Zanzibar 2020 Zanzibar nafasi yetu katika Muungano inachezewa

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,866
Vyama vyote na wagombea wote wa Urais katika uchaguzi wa mwaka huu wanatoka bara. Nafasi tuliyopewa kwa upande wa Z'bar ni ‘mugombea mwenza’.

Je, ni kweli kwamba Wazanzibari hatustahili kushika nafasi ya urais wa Tanzania? Haya ndo makosa ya kikatiba. Z’bar tuna nafasi ya rais wetu na hakuna mtu wa bara anaweza kushika nafasi hiyo.

Hata hivyo mgombea urais wa Z’bar, tunajua anavyopatikana huko bara. Lakini pia kuna nafasi ya Waziri Mkuu wa Serikali ya muungano ambayo miaka yote ni ya mtu wa bara.

Baada ya Mwinyi kuwa rais wa muungano, imeshindikana kabisa kuwa na mgombea urais toka Z’bar. Hili siyo tatizo la CCM ni tatizo la Tanganyika na Z'bar maana hata vyama vya upinzani sioni chama kilichomuweka M-Z’bari kugombea urais wa muungano. Kwa ujumla nafasi ya Z’bar ktk muungano inachezewa.
 
Mnaposubiri kupewa hilo ni tatizo mnatakiwa kujipanga ili mchukue hata hao wa bara sio km wanapewa wanajijenga kimakund wanaweka mikakati thabiti mwishowe kundi mojawapo linachukua nafas kund lililoshindwa linajipanga ref; 95 kund lililoshindwa walijipanga wakakwanyua 05 lakini walioshindwa na tano nao wakajipanga ndio hawa wanaotusomesha namb now lkn km mnasubir kupewa endeleeni kupiga dua na visimamo vya usiku labda Mungu atawafanyia shufaa.
 
Tatizo ni kuambiwa lazima kila chama kiwe na mgombea bara na visiwani. Mbona vyama vyote wagombea wanatoka bara?
 
Zanzibar siyo nchi. Pinda ashasema haya kitambo Sana. Huu ndiyo ukweli japo mchungu Sana.
 
Waziri mkuu wa serikali ya muungano ni kama ceremonial president wa Jamhuri ya watu wa Tanganyika.
 
..TL yuko Zanzibar leo...nina hakika ataudadavua muungano, na kupendekeza njia bora za kutatua changamoto zake.
 
Huu ndio uchaguzi wa mwisho kuhusu hatma ya zanzibar, tundu lissu alisema zanzibar ipo kama koloni la tanganyika, wanaminywa haki nyingi....

Wajinga watasubiri mpaka amani itoweke wapigane kama sudani ndo washughulikie muungano,

Wenye akili watajadili ni njia gani bora ya kugawanyisha muungano......

Huyo ndo tundu lisu kiboko ya mkoroni mweusi
 
Hakuna aliyewastua wazenj kama Mtikila (RIP). Tena Mtikila alikuwa na akili kuliko huyu anayepiga kelele kila kona: Maongezi ya Mtikila kila mtu alisema naam!
 
Vyama vyote na wagombea wote wa Urais katika uchaguzi wa mwaka huu wanatoka bara. Nafasi tuliyopewa kwa upande wa Z'bar ni ‘mugombea mwenza’.

Je, ni kweli kwamba Wazanzibari hatustahili kushika nafasi ya urais wa Tanzania? Haya ndo makosa ya kikatiba. Z’bar tuna nafasi ya rais wetu na hakuna mtu wa bara anaweza kushika nafasi hiyo.

Hata hivyo mgombea urais wa Z’bar, tunajua anavyopatikana huko bara. Lakini pia kuna nafasi ya Waziri Mkuu wa Serikali ya muungano ambayo miaka yote ni ya mtu wa bara.

Baada ya Mwinyi kuwa rais wa muungano, imeshindikana kabisa kuwa na mgombea urais toka Z’bar. Hili siyo tatizo la CCM ni tatizo la Tanganyika na Z'bar maana hata vyama vya upinzani sioni chama kilichomuweka M-Z’bari kugombea urais wa muungano. Kwa ujumla nafasi ya Z’bar ktk muungano inachezewa.

Zanzibar mnakosea wapi? Mtachaguliwa Rais Dodoma mpaka lini? Mbona hamjiongezi?
 
Hakuna aliyewastua wazenj kama Mtikila (RIP). Tena Mtikila alikuwa na akili kuliko huyu anayepiga kelele kila kona: Maongezi ya Mtikila kila mtu alisema naam!
Nyie wanafiki tu. Wakati Mtikila akiwepo mbona mlimuona msaliti?
 
Back
Top Bottom