Zanzibar: Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar asema SMZ kufanya kazi na Serikali ya Uingereza katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kidunia

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
608
1,540
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema Serikali ya Zanzibar imekubali kufanya kazi pamoja na Serikali ya Uingereza katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kidunia, likiwemo suala la madawa ya kulevya, kwa lengo la kuendelea kuilinda Zanzibar na uhalifu huo.

Mheshimiwa Othman ameyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Msaidizi Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bwana Rick Shearn, wakati balozi huyo alipofika kwa ajili ya kujitambulisha kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ofisini kwake Migombani, Mjini Unguja hivi leo.

Balozi Shearn ameonesha azma ya Serikali ya Uingereza kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye masuala kadhaa, likiwemo hilo la kupambana na uhalifu unaovuuka mipaka ya mataifa.

Mheshimiwa Othman amesema bado kuna mambo yanaendelea kuiumiza dunia hasa suala la madawa ya kulevya na ufichwaji wa fedha za kihalifu.
“Serikali imekubaliana kupitia vyombo mbalimbali vinavyohusika na usimamizi wa sheria, uchunguzi, usimamizi wa kodi pamoja na vile vinavyosimamia maeneo makuu ya kuingia Zanzibar, kufanya kazi pamoja na Uingereza kwa lengo la kudhibiti uhalifu huu wa kidunia,“ alisema Makamu huyo wa Kwanza wa Rais, akiongeza kwamba Balozi Shearn ameahidi kutoa ushirikiano katika kuvijengea uwezo vyombo hivyo pamoja na kutanuwa wigo wa ushirikiano na vyombo vya kimataifa.

Sambamba na hilo, Uingereza imeahidi pia kuongeza nguvu ili kuboresha uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Othman amekutana na muwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Bi. Shalin Bahugana, ambaye ameihakikishia Serikali ya Zanzibar mashirikiano ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inaendelea kuwa vyema katika masuala mbali mbali ya kiafya na maisha kwa vijana wake.

Mwakilishi huyo amesema wamejipanga kuja na mkakati maalum wa kuwasaidia vijana kutokana na changamoto za kimaisha na za kiuchumi kwa kutoa taaluma juu ya kujenga maisha yao.
“Sisi katika UNICEF tumeandaa mpango mkubwa kuhusiana na utoaji wa taaluma juu ya lishe bora, jambo ambalo limekuwa tatizo kwa wananchi walio wengi kujisimamia katika suala zima la ulaji, na hivyo kupelekea kukosa jamii iliyo bora,“ alisema Bi Bahugana.

Kwa upande wake, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amemuhakikishia mwakilishi huyo wa UNICEF kuwa Serikali itaendelea kuungana nao pamoja katika kuhakikisha jamii ya Zanzibar inakuwa na ustawi mzuri, hasa katika suala la afya.View attachment 1775727View attachment 1775728View attachment 1775729

IMG-20210506-WA0016.jpg
 
Safi sana ACT,

wengine wako ubelgiji wanalelewa huko!

Jengeni Zanzibar yenu hakuna mtu kutoka nje atakuja kuijenga Zanzibar.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema Serikali ya Zanzibar imekubali kufanya kazi pamoja na Serikali ya Uingereza katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kidunia
Kupambana na uhalifu ni kazi ya Polisi. Vyombo vya usalama wakiwemo Polisi wapo chini ya serikali ya muungano. Sasa hapa serikali ya Zanzibar inahusika vp?

Au mimi ndio mshamba/kilaza wa somo la uraia?
 
Kupambana na uhalifu ni kazi ya Polisi. Vyombo vya usalama wakiwemo Polisi wapo chini ya serikali ya muungano. Sasa hapa serikali ya Zanzibar inahusika vp?

Au mimi ndio mshamba/kilaza wa somo la uraia?
Mwenyewe nashangaa,hawa wazanzibar wana kiburi kipindi hiki.Nyerere aliliona hili Tatizo LA Siku Mzanzibar akiwa Rais wa Muungano halafu akaliacha hewani kama Jakaya alivyo fanya kwenye Katiba.

Akili za viongozi wa kiafrika wanazijua wenyewe.
 
Back
Top Bottom