Zanzibar: Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima afungiwa kwa miezi sita baada ya kusambaza taarifa za mgonjwa wa Corona bila ruhusa

Samwel Ngulinzira,
Sasa hizi sheria zipo kwa watu baadhi,kwa sababu mkuu wa mkoa wa dar alitangaza na hakuna sheria yeyote iliyofuatwa.na huyo muandishi hakutaja majina yeye kataja idadi.
 
Sasa hizi sheria zipo kwa watu baadhi,kwa sababu mkuu wa mkoa wa dar alitangaza na hakuna sheria yeyote iliyofuatwa.na huyo muandishi hakutaja majina yeye kataja idadi.
Yeye mkuu wa mkoa ni mwandishi wa habari wa gazeti Gani? Maana mwandishi kafungiwa kufanya kazi za uanahabari basi tuseme na Makonda hatafanya kazi Za uandishi wa habari kwa muda flani sasa itakua na maana Labda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye mkuu wa mkoa ni mwandishi wa habari wa gazeti Gani? Maana mwandishi kafungiwa kufanya kazi za uanahabari basi tuseme na Makonda hatafanya kazi Za uandishi wa habari kwa muda flani sasa itakua na maana Labda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hatua angalii kazi ya mtu,tunaangalia kosa je mkuu wa mkoa alifanya kosa na sheria inasemaje.kama hajafanya kosa sawa ila kama kafanya.hii sheria ina fanya kazi kwa watu baadhi tu wengine haiwahusu.lile jambo angefanya mtu mwengine sasa hivi naona angekuwa segerea.
 
Kutoa taarifa ya mgonjwa bila ridhaa ya mgonjwa ni kosa, hii in kwa madaktari, wauguzi au mtu yeyote.
Kutoa taarifa ya kifedha ya mtu, kwa mfano kutangaza mtu fulani ana akiba ya shilingi flani au anadaiwa kiasi flani bila ridhaa ya mhusika ni kosa kisheria.
Kutoa taarifa ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi bila kumshirikisha mwanafunzi au mzazi ni kosa kisheria.
Kila taaluma ina miiko ya kazi.

Kwa hiyo mimi kama mwandishi wa habari baada ya kufanya utafiti juu ya mtu fulani anajipatia utajiri kwa njia zisizo za halali au ni mhujumu wa uchumi wa nchi na baada ya kupata ushahidi wa kutosha siruhusiwi kuandika habari hii?

Nitakuwa mkosa nikisema kutaja mali alizojikusanyia kutoka fedha, majumba au hata mashamba bila ya idhini yake?

Je ni kosa kuandika habari ya kiongozi wa dini au chama anaekwenda kinyume na maadili ya imani au ya chama chake bila ya idhini ya mhusika?
 
mtanzania in exile,
Nadhani hujanielewa vizuri.
Nachomaanisha ni ile taarifa ya kifedha ya mtu, suala la taarifa za uchunguzi ni jingine kabisa.
Hata ukienda benki kuangalia salio la akaunti ya mtu mwingine hawawezi kukupatia.

Nmewahi kwenda kumuangalizia mtu deni lake la ada ili nimlipie, kiukweli sikufanikiwa maana mhasibu alinambia mhusika lazima awepo physically au taarifa rasmi ya kuonesha kuwa katoa ridhaa ya kutoa taarifa ya deni lake.

Jaribu kujiuliza kwa nini hadi leo Zitto Kabwe hajataja majina ya walioficha pesa Uswiss wala kiwango cha pesa walichoficha.
 
Samwel Ngulinzira,
Naomba kuuliza hapo mgonjwa ni yupi? Ni yule ambaye yupo hospitali au yule anayejiuguza nyumbani? Nasema hivi kama huyo ndugu mkuu wa mkoa hasingemtaja hakika asingepelekwa hospitali na ingekuwa kizaazaa. Kwa nini wamfiche mgonjwa?
 
Back
Top Bottom