Zanzibar: Rais Mwinyi atengua uteuzi wa viongozi watano

Kiturilo

JF-Expert Member
Sep 27, 2021
709
2,858
Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa viongozi katika Wizara za elimu, Uchumi na Uwekezaji na wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Katibu Mkuu Mtendaji, Zena Said leo Februari 3, 2022 imewataja waliotenguliwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Omar Ali Omar.

Mwingine aliyetajwa katika taarifa hiyo ni Suleiman Yahya Ame Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu katika wizara hiyo ya elimu.

Wengine ni Fatma Iddi Ali, Kamishna wa Kazi katika ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji na Salum Ubwa Nassor, Ofisa Mdhamini, Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Pemba.

Katika orodha hiyo pia kuna Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Watoto katika Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Nasima Haji Choum

Ametengua nafasi hizo kuanzia leo.

20220203_123823.jpg
 
Amewafuta kazi, siyo kutengua uteuzi.

Sujui kwanini huwa taarifa hizi hurembwa na neno "kutengua uteuzi" badala ya "kufukuza kazi", "kufuta kazi" au "kusitisha kazi/mkataba".
 
Anatengua uteuzi lakin wanaendelea na majukumu kama Watumishi wa Umma,

Ukiwa Mkurugenzi wa Halmshauri ukaachishwa hiyo kazi na kuendelea kuwa Afisa Mipango au Afisa utumishi hapo unakuwa umetenguliwa Uteuzi ila hukafukuzwa kazi
Amewafuta kazi, siyo kutengua uteuzi.

Sujui kwanini huwa taarifa hizi hurembwa na neno "kutengua uteuzi" badala ya "kufukuza kazi", "kufuta kazi" au "kusitisha kazi/mkataba".
 
Nadhani huyu jamaa ndio Rais anayeongoza kwa kutengua watu duniani kwa sasa , Cha kushangaza sasa dhiki ya Wazanzibar iko palepale !
Wazanzibari hawana shida wala dhiki.

Wenye shida ni Chadema ndio maana chama mlimuuzia Lowassa kwa fedha kiduchu tu ambazo hata kuwasaidia mjenge ofisi hazikuweza.
 
Japokua "kufukuza wengine" sio kipimo pekee (au si kipimo kabisa) cha uongozi mzuri, nadhani Prof. Kitila, Mwita Waitara, Dr. Chamuriho na Godfrey Mwambe "walifukuzwa" na mwenyekiti wa Yanga Mshindo Mbete Msolla.
Tunanukuu maneno yake aliyosema mwenyewe juzi kwenye kitchen party ya mawaziri.
 
Back
Top Bottom