Zanzibar: Mwili wa Mbunge, Marehemu Khatib umezikwa katika kijiji cha Shumba Mjini, Wilaya ya Micheweni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amewanasihi ndugu wa Marehemu Khatib Said Haji kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa kuondokewa na kipenzi chao, wakijuwa kuwa ndugu yao huyo ameondoka akiwa ametimiza wajibu mkubwa kwa nchi na jamii yake.

Marehemu Khatib, aliyefariki dunia jijini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa, alikuwa mbunge wa jimbo la Konde kisiwani Pemba kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar aliyehudhuria mazishi ya Mbunge huyo, alikutana na familia ya Marehemu kijijini kwao Konde Majenzi, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

"Najua ni vigumu kuyapokea yaliyotokea, lakini nawaomba sana muwe na subira katika kipindi hiki kigumu. Msiba huu umewagusa wengi, kwani Marehemu Khatib alikuwa mtetezi wa wanyonge na mtu wa kusisitiza haki kutendeka. Siku zote ameishi katika ukweli na uwazi, jambo ambalo limemjengea umaarufu na mapenzi makubwa kwa wanajamii,” alisema.

Aidha Mheshimiwa Othman alipeleka salamu za pole kwa familia hiyo kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

"Mheshimiwa Rais anawapa pole. Sote kwa pamoja tumeguswa sana na msiba huu na tunamtakia ndugu yetu safari njema,” alisema.

Alhaj Othman amewaambia wanafamilia hao kwamba japokuwa ni vigumu kuzuia hisia za huzuni, lakini kilichotokea ni wajibu wa kila mwanaadamu. “Jukumu letu kubwa lililosalia kwake sasa ni kumuombea dua ili zimfae huko aendako.”

Marehemu Khatib amezikwa katika kijiji cha Shumba Mjini, Wilaya ya Micheweni, kisiwani Pemba.

Marehemu Khatib ameacha kizuka na watoto sita.

Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tunarejea.

1621574529695.png


1621574541772.png

1621574554637.png

1621574567626.png
 
Back
Top Bottom