Zanzibar 2020 Zanzibar: Vikosi vya SMZ Vyavamia Ofisi ya Ngome ya Vijana wa ACT-Wazalendo. Nassor Ahmed Mazrui atekwa

Jamani haya mambo ya kishamba tuacheni hii kane ya 21 watu washindane kwa hoja sio mambo ya kutekana hatuhitaji kufika huko amani ya nchi hii ni muhimu kuliko maslahi ya mtu au chama. pigeni kampeni wacha watu waamue wakichagua hovyo watajifunza wenyewe.

Hatujamaliza mambo ya mashekh mnaanza huu ujinga kwanini? watu wamechoka amani? kulikuwa na watu wana nguvu na wako mpaka leo huko Belarus yule alikuwa haguswi lakini anapambana na watu huu mwezi wa pili sembuse sisi. Waachieni wote waliofungwa kisiasa tushindane tu kwa amani. Naiombea amani nchi yangu maana kurudisha amani ni miaka kuvunja siku moja tu.
 
Nikitazama hivi video, sioni ni kwanini vijana wa kizanzibari wanakimbia wakati wako katika makaazi yao. Niliwahi kushauri huko nyuma na sasa narudia tena. Watu wajitathmini na kujipanga kulinda makazi yao.

Huwezi kuishi katika mtindo huu wa kukimbia kukimbia kila wakati. Hao vijana wa JKU wanatakiwa wasiweze kufika katika makaazi jua linapotua. Lazima wananchi waunde vikundi vyao ya kujihami.

Hili wazo sio geni, ni sawa na lile la Sungu-sungu miaka ile ya huko nyuma. Huwezi kuishi ukiwa na woga na khofu ya kukimbia kimbia mara zote ukiwa mtaani kwako. Kama mapanga yapo, kama mikuki ipo inatosha kulinda familia zetu na mitaa yetu ikawa salama.

Nasikitishwa sana na hali hii ya kuona vijana wakikosa amani ya kuishi na badala yake wakiwa wanakimbia kimbia kimbia badala kuwakabili hao JKU.
 
Vikosi vya SMZ siku hizi limebaki jina tu.Makamanda karibu wote ni watau wakuja na sijui ni nani aliyewaleta.Wangekuwa ni JKU wazalendo wasingekuwa washari namna hii.Huwa hawana huruma na wazanzibari.
 
Hivi Nigeria wamewezaje?!
Wana elimu,elimu uleta ujasiri,na mbinu za kupambana na wahuni.Maana Kama vyombo vya dola wakianza kufanya vitendo vya kihuni vya kukiuka sheria na kanuni ziwaongozao ugeuka kuwa ni genge la wahuni ambalo yafaa sasa kupambana na wahuni na zipo njia nyingi za kuwadhibiti wahuni hata Kama wamekuja na silaha za Moto.

Mfano hao wahuni waliokuja hapo znz ingepigwa yowe wakazingirwa pande zote na asitoke mtu kwa maana wamekuja Kama wahuni.
 
Tunawasihi watanzania kufuata sheria, kutofanya fujo wala kuharibu mali. Tuwe watulivu muda wote huku tukisimamia haki zetu. Tupige na kulinda kura zetu bila hofu wala woga wowote hii ni Haki zetu kisheria. Ukipiga kura kaa umbali wa mita 200 kutoka kituo cha kura. TUTASHINDA!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana elimu,elimu uleta ujasiri,na mbinu za kupambana na wahuni.Maana Kama vyombo vya dola wakianza kufanya vitendo vya kihuni vya kukiuka sheria na kanuni ziwaongozao ugeuka kuwa ni genge la wahuni ambalo yafaa sasa kupambana na wahuni na zipo njia nyingi za kuwadhibiti wahuni hata Kama wamekuja na silaha za Moto.
Mfano hao wahuni waliokuja hapo znz ingepigwa yowe wakazingirwa pande zote na asitoke mtu kwa maana wamekuja Kama wahuni.
Zanzibar nao wanapiga yowe?!

Huku kwetu Musoma ukipiga yowe lazima mtu afe.

Utadhani watu huwa wanasubiria yowe, yani hujamaliza huuuuwii, kadakwa.
 
1603623714042.png
 
Dah yaani kumbe siku hizi JKU wamekuwa na mamlaka na majukumu ya kijeshi? JKU si ilikuwa ni kama JKT tu huko nyuma na watu wanakwenda kwa mwaka mmoja mmoja tu wa kujenga taifa? Inaonyesha mambo yamebadilika na sasa wanajiona wao kama FFU!
 
Jibu swali alifuata nini kwenye Kambi ya Jeshi?
Kwani Lugalo nje hakuna barabara ya kwenda Bagamoyo?
Si walikuwa wanamfuata kwa nyuma wakiitafuta site ya kufanya uhalifu wao!!!
Au mwenzetu umeelewa kambini ni ndani wanapotunzia silaha?
 
Kwa hali iliyovyo Visiwani Zanzibar kwa sasa Spark ndogo inaweza kuleta Mlipuko wa Hatareee

Ole wao CCM wasimtangaze mshindi wa HAKI ole wao.
 
Yaani sasa hivi mtu anaweza kwenda kw mchepuko wake halafu Inasingiziwa CCM.
 
Meseji za whatsap huwa hazifanani ivyo, pia mawasiliano hayo ni ya kutengeneza.

Lkn hata kama ni ivyo matendo ya vyombo vya dola ni ya kipuuzi sana, wanafanya uhalifu kwa wapinzan mda wote.

Wamewakamata viongozi wa chadema kanda ya ziwa ati wana kadi za watu za kupigia kura, ivi hili zoezi la kutafuta mawakala haliitaji kutolewa kopi ya vitambulisho vya nec vya mawakala kwa ajili ya kuambatanishwa.

Askari hawa hawalijui hili?? Mbona hata nec wenyewe hawalisemei hilo? Ayo ni maandalizi ya mbeleko kwa ccm
 
WanaJf, Salaam!

Kitendo kilichovumishwa kwamba Nassor Mazurui ametekwa nakiona kama njama za ACT Wazalendo kujiongezea umaarufu, kuzua taharuki na kuipaka matope Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Siasa ziwepo lkn tuache kutengeneza matukio kwa ajili ya kupata kura za huruma.

Siasa ziwepo lkn tuache kutengeneza taharuki dhidi ya wapigakura na kuwachonganisha na Serikali yao inayowapenda na kuwathamini,

Mwisho tarehe 28 Oktoba 2020 imefika tujitokeze kuichagua CCM
 
Back
Top Bottom