Zanzibar: Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Mhe Ali Hussein amesema Serikali ya awamu ya nane imedhamiria kuona sekta ya elimu inaendelea kupiga hatua

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
733
475
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein amesema awamu ya nane imedhamiria kuona sekta ya Elimu inaendelea kupiga hatua kwa kuendelea kupunguza changamoto mbalimbali.

Amesema hayo wakati akifungua kongamano la kitaaluma la siku moja Katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Kampasi ya Maruhubi Mkoa wa Mjini Unguja.

Amesema Serikali inaendelea kuboresha miundo mbinu ya kielimu na pamoja na maslahi ya walimu ili Elimu ipatikane Katika mazingira mazuri na salama.

Amesema historia inaonesha Elimu hapo awali ilipatikana kwa matabaka lakini baada ya Mapinduzi Elimu ni haki ya lazima kwa kila mtu kuipata.

Hivyo ameeleza kuwa ili wananchi waitumie haki ya kupata Elimu ni vyema kuimarisha miundo mbinu yote ya kielimu ili kufikia malengo ya Taifa ya kuzalisha wataalam wazalendo kupitia fani mbalimbali.

Nae Mkurugenzi Idara ya michezo Wizara ya Elimu Zanzibar bwana Ahmed Abdallah Mussa amesema uwepo wa kongamano la kitaaluma ni kuhakikisha jamii inapata kujua historia ya Elimu ilivyoanzia na kuona jinsi inavyoendelea kwa kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake ya kuelimika.

Nao washiriki wa kongamano hilo wamesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi kupunguza baadhi ya changamoto lakini Bado wameiomba wizara ya Elimu kuajiri watu wa ushauri Nasaha kwa kila Skuli kwani Wanafunzi wengi wanaonekana kukosa uwezo wa kufanya vizur kutokana na msongo wa mawazo.

Kongamano hilo la kitaaluma ni miongoni mwa shamra shamra za kuelekea kilele Cha miaka 58 ya tamasha la Elimu bila ya malipo ambapo huadhumishwa kila mwaka ifikapo Tarehe 23 September.View attachment 2360193View attachment 2360192
IMG-20220918-WA0008.jpg
 
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein amesema awamu ya nane imedhamiria kuona sekta ya Elimu inaendelea kupiga hatua kwa kuendelea kupunguza changamoto mbalimbali.

Amesema hayo wakati akifungua kongamano la kitaaluma la siku moja Katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Kampasi ya Maruhubi Mkoa wa Mjini Unguja.

Amesema Serikali inaendelea kuboresha miundo mbinu ya kielimu na pamoja na maslahi ya walimu ili Elimu ipatikane Katika mazingira mazuri na salama.

Amesema historia inaonesha Elimu hapo awali ilipatikana kwa matabaka lakini baada ya Mapinduzi Elimu ni haki ya lazima kwa kila mtu kuipata.

Hivyo ameeleza kuwa ili wananchi waitumie haki ya kupata Elimu ni vyema kuimarisha miundo mbinu yote ya kielimu ili kufikia malengo ya Taifa ya kuzalisha wataalam wazalendo kupitia fani mbalimbali.

Nae Mkurugenzi Idara ya michezo Wizara ya Elimu Zanzibar bwana Ahmed Abdallah Mussa amesema uwepo wa kongamano la kitaaluma ni kuhakikisha jamii inapata kujua historia ya Elimu ilivyoanzia na kuona jinsi inavyoendelea kwa kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake ya kuelimika.

Nao washiriki wa kongamano hilo wamesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi kupunguza baadhi ya changamoto lakini Bado wameiomba wizara ya Elimu kuajiri watu wa ushauri Nasaha kwa kila Skuli kwani Wanafunzi wengi wanaonekana kukosa uwezo wa kufanya vizur kutokana na msongo wa mawazo.

Kongamano hilo la kitaaluma ni miongoni mwa shamra shamra za kuelekea kilele Cha miaka 58 ya tamasha la Elimu bila ya malipo ambapo huadhumishwa kila mwaka ifikapo Tarehe 23 September.View attachment 2360193View attachment 2360192View attachment 2360194
Nilipoona serikali ya awamu ya nAne nikashtuka kidogo mbele ya serikali ya zanzibar hata sisi tuna wakimbiza sasa awamu ya sita
 
Back
Top Bottom