Zanzibar: Polisi afukuzwa kazi baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mtu aliyekuwa akikabiliwa na kosa la wizi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,763
4,326
JESHI la Polisi Zanzibar limemfukuza kazi askari polisi Hussein Yahya Rashid (36) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kusababisha kifo cha Mussa Suleiman ambaye alituhumiwa kwa kosa la wizi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Awadh Juma Mohamed alithibitisha kufukuzwa kazi kwa askari Polisi Hussein mwenye namba za uaskari 3307412 ambaye Novemba 11 mwaka jana alimkabidhi mtuhumiwa wa kosa la wizi kwa raia ambao walimshambulia hadi kusababisha kifo chake.

Alisema askari huyo alitakiwa kumkabidhi mtuhumiwa kwa jeshi la Polisi au kituo chochote kile ili kupata hifadhi na kusubiri taratibu nyingine za upelelezi pamoja na kufunguliwa mashtaka.

Alifahamisha kuwa siku zote wahalifu wanapotenda makosa kimbilio lao ni vituo vya ulinzi ikiwemo Jeshi la Polisi ambapo wanaamini kwamba hatua za kisheria zitafuatwa, ikiwemo kufunguliwa mashtaka.

“Ni kweli Jeshi la Polisi limemfukuza kazi aliyekuwa askari wake, Hussein Yahya Rashid ambaye alimkamata raia anayetuhumiwa kwa makosa ya wizi...sasa yeye badala ya kumpeleka katika kituo cha Polisi alimsalimisha kwa raia wenye hasira na kusababisha kifo chake,” alisema.

Kamanda Awadhi aliwataka askari wengine wa jeshi la polisi kuzifahamu sheria zinazoliongoza jeshi hilo ambalo linafanya kazi zake kwa ushirikiano mkubwa na raia.

“Jeshi la Polisi kazi yake kubwa ni kulinda usalama wa raia maisha yao na mali zao, huwezi kumkamata mtuhumiwa wa kosa la wizi na kumpeleka kwa raia wenye hasira na kumuua,”alisema.

Habari Leo
 
Polisi wakiua wasishitakiwe. Alisema rais wetu mpendwa.

Huyu alipashwa kupelekwa kortini kushitakiwa kwa kosa la mauaji/mauaji bila kukusudia. Ningelkuwa Judge ningelimpa kosa la kuua kwa kukusudia maana alijua fika kuwa mob kustice in Tanzania ni kumuua mtuhumiwa na ndiyo maana alimkabidhi kwa raia akijua fika watampiga na ende result ni kifo (as a rule in Tanzania when it comes to mob justice)
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom