Zanzibar: Ugaidi wa mazombi umeanza tena Unguja

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
33,235
8,779
Mazombi yakiongozwa na Polisi ya CCM yafanya ugaidi wa kuwashambulia wananchi tukielekea uchaguzi .

Wakaazi wa eneo la Kisauni, magharibi mwa kisiwa cha Unguja, wanasema kuwa usiku wa jana (Ijumaa 14 Februari 2020), walivamiwa na kundi la mazombi likisindikizwa na jeshi la polisi, baadhi yao wakapigwa, kuvunjiwa nyumba zao na kuibiwa fedha na vitu vyengine.

Huu ni wakati kwa Wazanzibari wote mlioko nje ya nchi kuanza maandamano ya kupinga vitendo hivi na kudhalilishwa Wazanzibari kwenye muungano. Pia kuandamana kupinga kukandamizwa Demokrasia Tanganyika na Zanzibar
 
Mazombi yakiongozwa na Polisi ya CCM yafanya ugaidi wa kuwashambulia wananchi tukielekea uchaguzi .

Wakaazi wa eneo la Kisauni, magharibi mwa kisiwa cha Unguja, wanasema kuwa usiku wa jana (Ijumaa 14 Februari 2020), walivamiwa na kundi la mazombi likisindikizwa na jeshi la polisi, baadhi yao wakapigwa, kuvunjiwa nyumba zao na kuibiwa fedha na vitu vyengine.

Hii ni hatari sana tunaomba serikali iliangalie jambo hili tukumbuke mjusi akifukuzwa sana hubadilika na kuwa nyoka
 
Hawa watu wanaoshirikiana nao kufanya huu uharamia wengi wao wanajuilikana. Dawa yao ni kuwavizia wakati wakiwa uraiani kuwavamia mmoja baada ya mmoja na kuwatia adabu tu. Kulipiza kisasi ni haki mbele ya Mungu. Haiwezekani watu wanauwa raia wasio na hatia na wao mukawatizama tu. Hao wanatumwa na kutumika kwa maslahi ya wachache wenye uroho wa madaraka bila ya kujali utu. Wakianza kutiwa adabu basi huo uharamia wataacha lakini kwa maneno tu mutakuja kushtukizia mushamalizika!
 
Back
Top Bottom