Zanzibar: Vigogo wa Upinzani Tanzania wakutana kujadili mwenendo wa siasa na demokrasia

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
Viongozi wa vyama vya upinzani wakiwa Zanzibar.
Zanzibar6.jpg


Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa vya upinzani nchini wamejichimbia visiwani Zanzibar kwa ajili ya kupatiana mafunzo mbalimbali juu ya mwenendo wa siasa na demokrasia.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi, pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa na Kiongozi wa ACT - Wazalendo Zitto Kabwe.

Mbali na hao, viongozi wengine walionekana na Rais wa Chama Cha Mawakili Tanzania, (TLS) Fatma Karume pamoja viongozi wengine mashuhuri nchini ambapo imeelezwa walijadili juu ya mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.

Akizungumza na www.eatv.tv Kaimu Msemaji wa chama cha CUF, Mbarara Mahagande amesema kikao hicho kimeandaliwa na taasisi ya Marekani IRSA kupitia kwa Katibu wa CUF, Maalim Seif.

"Ni kweli kuna semina inafanyika ya viongozi wa vyama inafanyika Zanzibar ambayo inafanyika kwa siku tatu, na aliyewaalika ni Katibu Mkuu wetu Maalim Seif na imeandaliwa na taasisi ya IRSA, watu wa democratic ya America," amesema Maharagande.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Maalim Seif aliandika "ni heshima kubwa kwangu na kwa CUF kuandaa na kuwa mwenyeji wa kikao cha kutathmini demokrasia yetu na kujitathmini sisi wenyewe kama vyama vya upinzani na mwelekeo wetu."
 
Watatumika sana lakini hawatafaulu, baada ya Zanzibar wataitwa Ulaya na America, watapewa fedha, mafunzo, mbinu na vifaa kwaajili ya 2020
Hayo maneno tu, hata kwenye chupi yapo.

Subirini "MTUNGO" wa EU na USA, ndio akili zitawakaa sawa. Kama waliweza kumkalisha kitako Saddam Hussein, Muamar Gaddafi, Robert Mugabe, nyie kina nani msitulie?
 
Back
Top Bottom