Zanzibar: TAMWA yasikitishwa na kitendo cha udhalilishaji cha kuwachoma sindano watoto bila ya sababu

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,779
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ) kinasikitishwa na kitendo cha udhalilishaji ambacho kimezuka hivi karibuni cha kuwachoma sindano watoto bila ya sababu.

Wakati nchi inaendeleza juhudi za kupambana kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kubakwa, kulawiti, kupigwa, ndoa na mimba za utotoni dhidi ya watoto, inasikitisha kuona kuwa imezuka aina nyengine ya udhalilishaji kwa kuwachoma watoto sindano.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari ikiwemo shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kupitia kitendo chake cha Mawiyo ni kwamba juzi watoto watatu walichomwa sindano na mtu asiyejulikana.

Taarifa hizo zimeeleza kwamba watoto hao watatu ambao wawili kati yao wana umri wa miaka mitano huku mmoja akiwa na miaka saba walidaiwa kuchomwa sindano na mtu aliyetenda tukio hilo kukimbia sehemu isiyojulikana huku watoto wamebaki na kilio cha maumivu ya sindano.

Tukio hilo liliripotiwa Septemba 15, 2020 huko katika shehia ya Mwanyanya wilaya ya Magharib A, Mkoa wa Mjini Magharib Unguja wakati watoto hao wakitoka skuli na kuelekea nyumbani.

TAMWA ZNZ kinaamini tukio hilo si la kawaida hivyo tunaviomba vyombo vya sheria kulichukulia hatua kali kwani hii ni mara nyengine kitendo hicho kimeripotiwa katika kisiwa cha Unguja.

TAMWA 1.jpg


Kitendo kama hicho kiliripotiwa Januari 10, 2020 eneo la Daraja bovu ambapo watoto sita(6) wenye umri wa miaka 4 hadi minane(8) walichomwa sindano bila ya sababu na mtu aliyefahamika kwa jina la Salim Ali Malik ambapo kesi yake ilitolewa kuhumu tarehe 24/8/2020 katika Mahakama ya Mwanzo Mwanakwerekwe ambapo mtuhumiwa alitakiwa kulipa shilingi laki 600,000 au kwenda kutumia kifungo cha miezi sita.

Kwa mujibu wa hali ya maisha ya sasa kiasi hicho ni kidogo sana kutokana na ukubwa wa kosa hilo na hivyo hakiwezi kuwatisha ipasavyo wanaofikiria kufanya vitendo hivyo.

Aidha TAMWA ZNZ inaishauri Serikali ifanye utaratibu maalum wa kuchunguza suala hili ili ielewe dhamira hasa ya baadhi ya wahalifu hao kufanya vitendo hivyo. Kutokana na taarifa za wazazi wa watoto sita waliochomwa sindano zimeeleza kwamba sindano hiyo ilikuwa na sumu ya kuweza kuua mtu.

TAMWA 2.jpg
 
Baada ya kuchomwa hawakupata infection yeyote baada ya kupimwa ?

Wasije kuwa wanasambaza ukimwi
 
Huyo Malik aliyetiwa hatiani alitakiwa abanwe p&mbu kwa koleo la moto (redhot) lililopakwa pilipili kichaa hadi aseme ni kwanini aliwachoma sindano watoto hao??!!, this doesn’t make sense??!!
 
Vitu kama hivi kama ni kweli havihitaji kuvumiliwa kabisa , lazima akamatwe ahojiwe kwanini amefanya kitendo hicho na aeleze aliyemtuma ni nani na kwanini
 
Back
Top Bottom