#COVID19 Zanzibar: Serikali yapokea msaada wa vifaa vya haraka vya kupimia COVID 19 aina ya Rapid Test

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
605
1,536
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yapokea msaada wa vifaa vya haraka vya kupimia COVID 19 aina ya Rapid Test, vyenye thamani ya shilingi Milion 250 za Kitanzania.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar amepokea msaada huo kutoka kwa kampuni ya SD BIOSENSOR ya nchini Korea.

Makabidhiano hayo ya vifaa vyenye uwezo wa kutoa majibu ya COVID 19 ndani ya dakika 15, yamefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni mjini Zanzibar.

"Msaada huu umefika katika kipindi muwafaka ambapo Serikali inaongeza kasi za mapambano dhidi ya maradhi ya Corona" alieleza Makamu wa kwanza.

Aidha Mheshimiwa Othman amesema kwamba, awali vipomo vya COVID 19, vilikuwa vikifanyika zaidi kwa wasafiri ama watu wanaoshukiwa kuwa na maambukizi, lakini kwa msaada huu wa vifaa vipya na vyenye uwezo mkubwa, zoezi la upimaji litaweza kupanua wigo zaidi mpaka katika maeneo ya kijamii.

Pamoja na hayo Makamu wa kwanza, amefafanua kwamba Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuweka miundombinu mizuri ya kinga,uchunguzi na namna ya matibabu kwa watakaobainika kuambukizwa ugonjwa huo.

Nae Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,jinsia na Watoto Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kwamba kwasasa ,Zanzibar hakuna hata mgonjwa mmoja ambae amethibitika kuwa na COVID 19, ila ameitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari.

Mwakilishi wa kampuni ya SD BIOSENSOR, Bwana Sunjay Padatia, amesema wao wametoa msaada wa vifaa hivyo ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya janga la CORONA.

IMG-20210521-WA0027.jpg
 
Ni jambo jema, Tanzania sasa inarudi wenye misingi yake kuyatambua majanga ya kimataifa kama ni yetus sote badala ya kujitenga.
 
Kwani anayesimamia msaada kama huo huku Bara ni nani? Au umeingia kimya kimya kisha kuuzwa kimagendo?
 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yapokea msaada wa vifaa vya haraka vya kupimia COVID 19 aina ya Rapid Test, vyenye thamani ya shilingi Milion 250 za Kitanzania.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar amepokea msaada huo kutoka kwa kampuni ya SD BIOSENSOR ya nchini Korea.

Makabidhiano hayo ya vifaa vyenye uwezo wa kutoa majibu ya COVID 19 ndani ya dakika 15, yamefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni mjini Zanzibar.

"Msaada huu umefika katika kipindi muwafaka ambapo Serikali inaongeza kasi za mapambano dhidi ya maradhi ya Corona" alieleza Makamu wa kwanza.

Aidha Mheshimiwa Othman amesema kwamba, awali vipomo vya COVID 19, vilikuwa vikifanyika zaidi kwa wasafiri ama watu wanaoshukiwa kuwa na maambukizi, lakini kwa msaada huu wa vifaa vipya na vyenye uwezo mkubwa, zoezi la upimaji litaweza kupanua wigo zaidi mpaka katika maeneo ya kijamii.

Pamoja na hayo Makamu wa kwanza, amefafanua kwamba Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuweka miundombinu mizuri ya kinga,uchunguzi na namna ya matibabu kwa watakaobainika kuambukizwa ugonjwa huo.

Nae Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee, jinsia na Watoto Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kwamba kwasasa, Zanzibar hakuna hata mgonjwa mmoja ambae amethibitika kuwa na COVID 19, ila ameitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari.

Mwakilishi wa kampuni ya SD BIOSENSOR, Bwana Sunjay Padatia, amesema wao wametoa msaada wa vifaa hivyo ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya janga la CORONA.

IMG_20210522_041813_961.jpg
IMG_20210522_041819_090.jpg
 
"Nae Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,jinsia na Watoto Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kwamba kwasasa ,Zanzibar hakuna hata mgonjwa mmoja ambae amethibitika kuwa na COVID 19"…..….
 
Sijui na kile kipimo kipya cha kichina kimo? Mhh, mimi mpaka kwa ncha ya upanga, 'uchiteme wala uchimung'unye njomba' ndo naenda kupima.
Sasa mkuu km umezaliwa kwa mpalange shughuli zako ziko kariakoo, utafia kwa mpalange utazikwa kwa mpalange, covid uipime ili nini. Upatiwe chanjo ili nini?

Wenzako sasa wanatoka nje ya nchi ili maisha yaendelee. Hao ni lazima wakapime na wapatiwe chanjo.
 
"Nae Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,jinsia na Watoto Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kwamba kwasasa ,Zanzibar hakuna hata mgonjwa mmoja ambae amethibitika kuwa na COVID 19"…..….
Hizi rapid test kits zimekuwa programmed kutoa fake positive results kwa asilimia kubwa ili kuipa kiki çorona!!
 
Sijui na kile kipimo kipya cha kichina kimo? Mhh, mimi mpaka kwa ncha ya upanga, 'uchiteme wala uchimung'unye njomba' ndo naenda kupima.
Tatizo ni propaganda... watoto wenu wakizaliwa wanachanjwa wala hakuna anayehoji kuhusu usalama au madhara ya hizo chanjo!!! Ama ni ubinafsi au woga?
 
Hizi rapid test kits zimekuwa programmed kutoa fake positive results kwa asilimia kubwa ili kuipa kiki çorona!!
Uongo ni pale unatoa taarifa isiyo halisi kama vile ni jambo halisi! Nyie ndo wale ‘wapima mapapai’ kuprove uongo wenu, kisha wenyewe mnapigwa dafrao na corona hiyo hiyo!
 
Back
Top Bottom