ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 608
- 1,540
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yapokea msaada wa vifaa vya haraka vya kupimia COVID 19 aina ya Rapid Test, vyenye thamani ya shilingi Milion 250 za Kitanzania.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar amepokea msaada huo kutoka kwa kampuni ya SD BIOSENSOR ya nchini Korea.
Makabidhiano hayo ya vifaa vyenye uwezo wa kutoa majibu ya COVID 19 ndani ya dakika 15, yamefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni mjini Zanzibar.
"Msaada huu umefika katika kipindi muwafaka ambapo Serikali inaongeza kasi za mapambano dhidi ya maradhi ya Corona" alieleza Makamu wa kwanza.
Aidha Mheshimiwa Othman amesema kwamba, awali vipomo vya COVID 19, vilikuwa vikifanyika zaidi kwa wasafiri ama watu wanaoshukiwa kuwa na maambukizi, lakini kwa msaada huu wa vifaa vipya na vyenye uwezo mkubwa, zoezi la upimaji litaweza kupanua wigo zaidi mpaka katika maeneo ya kijamii.
Pamoja na hayo Makamu wa kwanza, amefafanua kwamba Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuweka miundombinu mizuri ya kinga,uchunguzi na namna ya matibabu kwa watakaobainika kuambukizwa ugonjwa huo.
Nae Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii,Wazee,jinsia na Watoto Zanzibar, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kwamba kwasasa ,Zanzibar hakuna hata mgonjwa mmoja ambae amethibitika kuwa na COVID 19, ila ameitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari.
Mwakilishi wa kampuni ya SD BIOSENSOR, Bwana Sunjay Padatia, amesema wao wametoa msaada wa vifaa hivyo ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya janga la CORONA.