Zanzibar: Padre apigwa Risasi na watu wasiojulikana

Status
Not open for further replies.

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Kwa mujibu wa Breaking News Sasa hivi toka Radio One, Padre anayejulikana kwa jina la Ambrose Mkenda amepigwa Risasi na Watu wasiofahamika kwenye gate la nyumbani kwake wakati akifunguliwa gate aingie nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar, ambako ndiko makazi yake yalipo akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha pekee yake.

Hali yake sio nzuri kwani Risasi aliyopigwa imemdhuru maeneo ya mdomoni.

Waliompiga Risasi Padre huyo inasemekana ni watu waliokuwa kwenye pikipiki, ambao walimvamia akisubilia afunguliwe gate kuingia nyumbani kwake.

Kuna nini? Katika siku muhimu kwa waumini wa Kikristo kufanyika kwa tendo kama ilo kwa kiongozi wa madhehebu makubwa kama Roman Catholic.

Wanaojua kinachojili huko Zanzibar watujuze Tafadhari kulikoni, katika siku njema kama hii ya Christmas.

NOTE:
Ujumbe Mkuu wa Kanisa La Roman Catholic katika Christmas ya mwaka huu 2012:
"UPENDO NA AMANI NDIO UJUMBE MKUMBWA WA SIKUKUU HIYO"

attachment.php

Picha kwa niaba ya Mwanajamii forum kwa ID ya Mchami


TAARIFA YA LEO TAREHE 26/12/2012 KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TUKIO:
Father Ambros Mkenda wa Parokia ya Mpendae katika Kanisa Katoliki Mjini Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake majira ya saa 12 jioni wakati akitokea kanisani

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma Mohammed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema Father amepigwa risasi na ameumizwa sehemu ya kichwa na amekuwa akitoka damu nyingi kichwani na tayari anapatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.

Alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wahusika walifanya uhalifu huo kwa madhumuni gani kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Sisi tunahesabu kuwa kitendo hiki ni kitendo cha kihalifu na tunawatafuta wahalifu waliofanya kitendo hiki kwa hivyo bado ni mapema kusema kwamba kitendo hiki kimefanywa na nani kwa kuwa bado uchunguzi wetu unaendelea na hadi sasa hakuna mtu tuliyemshika kuhusikana na tukio hili” alisema Kamanda.

Kamanda Aziz akisimulia tukio hilo alisema walipata taarifa majira ya saa 2 na kwenda katika eneo la tukio ambapo Father alikuwa akitokea kanisani na kutaka kuelekea nyumbani kwake wakati akiwa ndani ya gari ndipo aliposhambuliwa na watu wasiojulikana na kuanguka.

“Tumekuta mabaki ya risasi ndani ya gari yake na katika vioo vyake vya gari vimevunjika na tumekuta damu chini pale” alisema Kamanda.

Aidha Kamanda Azizi alisema Father Ambros yeye ni mhasibu pale kanisani na hivyo mara nyingi watu wananaamini kwamba katika siku za krismass mara nyingi sadaka hukusanywa fedha nyingi na hivyo wanamini kwamba alikuwa fedha mikononi na ndipo inawezekana waliamua kumpiga risasi wakitaka kuchukua fedha hizo.

Hata hivyo alisema uchunguzi wa awali ndio utakaoeleza ni suala gani lililopelekea kupigwa risasi lakini wanaendelea na uchunguzi huo ambapo uchunguzi ndio utakaojulikana sababu kamili ya tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Askofu Michael Hafidh wa Kanisa la Anglikan la Mkunazini amesema wamesikitishwa na wamepokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo hasa kwa kuzingatia matukio kama hayo hayajawahi kutokea ya kuwahujumu viongozi wa dini.

Alisema tukio hilo ni miongoni mwa matukio ya kushtusha na yanaashiria hali mbaya ya kiusalama na kuwaomba viongozi wa serikali kuchukua hatua za tahadhari kubwa kwani matukio kama hayo yameanza kutokea kwa viongozi wa dini ambapo mwanzo ilianzia kwa Sheikh Soraga na baadae kutokea kwa Father Ambros.

