Zanzibar kuzuia uvutaji sigara hadharani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar kuzuia uvutaji sigara hadharani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Oct 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Imeandikwa na Khatib Suleiman, Zanzibar; Tarehe: 18th October 2011


  SHERIA ya Afya ya Jamii ya mwaka 1936, itafanyiwa marekebisho makubwa na kuongezwa baadhi ya vipengele kikiwemo cha kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika mikusanyiko ya watu.

  Waziri wa Afya, Juma Duni Haji alisema hayo jana wakati akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi wa Chake Chake, Omar Ali Shehe (CUF).

  Omar alitaka Serikali ieleze athari za sigara kwa jamii na mikakati iliyopo ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara hadharani.

  Duni alikiri kuwepo kwa madhara makubwa ya sigara kwa binaadamu kwa zaidi ya watu wanaovuta ambao huathirika mapafu na sehemu nyengine za mwili wa binadamu.

  Alisema kazi kubwa inayofanywa na wizara kwa sasa ni kuipitia Sheria ya Afya ya Jamii ya Mwaka 1936 na kuifanyia marekebisho ambayo suala zima la uvutaji wa sigara hadharani litashughulikiwa.

  "Wizara ya Afya ya Jamii inafahamu athari za sigara kwa wavutaji na tumekuwa tukitoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu madhara ya sigara," alisema Duni.

  Alisema Wizara ya Afya ya Jamii itashawishi Wizara ya Fedha ili iweke masharti makali ya kutoza kodi kwa bidhaa zote za sigara zinazoingia nchini ikiwemo kudhibiti matumizi ya sigara.

  "Mheshimiwa Naibu Spika tutafanya ushawishi kwa Wizara ya Fedha ili ushuru sigara na bidhaa zake upande kwa lengo la kudhibiti matumizi ya sigara," alisema. Hata hivyo, Duni alisema Serikali itaendelea kutoa elimu kuhusu madhara yanayotokana na uvutaji wa sigara na hatari zake kwa binadamu.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nchi ya Zanzibar itaelekea wapi? Sasa hakuna kuvuta Sigara hadharani Mimi sio Mvutaji lakini hii itaashiria nini baadaye?

  Hawataki Vinywaji kwahiyo hawataki pesa za kitalii

  Sasa hawataki sigara ukiangalia kodi serikali ya Zanzibar inayopata kutokana na Sigara ni kubwa kweli zaidi ya Mauzo ya Karafuu

  Labda wameona Mafuta yapo Pemba
   
 3. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Wanaelekea kubaya, hata wanaume mwishowe watavaa hijabu.!!!!!!!!!!!!
   
 4. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wajenge bustani maalumu wakavutie huko
   
 5. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,552
  Likes Received: 1,605
  Trophy Points: 280
  bustani za wavutaji fegi,

  hii kwa hisani ya TCC...
   
 6. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,552
  Likes Received: 1,605
  Trophy Points: 280
  uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya ya mvutaji na yeyote aliyekaribu na mvutaji wkt sigara ikivutwa.

  chukua hatua.
   
 7. black sniper

  black sniper JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2015
  Joined: Dec 10, 2013
  Messages: 5,824
  Likes Received: 2,489
  Trophy Points: 280
  Duniani kote wanapinga vita uvutaji wa sigara sehemu nyingi tu hasa kwenye watu wengi, mbona sigara zilikuwa zinavutwa kwenye mabasi zamani lakini sasa yamepitwa na wakati? Ni sawa tu, kuna nchi zingine wameenda mbali zaidi ukiwa umebeba watoto kwenye gari ukavuta sigara unapigwa faini
   
 8. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,552
  Likes Received: 1,605
  Trophy Points: 280
  hii sheria tokea mwaka 1936 haijafanyiwa marekebisho...

  itakuwa imepitwa na wakati.
   
 9. mzenjiboy

  mzenjiboy JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2015
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 834
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii story ni ya mwaka 2011, na huyo Juma Duni si waziri wa afya tena.

  Hii mada imehusu nini kuletwa hapa, au kila linalofanywa na Zanzibar ijapokuwa jema kwenu njie huwa baya ????
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2015
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Waziri akitoka wizarani na matamko yake yanakufa?
   
Loading...