Zanzibar: Mvunjaji Sheria, Criminal ni Shein na Genge Lake na Sio Seif

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Nimenyamaza Muda Nisikie Matamko Dhidi ya Shein aliyeiba Urais Wa Zanzibar kwa Uchaguzi haramu, Sijasikia condemnation nzito dhidi yake Zaidi ya Ile iliyotoka kwa Mh. Zitto Kabwe na Nampongeza sana. Namanisha Kauli ya Kumpinga Vikali Haini Shein kwa kujua wazi yeye Ndiye Mvunja Sheria halafu anatoa kauli za Kumtisha Seif, Mithili ya Anayenguruma kwa sauti ya Simba huku akiwa na Vimisuli vya Nguchiro, Maana anajua wenye nguvu ni wale waliomtuma.

Shein na CCM, Wanataka Kuihadaa Zanzibar, Tanzania nzima na Dunia Kuwa Dhuluma, Uhaini na Uharamia, walioufanya Kwa Kiburi Kikubwa Kufuta Matokeo ya Urais Zanzibar yalikuwa kwa Maalim Seif Peke yake na kwa Hiyo Wanataka KunaPesha Kuwa Anayeumia, na anayenungunika (Na Kwao huko ni Kuvunja sheria) Ni Seif peke yake.

Mimi Namwambia Shein, "The Criminal" kuwa, Ulipofanya Uhaini Kupora Urais Kwa Uchaguzi wa hadaa unajua Uliwaibia Wale wote waliopiga Kura Kwa Wingi sana Kukukataa wewe. Mbinu ya Kusema Kuwa ati Seif anauchu wa Madaraka, atakiona, Ni Kutaka kumtenga na Waliompigia Kura kwa Maelfu, Kwa Kujihadaa kuwa mlilofanya ni dogo na lilimhusu Seif peke yake.
Huyu Criminal Shein anasema kuwa ati Jinai haifutiki, Ndio ila Jinai Uliyofanya Shein Tena ukiwa kama Stooge wa waliokuagiza, Jinai yako ndio Haitafutika.

Naendelea Kusema Ulivyopa Urais wa Zanzibar wewe Pamoja na CCM hakuna Tofauti ya Majambazi waliokuwa wakivunja Milango kwa "Fatuma" Kuiba Redio Cassette player Miaka ile ya mwanzoni ya 1980

Kwa Kuhitimisha Niseme, CCM na Shein, Ninyi Ndio Wahalifu na Mnajua, Na Ukweli wa Pili Mlalamikaji na Mdhulumiwa Juu yenu sio Seif peke yake Ni Wanzibari Waliopiga Kura Kuwakataa Ninyi na Kumchagua Seif. Kusema Vingine ni Kuidanganya Dunia na Kujidanganya wenyewe.
 
Umeandika kwa hasira sana hebu jaribu kupitia huo msitari wa mwanzo kipengele cha mwisho kiko sawa au K inahitaji edit? Kama ulikusudia CCM Na Seif au CCM Na Shein?
 
Hivi wewe unaijua siasa ya Zanzibar au Unawehukwa tuu! Au unajaribu kumfananisha Seif na mwanasiasa mzalendo? You are wrong! this man will cost Tanzania and Zanzibar in particular! Hata hayati baba wa Taifa alimjua mapema huyu jamaa tangu zamani. So mfatilie historia ya maisha ya Seif Sharif Hamad ndani ya Siasa ndio utamjua Seif ni nani!
 
Asante, Nimeedit, Ila Nachukia sana, Uonevu, Unafiki wa wazi, Can you imagine mtu anakuja kwenye nyumba yako, anambaka Mkeo halafu anaitishia kuwa Ukiendelea Kunung'unika Kwanini ambake mkeo atakupiga na kukutia adabu kwa kuwa unachokifanya ni Uhalifu?
Unajionaje Ukiliona likibaka linamchomolea Mzee wa watu pale Manzese halafu hili likibaka ndilo linampigia huyu mzee kelele za mwizi ili yule aiyeibiwa achomwe tairi. Hili ndilo wanalofanya CCM, Na Shein, Ningekuwa na Uwezo wa Kubadilisha Jina la mtu Ningemwita Shame, Kwa kuwa hata kama alilzimishwa, Angeweza Kukataa.

Mimi ni Mkristo sijui Uislamu Unasemaje kila Kitu lakini naamini kwa Waislamu, Dhuluma, Unafiki na Uwongo Pia ni dhambi mbaya sana. Mimi Nilikuwa Makamu Mwenyekiti wa serikali ya Wanafunzi nikiwa Form II pale Azania, Niliopofika III Nikagombea Ukatibu mkuu wa Shule, Innosent Mwessiga Akagombea Uwenyekiti, na Katika Ukatibu nilikuwa Nikigombea Kijana aliyejulikana kama JOBAKA (Jonatha Baraka Kasesela) kwa Kifupi. Kwenye Kura alinishinda ingawa sio kwa Kura nyingi. Na kwa Kuwa Serikali niliyokuwepo bado ilikuwa haijaondoka, Nilikuwepo katika Kuhesabu Kura.

Waalimu akiwepo Mkuu wa Shule, Wakaniita wakaniambia Tutakutangaza wewe Kuwa Ndiye Katibu kwa Kuwa JOBAKA hajavaa Beji, na Uniform sawa sawa na Tunaona Wanafunzi wamempa Kura zaidi kwa kuwa ni genge lao. Niliwashukuru waalimu, ila niliwaambia, Namjua JOBAKA, hatufanani, ila Ni kijana anayeweza Kuongoza na Akiwa na Majukumu ana nidhamu nzuri. Niliongeza kuwa ingekuwa sivyo nisingewapotosha. Wakakubaliana na Mimi, JOBAKA alikuwa Katibu mzuri sana. Mimi nikawa mwanafunzi wa kawaida. Sasa Mimi Nimekuwa Loyal kutetea haki na Kweli kwa Matendo na Maneno. Somebody has to do it am sorry, And one day soon I will do it in a a more vocal and elaborate fashion.
 
Sio uedit tuu futa kabisa hiyo thread yako! and next time usifate mkumbo tuu! narudia tena kamsome Seif Sharif Hamad tangu enzi za hayati baba wa Taifa, siasa zake wakati wa Mzee Ali Hassan Mwinyi, Kipindi chake wakati wa Mkapa (hasa chanzo cha mauwaji Pemba na Unguja, na sababu za kuingiza Tanzania kwenye ramani ya nchi zilizowahi kuwa na wakimbizi ), siasa zake wakati wa Kikwete na kuibuka kwa Serekali ya Ummoja wa Kitaifa ( na kuwepo kwa serekali ya kitaifa kwa Kiongozi asie na utaifa zaidi ya uchu wa Uraisi)!
 