“ Hii ni hali ya hatari katika nchi yetu na haipendezi lakini serikali lazima ijue sisi hatuwezi kujua wala hatuwezi kujilinda lakini serikali inapaswa kutulinda sisi ndio wananchi wake” alisema Askofu Hafidh.

Askofu Hafidh alisema hivi karibuni kumekuwepo vipeperushi vilivyosambazwa na watu vikiwatisha watu wenye imani ya kikristo ambapo alisema miongoni mwao walikuwa na khofu juu ya kusambazwa kwa vipeperushi hivyo na kuiomba serikali iongeze ulinzi.

“Tumeona hivi vipeperushi na kwa kweli tulikuwa na khofu juu ya vipeperushi hivi lakini ndio tunasema tunaelekea wapi katika maisha haya” alisema Akofu Hafidh.

“Sisi hatuamini kwamba kuna kisasi kwa viongozi wa dini lakini tunachukulia hilo ni tukio la kihalifu na pia hatuna vipeperushi vya aina yoyote vinavyoelezea kuwatisha viongozi wa dini kwa hivyo tunachukulia hayo ni matukio ya kihalifu na wala hatuamini kwamba matukio haya ni ya dini fulani” alisema Kamanda Azizi.

Akielezea kuhusiana na hilo Kamanda Aziz alisema jeshi la polisi limejipanga na kuzidisha ulinzi katika maeneo yote ya makanisa ambapo kumesambazwa polisi wa kutosha kwa kuwa wanajua wakati wa sherehe mambo ya kihalifu hujitokeza.

“Sisi kawaida huwa tunaweka ulinzi siku za sherehe zozote lakini kwanza makanisa yote yamewekwa ulinzi wa kutosha kabisa lakini wahalifu wanapotaka kufanya uhalifu huwezi kujua watatumia mbinu gani na saa ngapi na watafanya uhalifu huo wapi, lakini ulinzi upo wa kutosha” alisisitiza Kamanda Aziz.
 

Attachments

  • 12-25-2012 10-55-10 PM.jpg
    12-25-2012 10-55-10 PM.jpg
    31.4 KB · Views: 5,476
Mambo ya Kulea watu na kumuambia macho uchokozi wa kidini, Rwanda hiyo inakuja Tanzania Mungu epusha janga hili linalonyemelea Tanzania
 
Oooh my god! R.I.P!

TUMBIRI (Upanga, Dar es Salaam - Tanzania),
tumbiri@jamiiforums.com

Mkuu Pasco na wadau wote wa JF,
Nilisoma thread haraka haraka na wakati na-comment nilijua tayari ameshakufa. After all hata heading ya thread nayo haijakaa vizuri. Is better mods wangeirekebisha na kuwa "Padri ajeruhiwa kwa risasi" kuliko ilivyo hivi sasa.

TUMBIRI (Upanga, Dar es Salaam - Tanzania),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Hiyo risasi imemjeruhi au ni vipi?
Kwa Mujibu wa Mtangaji Faruku Karim, inasemekana hali yake sio nzuri na amekimbizwa hospitalini huku wakiangalia kama kuna uwezekano wa kumleta Tanzania Bara.
 
Oooh my god! R.I.P!

TUMBIRI (Upanga, Dar es Salaam - Tanzania),
tumbiri@jamiiforums.com
Hajathibitishwa kama kafa ila hali yake ni mbaya wanampango wa kumleta Tanzania bara kwa matibabu zaidi.Tumuombee apate aueni,kwa kuwa tendo hilo katika kipindi kama hiki hata kama ni wezi, basi target ni mbaya na ina ishara mbaya.
 
Labda kama ni maandishi mybe i wasnt paying attention.ila kwasasa sioni maandishi na tamthilia a woman of steel ndo iko hewani.
Na ninajua kama ni maandishi hawaweki jina la repota.sasa mtu anajuaje kuwa ni farid ndo karipoti.?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom