Zanzibar: Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Semeni Hamis Vuai, azikwa

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
71
75
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Husein Ali Mwinyi amewaongoza viongozi, wanachama wa CCM na wananchi mbali mbali katika Mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Semeni Hamis Vuai leo Jumapili 29 Agosti, 2021 katika kijiji cha Tunguu Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini.

Viongozi wengine waliohudhuria katika Mazishi hayo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Abdallah Juma Sadala, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa CCM Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka, baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na viongozi wa ngazi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake.

Marehemu Semeni Hamis Vuai amefariki jana Jumamosi 28 Agosti, 2021 kitika hospital ya Rufaa Mnazi Moja mjini Zanzibar alipokua akipatiwa matibabu.

Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
IMG-20210829-WA0119.jpg
IMG-20210829-WA0123.jpg
IMG-20210829-WA0117.jpg
 
Siasa ya Tz mbwana Raia wa Tanganyika anakiwa Rais Zanzibar,na Raia wa Zanzibar anakuwa Rais Tanganyika.
Hii ndio blander aliyoifanya Nyerere!
 
Back
Top Bottom