Zanzibar ni bomu linalosubiri kulipuka, Watawala mkifanya kiburi halitoiacha nchi salama

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,090
Kwa vyovyote vile Wazanzibari ni dhahiri wameshaamua lolote na liwe, ukisikia kauli za watu wa Zanzibar, vijana hata wazee wanaonyesha hawajali tena na roho zao zimeshakinai na wako tayari kwa lolote!.

Zanzibar ya safari hii pengine ni Zanzibar iliyo bitter (uchungu) kuliko Zanzibar ya wakati wowote tangu mapinduzi ya mwaka 1964. Wananchi wamejiapiza kusimama kulinda haki yao ya kuchagua kiongozi wamtakaye, Wamejiapiza hadi ikibidi kufa!. Haya si maneno yangu ni maneno ya wazanzibari wengi wanaongea haya bila kificho. Uongozi mzima chini ya Maalim Seif wameshatoa kauli zao kuwa wako tayari kwa lolote!

Sasa fukuto hili si la kawaida, Kama kuna watu wana akili ndani ya System, serikali na chama tawala inabidi sasa watulize akili badala ya maguvu!
Kuna haya mambo yafuatayo

1. Hatima ya muungano itategemea serikali itahandle vipi suala la uchaguzi wa Zanzibar

Mkimwaga damu hata ya watu kumi tu, hiyo ni death warrant ya muungano wenyewe!. Wazanzibar sasa badala ya kutaka muungano uliofair, Wataukataa kabisa hata muungano wenyewe. Na kiukweli hakuna atakayeweza kuulazimisha uwepo kama maelfu ya Wazanzibari wataingia mtaani non-stop kuukataa muungano wenyewe. Utaua wangapi kisha dunia ikuangalie tu?
Tendeni haki ili hiyo haki iwe kinga ya kuulinda muungano, Nje ya haki hakuna Muungano, Maana Wazanzibar watauona kama chombo cha ukoloni dhidi yao na wataukataa. Watawala fikirieni sana juu ya hili!

2. Uchaguzi huu wa Zanzibar inaweza kuwa sababu ya watu kufikishwa the Hague

Iwapo damu ya Mzanzibar itamwagika, hakuna atakayebaki salama kwa watakaohusika, wanaweza kujikuta mahali pagumu sana kisheria. Safari hii ni tofauti na zamani ambapo ilikuwa ni rahisi kuficha matukio kutokana na tekinojia ya mawasiliano kutokuwa imeendelea sana kuliko leo. Lakini kwa dunia ya leo chochote kitakachofanyika leo dakika hiyohiyo dunia itaona dhahiri. Sasa watoa amri na wenye mamlaka wachague moja, watoe haki kwa wananchi wa Zanzibar au wao wakatetee haki yao ya kuwa huru mbele ya mahakama ya uhalifu dhidi ya binadamu huko the Hague

3. Uwezo wa kutawala kwa serikali ijayo ya Zanzibar itategemea sana na jinsi watawala wa sasa watakavyohandle uchaguzi huu

Iwapo kutatokea sintofahamu katika uchaguzi huu hadi kupelekea kumwaga damu yoyote ya mwananchi wa Zanzibar, basi serikali itakayoundwa huko Zanzibar kama ni ya CCM, kamwe haitokuwa na uhalali mbele ya wananchi wa Zanzibar, wataidharau. Serikali hiyo itatafuta legitimacy zaidi kwa watawala wa bara kuliko wananchi wa Zanzibar. Itakuwa serikali isiyojiamini, ya kinyapara tu na kamwe haitoleta maendeleo yoyote ya maana kwa Wazanzibari. Kwa hivyo itakuwa serikali mzigo kwa Tanganyika maana itakuwa ni tegemezi zaidi kwa Tanganyika. Hii kitu itaathiri pia hata uchumi wa Tanganyika maana itabidi iingie hazina kuisaidia serikali hiyo ya SMZ kwa sababu serikali hiyo itakuwa hohehahe zaidi

