Zanzibar na China zasaini mkataba wa mashirikiano ya kiuchumi na kiufundi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar na China zasaini mkataba wa mashirikiano ya kiuchumi na kiufundi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Sep 7, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=3]Zanzibar na China zasaini mkataba wa mashirikiano ya kiuchumi na kiufundi[/h]

  [​IMG]
  Waziri wa Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Omar Yussuf Mzee,kwa Upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitiliana saini Mkataba wa Mashirikiano ya Kiuchumi na
  Kiufundi,na Naibu Waziri wa Biashara wa China ZHONG SHAN,kwa Upande wa jamhuri ya Watu wa China,katika mashirikiano hayo Zanzibar itapatiwa RMB 60 Milioni sawa na Fedha za Tanzania 14,8 Bilioni,ambapo fedha hizi ziatatumika katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.
  {Picha na Ramadhan Othman Ikulu.}
  [​IMG]
  Waziri wa Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Omar Yussuf Mzee,kwa Upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akibadilishana Mikataba baada ya kutiana saini Mashirikiano ya
  Kiuchumi na Kiufundi,na Naibu Waziri wa Biashara wa China ZHONG SHAN,kwa Upande wa jamhuri ya Watu wa China,katika mashirikiano hayo Zanzibar itapatiwa RMB 60 Milioni sawa na Fedha za Tanzania 14,8 Bilioni,ambapo fedha hizi ziatatumika katika kutekeleza miradi mbali
  mbali ya maendeleo. {Picha na Ramadhan Othman Ikulu.}


  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China leo zimetiliana saini Mkataba juu ya Mashirikiano ya Kiuchumi na Kiufundi ambapo Zanzibar itapatiwa jumla ya RMB 60 Millioni sawa na TZS,14.8 BILLIONI.

  Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Waziri wa Nchi Fedha ,Uchumi na Mipango ya Maendelro Omar Yussuf Mzee ndie alietia saini na kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Naibu Waziri wa Biashara Zhong Shan ndie alietiana saini ambapo ulishuhudiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sief Ali Idd na kwa upande wa China Naibu Waziri Mkuu wa nchi Hui Liangyu.

  Kwa mujibu wa Mkataba huo wa Mashirikiano Zanzibar itafaidika katika Ujenzi wa Majengo mapya na Ukarabati mkubwa wa Majengo yaliopo katika Hospitali ya Abdulla Mzee ..Pia Ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Mwananakwerekwe.Halkadhalika Zanzibar itafaidika katika utiaji wa Taa za Barabarani zitakazotumia Nishati ya jua katika baadhi ya Barabara kuu za Mjini.

  Aidha Mkataba huo unaelezea kuwa Zanzibar itapata Mafunzo Mafupi na Marefu katika Fani tofauti ambayo itapendekezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar . Mbali na hayo pia kutakuwapo Uchimbaji wa Visima vya Maji pamoja na maeneo mengine ambayo Nchi mbili zitakubaliana.

  Pia ujumbe huo wa China umetiliana saini na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya msaada wa Wataalamu wanne(4) kutoka China ambao watakuwepo Zanzibar kwa miaka miwili(2) ambao watawafundisha Mafundi wa Mitambo wa Studio yakurushia matangazo ya Redio pamoja na kutoa Vifaa mbali mbali kwa ajili ya Studio hiyo.

  Ujumbe huo wa China ukiongozwa na Naibu Waziri Mkuu uliwasili Zanzibar leo jioni na kupokelewa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwamo Mawaziri. Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu pamoja na maofisa mbali mbali wa Serikali.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein jioni hiyo hiyo alikuwa na Mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa China Hui Liangyu Ikulu ambapo walizungumzia juu ya Ushirikiano kati ya Nchi zao.

  Usiku huu Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Amemuandalia Chakula Naibu Waziri Mkuu wa China pamoja na ujumbe wake huko katika hoteli ya Lagemma Nungwi.

  Kesho asubuhi Naibu Waziri Mkuu wa China na ujumbe wake watatembelea kanisa la Anglican Mkunazini na baadae kuelekea Beit el Ajaib na Jumba la Wananachi Forodhani na kuelekea Uwanja wa ndege kwa kurejea Dar es Slaam.

  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
   
 2. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Tulizowshaa Wazanzibar kuwa kila kitu cha nje ya Zanzibar ni Muungano lazima tuombe izini kutoka Tanganyika ijitayo Tanzania.

  Hii yote ilikuwa ni wenzetu kututawala kimpinu na kutuona ma-foolish hivi sasa baada ya vuguvugu la Wazanzibar kuukataa Muungano ndio wakoloni no2 wanajaribu kulegeza badhi ya vitu.
   
 3. mzalendokimathi

  mzalendokimathi Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tutafanikiwa tu Mungu akipenda hata kama watanganyika hawataki,,washenzi wakubwa wale
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,068
  Trophy Points: 280
  ..mkiwa nje ya muungano mtayakosa yote hayo.

  ..ndugu zenu wa Comoro wanatupigia magoti tuungane nao, nyinyi mnaleta kiburi na nyodo.

  ..halafu linganisha hiyo pesa aliyowapa Wachina na mapesa mnayopewa na wa-Tanganyika.

  ..Tanganyika tumekupeni bilioni 32, wakati China wamewapa bilion 14.8.
   
 5. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Itakuweje Tanzania wakisign makataba na Tibet?Taiwan?Au Hong Kong? au hata tumkaribishe Dalai Lama? ,...Our dearest friend china.Sijui itakuweje na Israel wakisign mkataba na zanzibar wa mambo ya ulinzi na mengine kama tunavyojituma kwa wapalestina,ila tumetosha Dalai Lama
   
 6. b

  bin rasshid Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  miungoni mwa wajinga wewe ni namba moja kabla ya muungano tulikosa nini ,wakomoro wanataka muungano sio dhulma na hizo pesa za tanganyika ni mnazotupa ni za wizi mnatuibia pesa chungu mzima halamnatujejea kwa kurudisha kimtindo hapa hatuungana mmetudhulum kwa tanganyika kuita tanzania na mengine yakafuata nchi yenu ina washinda halafu mnatka muungano mkomora yupi anataka muungano nawezi nyie mdanganya mwengine simzanzibar puu.
   
 7. Root

  Root JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,295
  Likes Received: 13,004
  Trophy Points: 280
  Oooh mi naona sasa ni wakati wa hii nchi kuanza jitegemea yenyewe

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hongereni sana. Mwendo mdundo sasa.

  hakuna kulala mpaka kieleweke.

  Mvungano mwisho Chumbe.
   
Loading...