Zanzibar: Rais atia saini miswaada mitatu - Spika

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho amewaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba tayari rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Sheni ametia saini miswaada mitatu iliyopitishwa na wajumbe hao katika kipindi cha Baraza la Wawakilishi kilichopita na sasa kuwa sheria kamili.

Kificho alisema miswaada mitatu iliyotiwa saini na rais ni pamoja na mswaada wa kuanzishwa kwa maabara ya mkemia mkuu wa serikali, mswaada wa kuanzishwa kwa shirika la taifa la biashara Zanzibar (ZSTC) pamoja na usanifu wa kuendesha mazao mengine na mswada wa kurekebisha baadhi ya sheria na kuweka kanuni za baraza.

‘Wajumbe wa baraza la wawakilishi nafurahi kuwajulisha kwamba miswaada mitatu iliyopitishwa na baraza hili tayari imekuwa sheria baada ya kutiwa saini na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi' alisema Spika.

Aidha Spika aliwajulisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu mabadiliko yaliyofanywa na rais wa Zanzibar Dk Sheni ya kumuondowa katika nafasi ya katibu wa baraza, Ibrahim Mzee Ibrahim.

Kificho alisema kwamba Ibrahim ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kusema huo ni wadhifa mkubwa hata kuliko nafasi yake ya awali.

‘Nataka wajumbe wa baraza la wawakilishi kukujulisheni mabadiliko hayo ambapo sasa mwenzetu Katibu wa Baraza Ibrahim hayupo tena na sisi baada ye kuteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP)' alisema Kificho.

Kificho aliwafahamisha wajumbe wa baraza la wawakilishi na kusema kwamba wadhifa huo ni mkubwa wenye hadhi ya kimataifa ikiwa ni sawa na Jaji wa Mahakama Kuu.

chanzo: Zanzibar yetu
 
mambo ya wazazimbari waachie wazanzibar, mm nimeshtuka nikajiuliza miswaada ipi tena kumbe ya akina yahee
 
mambo ya wazazimbari waachie wazanzibar, mm nimeshtuka nikajiuliza miswaada ipi tena kumbe ya akina yahee
.
Hata mimi nilidhani ni mambo ya Tanganyika, kumbe ni mambo ya nchi ya kigeni.
 
Hongera sana Mh Ibrahim Mzee. kinachotakiwa ni uadilifu na kufata sheria na kaanun za nchi.

hilo ndilo jambo jema
uadilifu,kujitoa kwa ajili ya Taifa lako,uzalendo ili hayo yatimie ni lazima tufuate azimio la arusha
 
Mambo ya kizanzibari waachiwe wenyewe. Waweke hata sheria ya kuviuza visiwa vyao hayatuhusu.
 
mambo ya nchi za nje anayajua bernad membe na ubalozi wetu huko.
sisi tunashughulikia nchi yetu ya maziwa na asali ambayo imeliwa na wakoloni mambo leo na vibaraka wao.
 
Jamani mtoa mada ungesema kama unaongelea nchi jirani ya zanzibar kuwa rais wao ametia ................ na bala bla nyingine

Umenishitua nikajua na ya ule wa kuongeza posho umesainiwa kumbe waongelea nchi za watu, yaani umenadika kama magazeti ya udaku kichwa cha habari tofauti na habari ndani todauti ila ndo ushanunua gazeti ufanyeje.

Nadhani haya masuala ya nchi za watu hayatuhusu sana sisi watanganyika, ya kaizari ayajue kaizari na ya kwetu tuyajue wenyewe...
 
...Kificho aliwafahamisha wajumbe wa baraza la wawakilishi na kusema kwamba wadhifa huo ni mkubwa wenye hadhi ya kimataifa ikiwa ni sawa na Jaji wa Mahakama Kuu....
Mbona hili ameliwekea msisitizo? Ina maana kwa kupewa wadhifa huo mpya watu wengi wangalifikiri amekuwa 'demoted'? Sijaona haja ya kujihami kwa suala ambalo lipo 'wazi'!
 
tukisha ongezewa mipaka ya bahari hii inchi ya zanzaibar itakuwa kama lethoto safi sana:poa:poa
 
Back
Top Bottom