Zanzibar kuwa na Sarafu/Currency yake 'Zanzibar Dinar' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar kuwa na Sarafu/Currency yake 'Zanzibar Dinar'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Funge, Feb 18, 2012.

 1. F

  Funge JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 585
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Zanzibar ina:
  Serikali yake
  Raisi wake
  Bendera yake
  Wimbo wake wa taifa
  Bank kuu- bank ya watu wa zanzibar
  Katiba yake
  Jeshi lake la ulinzi
  Kilicho baki ni kuwa sarafu ya zanzibar.
  Wito kwa wawakilishi: hakikisheni nchi inakua na sarafu yake.
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hili ni wazo zuri sana. Kushare same currency na watu wa bara tunakuwa hatuwatendei haki wazanzibar.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  all the best znz
   
 4. faizah

  faizah Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Yaap wana akili huku bara kila aliyedai utanganyika aliitwa msaliti
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ni wazo zuri sana kwa Zanzibar kuwa inajitegemea kimapato na kuwa na sarafu yake. Siku hizi tunaogopa kuuongelea Muungano sheria inasema uuongelee tu kwa kuudumisha na si kuuachisha.
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mkuu zomba,
  Nini faida ya kuwa na separate currency maana EU na mataifa mengine yenye uchumi imara zaidi kuliko Zenj wanakimbilia kuwa na common currency? Pia EAC wanataka kuwa na common currency huko mbeleni! Tujuzane pls! Maelezo yako yawe ya kiuchumi na sio ya kishabiki/kisiasa zaidi!
   
 7. F

  Funge JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 585
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwani members wa EU, wamepata faida gani?. Greece, Portugal wamepata faida gani katika hilo. Labda tujiulize pia kwanini UK wamekataa katakat kujiunga na single currency.
   
 8. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Hiyo Dinar kama sarafu ya huko uarabuni,hawa jamaa wanavyopenda kuutukuza Uarabu,mimi naomba tu wauvunje muungano ili tuone mpambano kati ya watumbatu,wamakunduchi na hao akina Jussa
   
 9. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kiukweli waznz waachiwe nchi yao waende zao,wakiendelea kung'ang'aniwa kero zinaongezeka.
  Mwal Jk alishawahi kusema"Mataifa makubwa yakitafuta kuungana ili kuimirisha kiuchumi,nchi maskini zinaomba kutengana"
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Feb 18, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo Zenj wana sababu kama za UK au vipi? Kama ndio ni sababu zipi? Tukiachana na mambo ya UK, EU, EAC, etc ni faida gani za kiuchumi ambazo Zanzibar itaipata kwa kuwa na separate currency vs common currency? Tujuzane jamani, maana wengine mambo ya kiuchumi hatuyafahamu kwa uzuri!!
   
 11. F

  Funge JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 585
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tunachokataa ni political union, inayotufanya tuwe watwana wa watanganyika. Kama ni kushirikiana kiuchumi, mbona tanganyika inashirkiana na nchi nyingi tu.
   
 12. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,108
  Likes Received: 7,366
  Trophy Points: 280
  Ulaya karibia wote wana-share currency moja,
  Sembuse sisi Na Zanzibar??????!!!!
  Watu wanafikiria East Africa kua na sarafu moja, mkuu unafikiria utengano???!!!
   
 13. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Sasa kama kiongozi mkuu wa wanaharakati wa Zanzibar wa kupinga Muungano ni Sheikh Bassaleh unategemea nini?
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  hahahahahaaaa.....hizi akili za akina Jussa za ajabu sana hizi.
  Mi nilifikiri mnataka kuwa na something like zenjipesa, kumbe ni dinar? Hopeless!!

  Badala ya kuhangaika kutafuta kujitoa kwenye muungano kwa kutumia mitandao, kwa nini msiwatumie wabunge na wawakilishi wenu ambao mpaka sasa wanaonekana ni wanafiki wakubwa wa swala la muungano?

  Mnapenda porojo sana nyie viumbe.
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,588
  Likes Received: 18,571
  Trophy Points: 280
  Mkuu Funge,
  Zanzibar ina Serikali yake ya SMZ,
  Raisi wake
  Bendera yake
  Wimbo wake wa taifa
  haina Bank kuu yake, bank ya watu wa zanzibar ni benki tuu kama NBC sio central bank, haina gavana, haina sarafu na haitambuliwi popote hata hapa bara tuu haipo!.

  Japo Zanzibar ina Katiba yake ila haina Jeshi lake la ulinzi, wale JKU ni mgambo tuu kwa tafsiri ya jeshi, hata KMKM sio polisi kweli.

  Zanzibar haiwezi kuwa na sarafu yake kwa sababu Zanzibar sio nchi, haina dola? Nchi ni Tanzania ndio yenye dola, na Zanzibar ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani!.
   
 16. e

  ejogo JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Scotland nao wanataka wawe huru toka UK.
   
 17. U

  Userne JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kweli umesema, manake hata tukivuka bahari kwenda kununua mchele shinyanga ima kyela tutaenda na pesa ya kizenj, na sio pesa yao ya madafu!
   
 18. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Still EU members bado wameretain currency zao, Kroner, Deutsche Mark, franc amid euro
   
 19. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Northern Ireland washatoka.

  Hakuna kinachowazuia wazanzibari!
   
 20. M

  Mnyaturu Member

  #20
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yote ni yale yale tunawatakia kilala kheri.
   
Loading...