekana huyu sheikh hakuipanga vizuri hii movie na dili limeshabumbuluka!

Na hii:
 
Naona Aibu kwa kweli kila mtandao ninaoingia nakuta habari za machafuko yanayosababishwa na Dini yangu ila naomba ndugu tusielewane vibaya sababu hawa ni wachochezi na si waislam kwel
 
Polisi wa ZNZ ni mdebwedo au ulojo!!!! wanafanya press conference na Gaidi! Hii ni hatari jamani! sheikh Farid alitakiwa awe ametiwa hatiani.
 
Back
Top Bottom