Vyombo vya habari hivi karibuni vimeripoti juhudi mpya za serikali yetu ya Tanzania kupitia Waziri Mahiga katika kujaribu kuleta suluhu mpya nchini Burundi. Tumeshuhudia Waziri Mahiga akianza mazungumzo na viongozi wahusika wa serikali iliyopo madarakani na wapinzani, hata viongozi wa nchi jirani. Binafsi, nakubaliana na uamuzi huu wa serikali yetu kwani sisi kama majirani tuna wajibu wa kusaidia kuleta suluhu kwa kinachoendelea Burundi, maana kwa jinsi hali inavyozidi kuwa mbaya nchini Burundi, nasi tunaathirika sana kama mtu mmoja mmoja au kama Taifa kiuchumi, kiusalama na kuendelea kubeba mzigo wa wakimbizi wanaofurika kila siku nchini mwetu. Burundi na majirani zetu wote wakiwa salama, nasi Tanzania ndio salama yetu. Burundi na majirani zetu wasipokuwa salama, tutatumbue kwamba sisi Tanzania hatuko salama. Sina shaka na uzoefu wa Balozi mkongwe Mahiga katika jukumu hili la utatuzi wa migogoro na kuleta amani maana ndio kazi zake na nina imani kwamba atafanya kazi nzuri.
Mazingira ya mzozo wa Burundi na huu wa kwetu wa Zanzibar yanalingana kwa kiasi fulani, tofauti ni kwamba Burundi kuna mauaji wakati Zanzibar hakuna mauaji, angalau kwa sasa, na pishilia mbali tuombe Mungu yasitokee. Tofauti nyingine ni kwamba wananchi walio wengi wa Burundi hawakubaliani na namna serikali ya Nkurunziza ilivyoingia madarakani, na wameamua kuchukua hatua kwa kuonyesha kutoridhishwa kwao kwa kupaza sauti zao, kwa maandamano, na njia nyingine ambazo serikali haikubaliani nazo. Polepole hadi tumefika hapa tulipofika. Mazingira yaliyopo Zanzibar ni kama yalivyoanza Burundi, yaani polepole, wananchi wanalalamika chini chini hadi kuna siku nao watapaza sauti na mwishowe hali itakuwa ngumu kuidhibiti. Tujiulize huu uvumilivu wa wananchi wa Zanzibar utadumu kwa muda gani? Na je kilichopo ni uvumilivu kweli au kitu kitu kingine?
Tanzania inajulikana kwamba ni kisiwa cha amani, juhudi za Balozi Mahiga ni ushahidi mmojawapo wa hili, hata Rais mstaafu wa awamu ya nne Rais Kikwete amefanya mengi katika kuleta amani katika eneo hili la Afrika Mashariki na Maziwa Makuu. Tuutumie uzoefu huu wa wanadiplomasia wetu kama akina Mahiga, JK, Membe, Mkapa na wengineo ili tuinusuru Zanzibar. Kwa uzoefu tulionao katika kutatua migogoro ya nchi za jirani hili la Zanzibar lisitushinde.
Chonde Chonde viongozi wote wakuu mpime nafsi zenu, mjitathimini, mumuogope Mungu na kisha mchukue hatua za haraka na za haki mmalize mgogoro na hali ya sintofahamu inayoendelea viziwani Zanzibar kwa sasa. Sioni mantiki ya kukimbilia kutatua mzozo wa Burundi ili hali Zanzibar hali ni tete.
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Marais wote wastaafu wa Muungano na wale wa Serikali ya Zanzibar, Mawaziri wote wastaafu pamoja na wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wale wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, pamoja na Maspika waliopo na wale waliostaafu. Hii fursa ya kuuthibitishia ulimwengu na kutembea vifua mbele kwamba tatizo la Zanzibar limekuja na tumelimaliza na sasa ni historia. Tusiipoteze hii fursa.
Bunge la Jamhuri ya Muungano limeshazinduliwa na baraza jipya la mawaziri limeshaapishwa na kuanza kazi kwa kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu, sasa kauli mbiu hii sasa ielekezwe Zanzibar. Uchumi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa unategemea sana utalii, na tatizo linaloendelea Zanzibar limeathiri sana sekta ya utalii, Mnafamu safari ngapi za watalii zimefutwa baada ya hali hii kujitokeza? Maana yake ni kwamba wafanyakazi wa mahotelini, melini, katika ndege wachuuzi wa mitaani na wananchi wa kawaida Unguja wanalia njaa, kwa kuwa idadi ya watalii imepungua sana. Hakuna mtalii anayetaka kwenda mahali ambapo hana uhakika wa usalama wake.
Chondechonde viongozi WOTE wa nchi hii msikae kimya, kila mmoja wenu katika nafsi zenu CHUKUENI HATUA MARA MOJA KWA MASLAHI YA WATU WA ZANZIBAR NA TANZANIA KWA UJUMLA