4. Utalii unaweza kushuka sana na uchumi kuyumba sana

Iwapo kutatokea sintofahamu huko hadi maisha ya wananchi kupotea, kutatoea publicity mbaya sana kwenye media, hii itaathiri sana utalii wa Zanzibar. Hii itaathiri uchumi wa Zanzibar, na maisha kuendelea kuwa magumu sana. Kama nilivyoeleza kwenye nukta ya tatu, Tanganyika nd italazimika kuingilia kati kuinusuru Zanzibar kifedha. Hii itapelekea miradi mingi huku Tanganyika isimame etc

5. Kwako mkuu wa Majeshi, kwa unyenyekevu mkubwa, Mission ya Zanzibar ni ya kisiasa siyo ya kijeshi, usije ukalitia jeshi la wananchi lawama ya bure sababu ya wachache tu wanaotafuta shortcut ya Madaraka baada ya kukataliwa na wananchi. Jeshi haliwezi kushinda mission ya kisiasa mbele ya watu walio determined

Miaka mitatu iliyopita tuliandika hapa JF kuwa mission ya korosho kule mikoa ya kusini ni mission ya kiutawala siyo ya kijeshi, na kwamba Jeshi kujiingiza katika mission hiyo ni kulitafutia lawama tu kwa sababu biashara ya korosho si kazi yake,na halitoiweza, na ilitokea hivyo

Pia ningependa nimwambie CDF kuwa, hali iliyopo Zanzibar ni hali ya kisiasa tu, kwamba kuna watu wamezidiwa kisiasa wanataka kutumia majeshi kukaa madarakani. Sasa ni uamuzi wa CDF, kuamua jeshi litumike kwa ajili ya CCM au liwe Neutral liache wanasiasa wachuane wenyewe kwa wenyewe na lenyewe lilinde mipaka na katiba ya nchi. Uchaguzi wa Zanzibar ni issue ya kisiasa, Kupeleka Jeshi kule na kupitisha vifaru mitaani ni kuescalate tensions tu. kwani, unawezaje kwa mfano kutumia kifaru dhidi ya raia wako mwenyewe?.
Ni hatari kwa nchi iwapo Wanzanzibar wataiona JW kama occupying force!. Kwamba ipo ili kupora maamuzi yao ya kisiasa!. Jeshi lisimame imara kwenye kipindi critical kama hiki, lisiwachekee wanasiasa hata kidogo, liwe wazi na liseme kuwaambia watawala kuwa Hatukupewa silaha na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzigeuza silaha hizo kwao

Kwa hiyo kwa kuhitimisha ni kwamba kutokutenda haki Zanzibar kutauua hata Muungano wenyewe at one point in time.
Haki ndo njia pekee ya kuinusuru Zanzibar na muungano.
 
wanangu wa kangagani wananiambia ama wamkabidhi nchi maalim au vituo vya polisi wete na chake viwe magofu! They are now in possession of handgrenades (8 in number ), successful imported from shimoni
Sasa huko mbona zile mashine ndo zawatazama kwenye nyuso zao?
 
Wanadhani wako juu ya sheria hivyo wanaweza kutia vilema, kuumiza na hata kuwaua Watanzania wasio na hatia na wakaendelea kupeta tu kama vile hakuna kilichotokea. Safari hii itawatokea puani au kwenye tundu lolote kwenye miili yao.
 
Nyie tuuweni tu. Hatuna hata fimbo. Mna vifaru, bunduki, ndege za kivita... Fanyeni itakavyowapendeza tu. Siku ya kwanza mtaua 20, kesho yake pia tutakuja barabarani... Mkiua tunazikana ama tunazikwa. Wanaobaki wanaendelea. Kitaeleweka tu.

