Zanzibar: Muswada wa utalii wapita kwa tabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar: Muswada wa utalii wapita kwa tabu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Apr 7, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Mswada wa sheria ya utalii jana umepita kwa tabu baada ya wajumbe kutofautiana juu ya mswada huo kuhusu suala la upendelezo la ajira kwa wazanzibari.

  Wakati wajumbe wasiokuwa mawaziri backbenchers wakitaka ajira katika sekta ya utalii ibaki kuwa ya wazanzibari kisheria, mawaziri wengi walitaka pendekezo la serikali kuwa ni ajira iwe ni ya mtanzania.

  Wakichangia muswada wa marekebisho ya sheria ya utalii ambao uliwasilishwa na waziri wa habari, utalii, utamaduni na mcihezo, Abdillahi Jihad Hassan ilibidi upite kwa kura kutokana na wajumbe hao kutokukubaliana katika kifungu hicgo kinachosomeka kuwa.

  “Kifungu cha 23 b. (3) mtu yeyote anayefanya biashara ya utalii aliyeajiri mtu ambaye sio Mtanzania kutoa huduma iliyoelezwa chini ya kifungu cha (1) cha kifungu hiki lazima apate ruhusa ya maandishi kutoka kwa waziri baada ya kumthibitishia waziri kuwa hakuna mtu wa ndani (Zanzibar) wa kujaza nafasi hiyo.”

  Kambi ya wajumbe wasio na wizara wakiongozwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa walitaka kifungu hicho kiwe na jina la mzanziabri badala ya mtanzania ili kutoa upendeleo maalumu kwa wazanzibari.

  Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Abdillahi Jihad Hassan, Waziri wa Sheria na Katiba, Abubakar Khamis Bakari na Mwanasheria Mkuu Othman Masoud Othman wote kwa pamoja walitoa maelezo kwamba licha ya wao kutaka wazanzibari wawe na upendeleo katika sheria hiyo inayojadiliwa lakini sheria ya kazi inatamka neno mtanzania kwa hivyo kuwa na sheria nyengine inayotamka mzanzibari ni kuleta mgongano wa kisheria.

  Mwanasheria Mkuu alikwenda mbali zaidi na kuelezea kuwa hali hiyo inaweza ikasababisha Tanzania bara wakatunga sheria ambayo itadhibiti wazanzibari na kwamba hivi sasa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo Zanzibar ni sehemu yake zinaelekea katia soko huria.

  “Mheshimiwa Mwenyekiti sio kama hatutaki ibakie Zanzibar lakini kuwa na sheria mbili tofauti inaweza kuleta matatizo na sio lazima kuwa na sheria katika utekelezaji wake” alisema mwanasheria huyo.

  Hali hiyo iliwalazimu wajumbe hao chini ya Mwenyekiti, Mgeni Hassan Juma aliyekuwa akiongoza kikao hicho kupiga kura ambapo wajumbe 47 waliokuwemo wakati huo walipiga kura ya ndio (Mtanzania) na hapana (Mzanzibari).

  Baada ya kupiga kura kwa kuinua mikono wajumbe 40 wakatoka sare kwa wajumbe 20 kuunga mkono na wajumbe 20 kukataa na kupelekea mwenyekiti kuamua kuitisha tena kura kwa njia ya wajumbe kuitwa majina mmoja mmoja, ambapo wajumbe wengine saba kuongezeka.

  Matokeo ya mwisho yaliosomwa na Katibu wa Baraza hilo, Yahya Khamis Hamad yaliipa ushindi upande wa serikali kwa wajumbe 22 kuunga mkono na 21 kukataa ambapo, wajumbe wawili waliharibu kura zao na wawili kuamua kukaa kimya.

  Wakati wa kuchangia mswada huo wajumbe wengi walisema kwamba ajira nyingi zimechukuwa na wageni katika mahoteli na kuwanyima haki wazanzibari fursa ya kufanya kazi hata zile ndogo ndogo na kutaka serikali iweke sheria kali ya kudhibiti hali hiyo.

  Mwakilishi wa Jimbo la Kitope (CCM) Makame Mshimba Mbarouk alitoa mfano wa Dubai na nchi za Ulaya ambapo ni vigumu kupata ajira kwa mtu asiyekuwa raia na kwamba serikali ya Zanzibar imekosa udhibiti hata vitambulisho vya mzanzibari vinapatikana kwa wageni kutoka nje ya Tanzania.

  Alisema wageni kutoka nje ya Tanzania wamekuwa wakipewa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi (ZANID) na kuvitumia vibaya vitambulisho hivyo mahotelini kwa kufanyia uhalifu jambo ambalo bado serikali imekaa kimya kuhusiana na suala hilo licha ya kuwa mara kwa mara matukio ya kihalifu kuripotiwa katika vyombo vya habari na polisi.

  “Wageni kutoka Kenya wana vitambulisho vya mzanzibari wakati wananchi wa kitope katika jimbo langu watu wa makunduchi wanalilia vitambulisho hawapewi leo anakuja mgeni kutoka mbali napewa kitambusliho na anafanya kazi…wageni hawa watakuja kutuponza maana uhalifu umezidi sana kila siku utasikia huyu kanyongwa, huyo kapigwa, huyu kachinjwa” alisema kwa hasira mwakilishi huyo.

  Naye Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa alisema hata nchi za zilizoendelea zimeweka sheria kama hizo za kuwapa kipaumbele wananchi wake kufanya kazi kabla ya kuwapa wageni hivyo sio aibu kwa Zanzibar kuweka kiengele kinachomtambulisha mzanzibari katika ajira.

  Jussa alisema haoni sababu yoyote ya serikali kukataa kuweka neno mzanzibari badala ya mtanzania hasa kwa kuzingatia suala hilo halileti mgongano wa kisheria kwa kuwa serikali ina haki ya kutunga sheria zake bila ya kuingiliwa na lolote.
  Wakichangia mswada huo baadhi ya wajumbe walitishia sekta ya utalii ifutwe kutokana na kuendelea kuharibu maadili ya mzanzibari na kutafuta vyanzo vyengine vya mapato ya nchi kuliko kuharibu maadili ya nchi.

  Walisema wamesema maadili ya mzanzibari yamepotea kabisa kutokana na sekta ya utalii kuachwa bila ya kushughulikiwa na kuwekewa mipango madhubuti ya kuweza kuendeleza utalii wenye kufuata mila, silka na utamaduni wa mzanzibari.

  Baada ya kupitishwa mswada huo kwa kura Mwenyekiti wa baraza la wawakilishi ameakhirisha kikao hicho hadi jumanne baada ya kumalizika sherehe za pasaka
   
 2. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bara tunatunga sheria ya umiriki ardhi. Ardhi imilikiwe na mtanganyika tu na leseni za biashara kwa bara zitolewa kwa watanganyika tu! Hapo ndo tutaheshimiana make nchi kavu haitawatosha watajenga hadi baharini.
   
Loading...