Asante, Nimeedit, Ila Nachukia sana, Uonevu, Unafiki wa wazi, Can you imagine mtu anakuja kwenye nyumba yako, anambaka Mkeo halafu anaitishia kuwa Ukiendelea Kunung'unika Kwanini ambake mkeo atakupiga na kukutia adabu kwa kuwa unachokifanya ni Uhalifu?
Unajionaje Ukiliona likibaka linamchomolea Mzee wa watu pale Manzese halafu hili likibaka ndilo linampigia huyu mzee kelele za mwizi ili yule aiyeibiwa achomwe tairi. Hili ndilo wanalofanya CCM, Na Shein, Ningekuwa na Uwezo wa Kubadilisha Jina la mtu Ningemwita Shame, Kwa kuwa hata kama alilzimishwa, Angeweza Kukataa. Mimi ni Mkristo sijui Uislamu Unasemaje kila Kitu lakini naamini kwa Waislamu, Dhuluma, Unafiki na Uwongo Pia ni dhambi mbaya sana. Mimi Nilikuwa Makamu Mwenyekiti wa serikali ya Wanafunzi nikiwa Form II pale Azania, Niliopofika III Nikagombea Ukatibu mkuu wa Shule, Innosent Mwessiga Akagombea Uwenyekiti, na Katika Ukatibu nilikuwa Nikigombea Kijana aliyejulikana kama JOBAKA (Jonatha Baraka Kasesela) kwa Kifupi. Kwenye Kura alinishinda ingawa sio kwa Kura nyingi. Na kwa Kuwa Serikali niliyokuwepo bado ilikuwa haijaondoka, Nilikuwepo katika Kuhesabu Kura. Waalimu akiwepo Mkuu wa Shule, Wakaniita wakaniambia Tutakutangaza wewe Kuwa Ndiye Katibu kwa Kuwa JOBAKA hajavaa Beji, na Uniform sawa sawa na Tunaona Wanafunzi wamempa Kura zaidi kwa kuwa ni genge lao. Niliwashukuru waalimu, ila niliwaambia, Namjua JOBAKA, hatufanani, ila Ni kijana anayeweza Kuongoza na Akiwa na Majukumu ana nidhamu nzuri. Niliongeza kuwa ingekuwa sivyo nisingewapotosha. Wakakubaliana na Mimi, JOBAKA alikuwa Katibu mzuri sana. Mimi nikawa mwanafunzi wa kawaida. Sasa Mimi Nimekuwa Loyal kutetea haki na Kweli kwa Matendo na Maneno. Somebody has to do it am sorry, And one day soon I will do it in a a more vocal and elaborate fashion.

wewe unaonekana mtata sana!! hah! unathubutu kuongea maneno makali kiasi hicho!
 
Mtoa mada umesema ukweli mtupu utafikiri na wewe ni mzungu maana ni wazungu tu ndiyo wamekemea kwa nguvu zote
 
Nimenyamaza Muda Nisikie Matamko Dhidi ya Shein aliyeiba Urais Wa Zanzibar kwa Uchaguzi haramu, Sijasikia condemnation nzito dhidi yake Zaidi ya Ile iliyotoka kwa Mh. Zitto Kabwe na Nampongeza sana. Namanisha Kauli ya Kumpinga Vikali Haini Shein kwa kujua wazi yeye Ndiye Mvunja Sheria halafu anatoa kauli za Kumtisha Seif, Mithili ya Anayenguruma kwa sauti ya Simba huku akiwa na Vimisuli vya Nguchiro, Maana anajua wenye nguvu ni wale waliomtuma.

Shein na CCM, Wanataka Kuihadaa Zanzibar, Tanzania nzima na Dunia Kuwa Dhuluma, Uhaini na Uharamia, walioufanya Kwa Kiburi Kikubwa Kufuta Matokeo ya Urais Zanzibar yalikuwa kwa Maalim Seif Peke yake na kwa Hiyo Wanataka KunaPesha Kuwa Anayeumia, na anayenungunika (Na Kwao huko ni Kuvunja sheria) Ni Seif peke yake.

Mimi Namwambia Shein, "The Criminal" kuwa, Ulipofanya Uhaini Kupora Urais Kwa Uchaguzi wa hadaa unajua Uliwaibia Wale wote waliopiga Kura Kwa Wingi sana Kukukataa wewe. Mbinu ya Kusema Kuwa ati Seif anauchu wa Madaraka, atakiona, Ni Kutaka kumtenga na Waliompigia Kura kwa Maelfu, Kwa Kujihadaa kuwa mlilofanya ni dogo na lilimhusu Seif peke yake.
Huyu Criminal Shein anasema kuwa ati Jinai haifutiki, Ndio ila Jinai Uliyofanya Shein Tena ukiwa kama Stooge wa waliokuagiza, Jinai yako ndio Haitafutika.

Naendelea Kusema Ulivyopa Urais wa Zanzibar wewe Pamoja na CCM hakuna Tofauti ya Majambazi waliokuwa wakivunja Milango kwa "Fatuma" Kuiba Redio Cassette player Miaka ile ya mwanzoni ya 1980

Kwa Kuhitimisha Niseme, CCM na Shein, Ninyi Ndio Wahalifu na Mnajua, Na Ukweli wa Pili Mlalamikaji na Mdhulumiwa Juu yenu sio Seif peke yake Ni Wanzibari Waliopiga Kura Kuwakataa Ninyi na Kumchagua Seif. Kusema Vingine ni Kuidanganya Dunia na Kujidanganya wenyewe.

Hivi ninyi CUF upuuzi mliofanya pemba wa kuvuruga uchaguzi mnaona sawa tuu isipokuwa marudio ni nongwa.sasa ngoja niwaeleze Zanzibar hamtatawala na mkileta vurugu mtadhibitiwa bora muondoke tuu muende huko mnakojifanya wakimbizi na kudai Tz inatawaliwa na wakristo.
 
Asante, Nimeedit, Ila Nachukia sana, Uonevu, Unafiki wa wazi, Can you imagine mtu anakuja kwenye nyumba yako, anambaka Mkeo halafu anaitishia kuwa Ukiendelea Kunung'unika Kwanini ambake mkeo atakupiga na kukutia adabu kwa kuwa unachokifanya ni Uhalifu?
Unajionaje Ukiliona likibaka linamchomolea Mzee wa watu pale Manzese halafu hili likibaka ndilo linampigia huyu mzee kelele za mwizi ili yule aiyeibiwa achomwe tairi. Hili ndilo wanalofanya CCM, Na Shein, Ningekuwa na Uwezo wa Kubadilisha Jina la mtu Ningemwita Shame, Kwa kuwa hata kama alilzimishwa, Angeweza Kukataa. Mimi ni Mkristo sijui Uislamu Unasemaje kila Kitu lakini naamini kwa Waislamu, Dhuluma, Unafiki na Uwongo Pia ni dhambi mbaya sana. Mimi Nilikuwa Makamu Mwenyekiti wa serikali ya Wanafunzi nikiwa Form II pale Azania, Niliopofika III Nikagombea Ukatibu mkuu wa Shule, Innosent Mwessiga Akagombea Uwenyekiti, na Katika Ukatibu nilikuwa Nikigombea Kijana aliyejulikana kama JOBAKA (Jonatha Baraka Kasesela) kwa Kifupi. Kwenye Kura alinishinda ingawa sio kwa Kura nyingi. Na kwa Kuwa Serikali niliyokuwepo bado ilikuwa haijaondoka, Nilikuwepo katika Kuhesabu Kura. Waalimu akiwepo Mkuu wa Shule, Wakaniita wakaniambia Tutakutangaza wewe Kuwa Ndiye Katibu kwa Kuwa JOBAKA hajavaa Beji, na Uniform sawa sawa na Tunaona Wanafunzi wamempa Kura zaidi kwa kuwa ni genge lao. Niliwashukuru waalimu, ila niliwaambia, Namjua JOBAKA, hatufanani, ila Ni kijana anayeweza Kuongoza na Akiwa na Majukumu ana nidhamu nzuri. Niliongeza kuwa ingekuwa sivyo nisingewapotosha. Wakakubaliana na Mimi, JOBAKA alikuwa Katibu mzuri sana. Mimi nikawa mwanafunzi wa kawaida. Sasa Mimi Nimekuwa Loyal kutetea haki na Kweli kwa Matendo na Maneno. Somebody has to do it am sorry, And one day soon I will do it in a a more vocal and elaborate fashion.

Kwanza nakupongeza kwa msimamo wako Na Mungu akuongoze zaidi kwakua dunia imejaa majaribio Na Sio jaribio. Ukija kwenye Dhulma Mkuu nakuhakikishia mwenye kudhulumu hawezi kumaliza maisha yake yote mpaka uzee akawa anatamba au Akabaki mwenye kuheshimiwa.
Mifano ipo mingi tunakataa kuifatilia wengi wanaona Ni mambo ya kisiasa tuu, au kimichezo au Ni Bahati mbaya ya maisha. Mungu Hana haraka Na mja wake, Majibu ya dhulma yapo hapahapa duniani. Ikiwa umewahi kutangulia Mbele ya haki unaowaacha nyuma yako, watoto Na urithi wako utaingia kwenye mitihani kwa kila chembe uliyoidhulumu.
 
Hivi wewe unaijua siasa ya Zanzibar au Unawehukwa tuu! Au unajaribu kumfananisha Seif na mwanasiasa mzalendo? You are wrong! this man will cost Tanzania and Zanzibar in particular! Hata hayati baba wa Taifa alimjua mapema huyu jamaa tangu zamani. So mfatilie historia ya maisha ya Seif Sharif Hamad ndani ya Siasa ndio utamjua Seif ni nani!
Mkuu, usibari topic; jamaa hajadiri uzuri au ubaya wa Shein au Maalim Seif; anacho jadiri ni nani aliyeshinda uchaguzi na nani aliyefanya jinai, is it Shein or Maalim Seif? Jikite hapo. Hayo mambo ya kutwambia sijui nani alijulikana na Mwalim hapa sio mahali pake, tengeneza Uzi tofauti na hu.
 
Hivi ninyi cuf upuuzi mliofanya pemba wa kuvuruga uchaguzi mnaona sawa tuu isipokuwa marudio ni nongwa.sasa ngoja niwaeleze zanzibar hamtatawala na mkileta vurugu mtadhibitiwa bora muondoke tuu muende huko mnakojifanya wakimbizi na kudai tz inatawaliwa na wakristo.
Kwani lini Dr. Shein amesilimu na kua muunguja? Mi najua hata yeye nae ni Mpemba na anatawala Zanzibar so sijaelewa hasa what is your point here!
 
you gays just leave alone siasa za Zanzibar! alie shinda urais ni Dr. Ali Mohamed Shein and anae ng'ang'ania urais kwa gharama hata ya kuwa fanya wananchi wa baguane, kwa machafuko na kumwaga damu ikibidi ni Seif Sharifu!
 
Sio uedit tuu futa kabisa hiyo thread yako! and next time usifate mkumbo tuu! narudia tena kamsome Seif Sharif Hamad tangu enzi za hayati baba wa Taifa, siasa zake wakati wa Mzee Ali Hassan Mwinyi, Kipindi chake wakati wa Mkapa (hasa chanzo cha mauwaji Pemba na Unguja, na sababu za kuingiza Tanzania kwenye ramani ya nchi zilizowahi kuwa na wakimbizi ), siasa zake wakati wa Kikwete na kuibuka kwa Serekali ya Ummoja wa Kitaifa ( na kuwepo kwa serekali ya kitaifa kwa Kiongozi asie na utaifa zaidi ya uchu wa Uraisi)!

Usimbebeshe tuhuma Mzee wa watu ,wewe sema ubaya wake acha vijimaneno maneno visivyo eleweka .Au unafikiri tumezaliwa juzi!?
 
Mkuu mimi sio kazi yangu kukupelekeni shule ya siasa za Zanzibar ila nakupeni Hints tuu, kama sio kilaza wa historia ya siasa ya Zanzibar (na hasa kumuhusu Seif Sharif na uchu wa Urais) then unaweza ukaelewa!
 
Mimi niulize uchu huu unakuja pale unaposhinda? Kwanini Serikali ilishindwa kumzuia Seif Kufanya siasa Tokea miaka ya 90, Kama Jumbe?
 
Back
Top Bottom