Hata I dd Ammin hakuuwa Waganda wote. Aliua alioua, waliobaki walibaki.
Andamana tu ili upate zawadi yako
 
Nyie tuuweni tu. Hatuna hata fimbo. Siku ya kwanza mtaua 20, kesho yake pia tutakuja barabarani... Mkiua tunazika ama tunazikwa. Wanaobaki wanaendelea. Kitaeleweka tu. Hata I dd Ammin hakuuwa Waganda wote. Aliua alioua, waliobaki walibaki.
Hakuna raia yoyote ambae atathubutu kuandamana.

Uchaguzi utakuwa na utulivu kuliko unavyofikiria.

Watanzania hawana desturi ya kupenda vurugu za kijinga.

Ila polisi wapo tayari kwa vurugu na chochokocho zitakazojitokeza wakati wa kupiga kura na baada ya shughuli hiyo kukamilika.

Mimi nipo hapa Kijitoupele Stone Town naona hali ni shwari kabisa.
 
Uwezo wa kutawala kwa serikali ijayo ya Zanzibar itategemea sana na jinsi watawala wa sasa watakavyohandle uchaguzi huu
Watatawala kwa mabavu ya bara kama ilivyokuwa kwa Dr. Shein baada ya Jecha kufanya yake.
Hatima ya muungano itategemea serikali itahandle vipi suala la uchaguzi wa Zanzibar
Watalqzimishwa na mabavu ya bara. Jeshi toka bara litapiga kambi huko.
 
Ma-CCM wote akiwemo Magufuli ndio mawazo yao haya. Eti unaweza waingizia Watanzania kidole kwenye makalio wakakuchekea tu. Huwa kuna mwisho wale.

Na mwisho ni 2020. Tuombe uzima siku 2-3 hizi. Udhalimu ungekuwa hauna mwisho, Wazungu leo wangekuwa bado wako Afrika hii.

Walitawala makarne na makarne, lakini mwisho ulifika. Hivyo hivyo na udhalimu wa CCM, una mwisho wake. Tena inatakiwa ipigwe marufuku kabisa wanachama wake watafute vyama vingine kama wanataka kufanya siasa.
Hakuna raia yoyote ambae atathubutu kuandamana.

Uchaguzi utakuwa na utulivu kuliko unavyofikiria.

Watanzania hawana desturi ya kupenda vurugu za kijinga.

Ila polisi wapo tayari kwa vurugu na chochokocho zitakazojitokeza wakati wa kupiga kura na baada ya shughuli hiyo kukamilika.

Mimi nipo hapa Kijitoupele naona hali ni shwari kabisa.
 
Watatawala kwa mabavu ya bara kama ilivyokuwa kwa Dr. Shein baada ya Jecha kufanya yake.

Watalqzimishwa na mabavu ya bara. Jeshi toka bara litapiga kambi huko.
Jee hao wanajeshi watawalinda ccm wanao kaa mitaani maana mm mdogo wangu au mjomba wangu akiuliwa mm nitadili na ccm aliyeko mtaani kwangu

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Ma-CCM wote akiwemo Magufuli ndio mawazo yao haya. Eti unaweza waingizia Watanzania kidole kwenye makalio wakakuchekea tu. Huwa kuna mwisho wale. Na mwisho ni 2020. Tuombe uzima siku 2-3 hizi.
Watanzania safari hii watamfundisha Tundu Lissu somo muhimu sana la kihistoria kwa kumpa kura zote raisi John Magufuli.

Litakuwa si fundisho kwa Tundu Lissu pekee bali hata kwa bosi wake Bob Amsterdam, washirika wao wote na wale wote wasoitakia mema Tanzania.

Baada ya JPM kutangazwa mshindi kwa kishindo tutangojea aapishwe rasmi na kisha kuhutubia Bunge la JMT ambalo safari hii litakuwa limesheheni wabunge karibu wote kutoka CCM.

Tukimaliza hilo twaendelea na maisha.
 
Back
Top Bottom