Zanzibar: Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima afungiwa kwa miezi sita baada ya kusambaza taarifa za mgonjwa wa Corona bila ruhusa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,367
2,000
Mwandishi wa Habari Talib Ussi Hamad wa Tanzania Daima amesimamishwa kufanya shughuli zote za Uandishi wa Habari kwa muda wa miezi 6 kuanzia leo baada ya kusambaza taarifa za Mgonjwa wa Coronavirus bila ridhaa yake

Kwa mujibu wa Kifungu cha 41, 42(a) n (b) cha Sheria ya Magazeti, Vitabu na Wakala wa Habari, Mwandishi huyo hatoruhusiwa kufanya shughuli yoyote ya Uandishi wa Habari katika kipindi hicho chote


1587382134474.png
 

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,531
2,000
Kwa hiyo alipata ridhaa ya familia? Mbona wanafamilia walimlalamikia kuwa hawakumtuma na wala yeye si msemaji wa familia.
Yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Kwa sababu walishatoa habari kama familia hakukuwa na ubaya namna alivyoliongelea lile suala.
 

MR. IBU

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
1,376
2,000
Kumbe kusema ukweli nalo ni kosa..hizi sheria zipo kwa baazi ya watu,wengine wakisema mnawa ogopa mnauchuna kimya.
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,774
2,000
Yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa. Kwa sababu walishatoa habari kama familia hakukuwa na ubaya namna alivyoliongelea lile suala.
Unafikiri ni kwanini sasa familia ililalamika? Halafu mbona hataji tena hao wagonjwa wengine? Kwani sasa hana uenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa?
 

carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
4,969
2,000
Tena alitakiwa awe jela kabisa..
Pamoja na bashite.
Huwezi kutoa taarifa za mgonjwa bila idhini yake halafu watu wakuchekee tu.

Privacy ya mgonjwa lazima iheshimiwe.
 

Samwel Ngulinzira

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
1,792
2,000
Kumbe kusema ukweli nalo ni kosa..hizi sheria zipo kwa baazi ya watu,wengine wakisema mnawa ogopa mnauchuna kimya.
Kutoa taarifa ya mgonjwa bila ridhaa ya mgonjwa ni kosa, hii in kwa madaktari, wauguzi au mtu yeyote.

Kutoa taarifa ya kifedha ya mtu, kwa mfano kutangaza mtu fulani ana akiba ya shilingi flani au anadaiwa kiasi flani bila ridhaa ya mhusika ni kosa kisheria.

Kutoa taarifa ya maendeleo ya kitaaluma ya mwanafunzi bila kumshirikisha mwanafunzi au mzazi ni kosa kisheria.

Kila taaluma ina miiko ya kazi.
 

mtanzania in exile

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
844
1,000
beth,
Duh sheria za wanahabari Tanzania ni za ajabu. Kwa hiyo kama muandishi wa habari akigundua kuna mtu, kwa mfano, anapokea rushwa, hatakiwi kuripoti bila idhini ya mhusika?

Naomba kuelimishwa. Pia ingelikuwa vizuri sana mkurugenzi wa idara ya habari angelinakili hicho kifungu cha sheria alichotumia ili umma ufahamu zaidi kilichojiri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom