Zanzibar: Moto wateketeza mabanda 100 ya wafanyabiashara soko la Mwanakwerekwe

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,353
Mabanda 100 ya wafanyabiashara katika soko la Mwana Kwerekwe Zanzibar yameteketea kwa moto.

-----------
moto18.jpg


Moto mkubwa ulioibuka joni hii katika soko kuu la Mwana Kwerekwe Zanzibar umeangamiza zaidi ya mabanda 100 ya vyakula na nguo na kusabisha hasara kubwa ya mamilioni ya fedha.

Moto huo umeweza kuteketeza mabanda hayo huku wamiliki wakishindwa kuudhibiti kutokana na upepo ambao baadhi ya wafanyabiashara hao wakiongea na ITV wamesema chanzo kikubwa cha moto huo ni jalala la taka likuwepo pembeni mwa soko hilo na vikundi vya mamantilie kudharau na kuchoma moto ndio uliosababisha kuteketezwa kwa mabanda hayo.

Wakati wafanyabiashara hao wakitoa sababu za jalala la taka kamishna msaidizi wa kikosiu cha zimamoto Zanzibar Haji Gora amelaumu baadhi ya watu kuchoma moto maksudi na kusababisha hasara hizo ambazo ni za mamilioni ya fedha na kuwataka wafanyabiashara hao kuwa na utaratibu wa kujilinda wenyewe na sio kusubiri zimamoto wafike.

Huu ni moja ya moto mkubwa uliokumba Zanzibar ambapo hasara yake ni kubwa na ni athari kubwa kwa wafanyabiashara hao wadogo ambao tegemeo lao kubwa ni biashara hiyo ya vyakula na mitumba ambavyo karibu vyote vinatoka Tanzania Bara.


Chanzo:
ITV
 
Mtoa mada acha kupotosha watu mabanda gani 100, ya upande gani, 100 yenyewe soko zima hayafiki leo unapotosha tu hapa. Haya thibitisha kwa picha ili nikose cha kuandika tena.
 
Mtoa mada acha kupotosha watu mabanda gani 100, ya upande gani, 100 yenyewe soko zima hayafiki leo unapotosha tu hapa. Haya thibitisha kwa picha ili nikose cha kuandika tena.
Nimesikia mwenyewe breaking news ITV wakisema zaidi ya mabanda 100
 
Hata upo uwezekano ikawa ni hujma mana yale mabanda pale ni wapemba watupu ndo wanajitafutia riziki,
 
Labda meza ndio zimeteketea kwa wingi lakini hazifiki hata 50, mabanda ni machache
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom