Zanzibar: Maafisa Tehama na Wakuu wa Vitengo watakiwa kuwa wabunifu

Ojuolegbha

Member
Sep 6, 2020
32
125
22 SEPTEMBA 2021

Na Raya Hamad – Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

Maafisa Tehama na wakuu wa vitengo wametakiwa kuwa wabunifu na kushirikiana katika majukumu yao ya kazi ili kuendana na kasi iliyopo ya ukuwaji wa teknologia ulimwenguni.

Mkurugenzi Mipango, sera na utafiti Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Bi. Daima Mohammed Mkalimoto ameyasema hayo leo wakati akizindua mafunzo kwa maofisa tehama na wakuu wa vitengo wa ofisi hiyo na taasisi zilizochini yake kwenye ukumbi wa mkutano wa ofisi hiyo Migombani.

Amesema serikali mtandao inatakiwa kuwa hai muda wote katika kutoa ushirikiano ili iwe ni suluhisho la kiutendaji katika mabadiliko na kufanya masuala ya tehama kuwa rahisi na kuwa na mfumo mmoja wenye tija kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Nae mkufunzi wa mafunzo hayo Ndugu Ali Abdi Ali kutoka Serikali Mtandao amesema maafisa tehama ili waendane kasi ya mabadiliko ya mawasiliano ni muhimu wawe wanapatiwa mafunzo ya mara kwa mara jambo ambalo litapelekea kuwa umakini katika utendaji wao wa kazi.

Aidha washiriki wa mafunzo hayo waishukuru Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kuomba muendelezo wa mafunzo hayo ili kuwa weledi zaidi na kufahamu maendeleo ya mawasiliano ya tehama View attachment 1948564 View attachment 1632319556376_DSC_3327.JPG
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom