Zanzibar 2020 Zanzibar: Vikosi vya SMZ Vyavamia Ofisi ya Ngome ya Vijana wa ACT-Wazalendo. Nassor Ahmed Mazrui atekwa

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
602
1,526
Vikosi vya SMZ jana usiku walivamia Barza ya Mwanakombo; hii ni Ofisi ya Ngome ya Vijana wa @ACTwazalendo. Vitu walivyoiba ni Tv na Viatu, pia waliondoka na Mlingoti wa Bendera.

Aidha leo hii Naibu Katibu Mkuu wetu upande wa Zanzibar ametekwa na watu wanaosemakana kuwa ni Vijana wa Jeshi la JKU.

Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe kupitia akaunti yake ya Twitter, amezitaka Mamlaka za Zanzibar kumuachilia mara moja Ndugu Mazrui.

ABE318DD-A8A4-4497-9E67-6288B1D8CA7E.jpeg
 
Naibu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui anadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana baada ya gari lake kugongwa eneo la Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi ( JKU).

Inadaiwa baada ya tukio la kugongwa, watu ambao hawafahamiki walimkamata na kutokomea naye kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo Jumapili Oktoba 25, eneo la Saateni wakati Mazrui ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya kampeni za Maalim Seif Sharif Hamad, akielekea katika ofisi za Makao Makuu ya ACT-Wazalendo zilizopo Vuga, Unguja.

Katika akaunti ya Twitter ya Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe aliposti taarifa hiyo akitaka watu waliomchukua wamuachie mara moja kiongozi wake anayewania pia uwakilishi katika jimbo la Mwera lililopo mkoa wa Mjini Magharibi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

"Uchunguzi ukikamilika tutatoa taarifa zaidi.Kwa sasa siwezi kulielezea kwa urefu tukio hilo ila ni kweli tumepokea taarifa hizo tumeshaanza kuzifanyia kazi," amesema Kamanda Haji.

021FBE15-29A9-43F0-8C72-78A923E94C9E.jpeg

=====

Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui anadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana baada ya gari lake kugongwa eneo la Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi ( JKU).

Inadaiwa baada ya tukio la kugongwa, watu ambao hawafahamiki walimkamata na kutokomea naye kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea asubuhi hii ya Jumapili Oktoba 25, eneo la Saateni wakati Mazrui ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya kampeni za Maalim Seif Sharif Hamad, akielekea katika ofisi za makao makuu ya ACT-Wazalendo zilizopo Vuga, Unguja.

Katika akaunti ya Twitter ya Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe aliposti taarifa hiyo akitaka watu waliomchukua wamuachie mara moja kiongozi wake anayewania pia uwakilishi katika jimbo la Mwera lililopo mkoa wa Mjini Magharibi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji akizungumza kwa simu na Mwananchi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

"Uchunguzi ukikamilika tutatoa taarifa zaidi.Kwa sasa siwezi kulielezea kwa urefu tukio hilo ila ni kweli tumepokea taarifa hizo tumeshaanza kuzifanyia kazi," amesema Kamanda Haji.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom